Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,810
Kesho Yanga watatupa karata yao dhidi ya Club Africain ya Tunisia. Kwangu hii ni mechi ngumu kuliko ile ya Al hilal. Yafuatayo ni mafungufu ambayo km kocha hajayafanyia kazi basi itakuwa ngumu kusonga mbele.
1.Kutengeneza mashambulizi kwa taratibu( slow). Warabu wakiwa ugenini huwa wanapenda kuipoozesha "game". Sasa km Yanga wataingia na staili ya "slow" km tulivyowazoea basi biashara itakuwa imeisha.
Yanga wanatakiwa kushambulia kwa kasi Ili kuweze kupata ubora wa Morison anaependa mpira wa nipe nikupe kwa kasi hapo ndipo huwa anapata mwanya wa kulazimisha timu pinzani kufanya makosa na kuweza kupata penalt au faulo nje ya 18.
2.Wawe makini na shambulizi la kushitukiza( Counter attacks). Mechi mbili na Al hilal Yanga walifungwa magoli mawili yanayofanana tena na mchezaji mmoja. Goli la Okra dhidi ya Simba ilikuwa ni counter pia. Ni km kocha ameshindwa kuwaelekeza wachezaji jinsi ya kuchukua tahadhari wakati wanapoenda mbele kushambulia. Kwenye Counter shape ya timu huwa inakaa ovyo (Shaghalabagala).Wachezaji wanaenda kukaba huku wamerundikana km mafungu ya nyanya. Wakipigwa chenga wote wanapotea. Na nadhani Club Africain watakuwa wamezifatilia kwa makini mechi za Yanga na kubaini haya niliyoyasema.
3. Udhaifu sehemu ya kiungo mkabaji na beki wa kati. Hili kila mtu analijua hakuna haja ya kuongea sana.
4. Mashambulizi yote kupitia kwa Mayele. Unapomtegemea mchezaji mmoja ndo afunge unairahisishia timu pinzani kuunda mkakati wa kumzuia hasa unapokutana na timu bora.Simba kwa mfano asipofunga Mosses Phiri Chama,Sakho,Okra, watafunga.
5. Idadi ndogo ya wachezaji kuingia eneo la mpinzani. Yanga wanaposhambulia huwa wanakuwa wachache eneo la mpinzani na hivyo kuwarahisishia wapinzani kuokoa mipira kwa urahisi au krosi nyingi kukosa mtu wa kumalizia.
Mimi haya ndo niliyoyaona,karibuni tuendelee kuwapa ushauri.