mwembemdogo
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 2,282
- 1,252
Mie nadhani wakati umefika Kwa Wizara ya habari kusimamia vilivyo chaguzi za viongozi wa vyama vya michezo hapa nchini.Nashauri hivyo kutokana Na TFF kukaa kimya wakati Klabu ya Yanga Kwa makusudi imemfanyisha mazoezi mchezaji Kessy ambaye ana mkataba Na Klabu yake ya Simba.TFF hiyo hiyo ikijua kabisa kuwa Klabu ya Yanga haikuwa Na kamati ya Utendaji bado ikaruhusu ijiundie kamati batili iliyosimamia Uchaguzi wake Na Rais wa TFF anautangazia umma eti anaipongeza klabu ya Yanga kufanya uchaguzi huku akijua dosari za uchaguzi huo. Wakati umefika Wizara iangalie viongozi wanagombea uongozi katika vyama wawe wanaupeo sio vilaza.