Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
MABINGWA wa soka Tanzania, Yanga, leo wanajitupa kwenye Uwanja wa Estádio Sagrada Esperança mjini Dundo mbele ya watazamaji 8,000 kupambana na wenyeji GD Sagrada, katika mechi ambayo inaweza kuwaacha wenyeji wakiwa kwenye msiba mzito.
Yanga inahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili iweze kufuzu kwa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya ushindi wake wa mabao 2-0 ilioupata jijini Dar es Salaam katika mechi ya kwanza ya raundi ya tatu.
Wachezaji raia wa Zimbabwe, Donald Ngoma na Thabani Kamusoku ambao walikosa mechi ya kwanza, leo watakuwa uwanjani kuongeza nguvu ili kuihakikishia timu hiyo ushindi muhimu na kufuzu kwa hatua hiyo adhimu.
Soma zaidi hapa => http://www.fikrapevu.com/yanga-kupeleka-msiba-kwa-sagrada-mjini-dundo-leo/