dindilichuma
JF-Expert Member
- Dec 19, 2015
- 1,719
- 2,671
Tumekua tukisikia kila baada ya uchaguzi Malalamiko ya walioshindwa kwenye uchaguzi husika. Ni nadra baada ya uchaguzi kutosikia maneno kama tumeibiwa kura, tume haikuwa huru n.k
Huwa najiuliza sana kwanini kila uchaguzi unapoitishwa Malalamiko huwa yaleyale na hata wapinzani huingia kwenye uchaguzi wakiwa wanajua hali halisi ila baada ya uchaguzi tunaanza kuyasikia haya Malalamiko ya siku zote?
Huwa inasemwa dalili za ukichaa ni kufanya jambo lilelile kwa njia zilezile ukitarajia matokeo tofauti. Hiki ndicho kinachofanywa kwenye siasa zetu tunafanya mambo yaleyale kwa mazingira yanayoshabihiana na tunatarajia matokeo tofauti.
Kwanini vyama vya upinzani havina nia ya dhati kuiondoa CCM madarakani?
Kwanini sasa hivi badala ya kuunganisha nguvu na kuhakikisha suala la katiba na hata ikishindikana basi tume ya uchaguzi tu vinapiganiwa kwa nguvu zote na akili zote?
Kwanini kunakua na hoja nyingi ambazo kiuhalisia hazitausaidia upinzani kuingia madarakani 2020? Mfano kwata anayowachezesha Makonda na akina Wema nakuambieni itafika 2020 tutaona tume ileile.
Mimi ningeuomba upinzani kama itafika 2020 kukiwa na tume hiihii basi uambieni umma mapema kwamba mtashindwa uchaguzi au msishiriki kabisa, kwasababu mkija na malalamiko ya miaka yote baada ya uchaguzi tutawapuuza na kuwaona mnadalili ya ukichaa.
Ipiganiwe tume huru ya uchaguzi na mabadiliko yote yatatokea.
Napata shaka na viongozi wa upinzani kama kweli ni watu sahihi? Kama kweli wanataka mabadiliko? Kama simapandikizi wa CCM ambao wanahakikisha upinzani hauingii madarakani kwa kisingizio kilekile kila mwaka (kuibiwa kura, tume ya uchaguzi)
Ili mtuaminishe kuwa kutakua na mabadiliko 2020 tunaomba muondoe kwanza visingizio ili wapiga kura wapige kura kwa kujiamini la sihivyo mtafanya watu wengi wasiende kupiga hata kura kwa kuwa mwishoni mtawaambia kura ziliibiwa.
Kama nikweli ziliibiwa nini kinafuata? Au ndio tumekaa tukisubiri ziibiwe tena 2020 kwa mazingira yaleyale. Napata mashaka huenda huwa kura haziibiwi ila hiki ni kisababu cha kutolea aibu ya kushindwa na kuwapa matumaini wanachama. Kama zingekua nikweli zinaibwa basi upinzani ungepambana kuziba mianya hiyo lakini la hasha.
Kuna utoto mwingi sana kwenye siasa za nchi hii, vyama vyetu haviko serious hata kidogo.