Uwanja wa Taifa: Vodacom Premier League VPL, Yanga 1 SC Vs 0 Mbao FC

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Katika Ligi Kuu Tanzania Bara VPL, leo Yanga SC, kukipiga na Mbao FC katika dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

Mchezo wa leo unatabiriwa kuwa wa ushindani kufualitia kumbukumbu ya mchezo wa awali ambapo Mbao FC waliibuka kwa ushindi wa 2-0.

Kwa sasa ligi ikiwa ukingoni tayari bingwa ameshapatika kwa Simba SC kunyakua Kombe hilo kabla ligi kumalizika rasmi, huku Azam FC hadi sasa ikiwa nafasi ya pili kwa kuizidi Yanga alama saba imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Yanga.

Yanga inayoshika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, inahitaji kushinda mchezo huo,ili kumaliza rekodi mbaya ya kucheza michezo tisa bila ya kushinda ikiwemo michezo sita bila ya kufunga bao.

FB_IMG_1526974679328.jpg
IMG_20180522_151831_480.jpg

Naam wakati wowote mpira utaanza

0' Mpira umeanza kwa Yanga kushambulia vilivyo lango la Mbao FC

5' Yusuf Mhilu alitaka kuwanyanyua wana Yanga kwa shambulizi lake lakini haikuwa hivyo

10' Yanga SC 0-0 Mbao FC uwanja wa Taifa.

Mchezo hauna kasi sana kwa pande mbili ingawa Yanga wanajitahidi kulifikia lango la Mbao FC

Wanachukua Mbao FC..lakini mpira wanapoteza na kuchukua Yanga

12' mchezaji Buswita anakosa bao la wazi kwa mpira wake kupaa lango la Mbao FC

18' Daud anashindwa kukaa vizuri kwenye lango la Mbao FC hivyo kushindwa kukwamisha mpira wavuni

23' Bado milango ni migumu Yanga SC dhidi ya Mbao FC.

25' Mchezaji wa Mbao FC anaunawa mpira ni faulo...Inapigwa na Kamusoko

28' Gooooooooaaaal, Yanga wanaandika bao la kwanza kufuatia Free Kick ya Kamusoko

Yanga SC 1-0 Mbao FC

35' Amos anapiga kona lakini golikipa wa Yanga anapangua na wanachukua Yanga sasa.

40' Kombo anakwenda mbele na mpira. Lakini Youthe Rostand golikipa anawahi mpira ule

42' Kamusoko anaumia anatoka nje..Na anaingia tena baada ya matibabu

44' Ndikumana anapiga shuti na kutoka nje ya lango la Yanga SC

45' Mpira ni mapumziko uwanja wa Taifa ambapo Yanga wako mbele kwa goli moja dhidi ya Mbao FC

Kipindi cha lala salama kimeanza..Mabadiliko kwa Yanga SC

Anatoka Yusuf Mhilu na nafasi yake inachukuliwa na Matheo

48' Matheo anapiga shuti kali..Lakini ni goal kick..!

Mbao wanapiga kona..Lakini haijazaa matunda.

55' Ndaki anakwenda kwenye benchi anaingia Kevin upande wa Mbao FC

58' Mwasa anapiga shuti na kuwa kona ya Nne...Inapigwa kona ambayo haikuzaa matunda upande wa Mbao FC

Njinja anapiga mpira mbele na kuondosha hatari zote lango la Yanga

65' Mbao FC wanashindwa kuandika bao baada ya wachezaji wa Yanga kuzubaa

Ni faulo kuelekea Yanga SC..Inapigwa nje.

69' Emmanuel anakwenda kwenye benchi na anainga Mwashiuya upande wa Yanga

Nafasi kwa Mbao FC..Lakini wanapoteza kwa kupaka sana rangi

Buswita anapiga shuti kali..Lakini linashindwa kulenga lango la Mbao FC

75' Daud anakwenda kwenye benchi anangia Paul Godfrey upande wa Yanga

79' Mwashuiya anakosa goli la wazi..Ilikuwa nafasi nzuri kuandika bao la pili.

Inapigwa shuti golikipa Youthe anadaka na kuanza kwa mchezaji wake

83' Yanga SC 1-0 Mbao FC uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam

Wakati wowote mpira utamalizika hapa uwanja wa Taifa..Mwamuzi anaangalia saa yake.

90' Naam mpira umekwisha uwanja wa Taifa ambapo Yanga wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbao FC ikiwa ni ushindi wao wa kwanza baada ya kupita mechi tisa mfululizo katika michuano yote
 
Wakuu, Leo mida hii ya SAA 04:00 jioni Yanga Sc na Mbao fc toka Mwanza wanachuana vikali.
So Yanga ataendeleza uteja mbele ya Mbao hali yakuwa yupo nyumbani au Yanga atalipiza kisasi..
Thus tubaki hapa tupeane Updates kuhusu hii mechi.

 
Back
Top Bottom