TUNAWEZA kabisa kuandika, kuwa safari ngumu ya kisiasa kuelekea 2015 inaanza rasmi leo kule Dodoma. Na hatma ya safari, kama ni njema au mbaya hutegemea na mguu wa kuanzia safari hiyo.
Ukianza na mguu mbaya, basi, ndio imetoka hiyo. Mitaani wanasema; " Imekula kwako!". Bunge ni mhimili muhimu sana katika mihimili mitatu ya dola; Sheria ( Bunge), Utekelezaji ( Rais) na Hukumu ( Mahakama).
Na nchi huongozwa na siasa. Na bungeni ndiko unakochezwa ' mchezo wa siasa'. Bila shaka ye yote, Spika Wa Bunge, ni mtu muhimu sana. Na ndio sababu ya ' mnyukano' huu tunaoushuhudia sasa katika kumpata Spika wa Bunge.
Na mwaka huu, kurunzi zinamulikia chama tawala, CCM, na Chama Kikubwa cha Upinzani bungeni, CHADEMA. Ni mtihani mgumu kwa Rais Jakaya Kikwete na Dr Willibrod Slaa kwa nafasi zao tofauti. Maana, Kikwete ndiye Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi. Harakati za kumpata mgombea Uspika kutoka CCM, kwa kiasi kikubwa zitategemea namna Kikwete atakavyotanguliza hekima, busara na hata kuwa na ujasiri wa kufanya maamuzi magumu itakapobidi.
Dr Slaa naye ameibuka kuwa mtu aliyejipatia umaarufu mkubwa kutokana na kuongoza kwa umahiri mkubwa, kampeni za Urais kwa tiketi ya CHADEMA. Kwa nafasi yake ya Ukatibu Mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, hata kama kwa kukaa kiti cha nyuma, kwa kutanguliza hekima na busara, anatazamiwa kuongoza harakati za kumpata mgombea nafasi ya kuwa kiongozi wa upinzani bungeni kutoka chama chake.
CCM ina mtihani mgumu:
Chama hicho kimeshinda na kufanikiwa kupata nafasi ya kuunda tena Serikali huku kikiwa na majeraha mengi. Masikini, tumesikia, kuwa kuna waliokuwa wakiishi na majeraha. Wanataka kwenda kuponya majeraha. Kwa kutumia dawa gani? Tutajua mbele ya safari. Na wasipopewa nafasi ya kwenda kutibu majeraha? Ndio hivyo tena, wataendelea kuishi na majeraha. Huu ni mtihani mgumu kwa CCM na Jakaya Kikwete.
Naam. Miaka mitano iliyopita haikuwa mepesi kwa CCM na hususan ndani ya Bunge. Kashfa za ufisadi na kuibuka kwa makundi miongoni mwa wabunge wake kumepelekea kwa kiasi kikubwa kuporomoka kwa umaarufu wa chama hicho na hata Rais aliyekuwa madarakani. Tukiwa na majibu mkononi, leo tunaweza kabisa kusema. Weredi na uzoefu wa kisiasa wa Jakaya Kikwete umemsaidia yeye ( Kikwete) na chama chake kubaki madarakani. Kama Dr Slaa angeingia kwenye mbio za Urais tangu mwezi January mwaka huu, basi, huenda leo simulizi zingekuwa ni nyingine kabisa.
Naam. Kuna makosa makubwa yamefanyika ndani ya chama hicho, CCM . Na CCM wenyewe wanakiri ukweli huo.
Wanachama wa CCM na wapenzi wa chama hicho wanasubiri kwa hamu sana kuona ni mguu gani Kikwete ataanza nao hii leo.; Mguu mzuri au mguu mbaya? Kwa maneno mengine, sehemu ya hukumu kwa CCM kutoka kwa umma kuelekea 2015, inaweza kuanza kutolewa Dodoma kuanzia leo.
Chama Cha Mapinduzi bado kinajivunia ' K' tatu; Ni chama Kikongwe, Kikubwa na Kinachotawala. Hivyo basi, bado kina hazina ya uzoefu. Kama CCM itajibu maswali ya mtihani wa kumpata mgombea Uspika haraka haraka, hivyo basi, kukosea. Basi, hata kusahihisha kosa hilo baadae nalo litakuwa ni kuongeza makosa. Kwa umma, kwa sasa, ni heri CCM iliyo madarakani na yenye kupambana na ufisadi na maovu mengine kuliko CCM iliyo madarakani na yenye kupambana na wabunge wapambanaji wa ufisadi kutoka upande wa pili; kwa maa ya kambi ya upinzani. Hilo la mwisho likitokea, basi, kuporomoka kwa umaarufu wa CCM kutakuwa ni sawa na wa nyumba ya karata.
Nini kitatokea kwenye chumba cha mtihani hii leo?
Kuna Scenario zifuatazo;
1. Nimesoma gazetini kuwa nafasi ya Unaibu Spika inagombaniwa na Jenister Mhagama. Hana mpinzani kutoka CCM. Tafsiri yake; kama CC ya CCM itapitisha jina hilo tu, basi, kwa kuzingatia gender balance, Spika hawezi kuwa mwanamke. Hivyo basi, majina kama Anne makinda, Anne Abdalah na Kate Kamba yatawekwa pembeni.
2. CC ya CCM inapeleka majina mawili ya wagombea Unaibu Uspika, moja la Jenister na lingiine la mwanamme, nani? Hatujui kwa sasa. Hapo itatoa mwelekeo wa vita ya Uspika, kwamba Spika anaweza kuwa mwanammke au mwanamme.
3. Kuna mgombea ‘atakayechinjwa' ndani ya CC kabla majina kupekekwa kwenye 'caucus' ya chama. Hapa yaweza kutoa tafsiri kuwa kundi zima la mgombea huyo litakuwa limechinjwa. Hapa kuna simulizi yenye mafundisho. Kabila la Wazaramo ni mkusanyiko wa koo tofauti. Miongoni mwa koo za Wazaramo ni koo ya Wabena. Koo hii imepata jina hilo kutokana na desturi ya koo hiyo ilipokwenda vitani.
Waliposhinda na kuwateka adui, basi, hawakuwaacha adui waendelee kushika pinde zao na mishale. Waliivunja vunja. Kuvunja kuna maana ya " Kubena' kwa Kizaramo. Ndio asili ya jina la koo hiyo. Na ndio chimbuko la neno " Libeneke" kwa maana lillovunjika. Ndugu yangu Michuzi amechangia kuukuza msamiati huo.
Ndio, Afrika wanasiasa ni wagumu sana kumaliza tofauti zao. Mchana watasema; " Sasa basi, yaishe, tunachimba shimo na kufukia pinde na mishale yetu". Usiku wanarudi na kufukua mashimo walimofukia pinde na mishale yao. Wataendeleza Libeneke! Koo ya Wabena Uzaramoni ilikuwa na watu wenye busara sana, waliijua dawa; kubena ( kuvunja) pinde na mishale ya adui, halafu ndio mazungumzo ya amani yanapoanza.
4. Jina la mgombea Uspika laweza kutoka nje kabisa ya wagombea wanaofikiriwa na wengi kwa sasa.
5.Jakaya Kikwete anaweza kufanya maamuzi magumu ambayo hakuna aliyeyatarajia, hivyo basi, kwa kasi kurudisha imani na umaarufu wake ambao kwa sasa umepungua. Na zaidi, kama mwanadamu, Jakaya Kikwete anafahamu, balaa kubwa linaloweza kumtokea maishani, ni kwa CCM kumfia mikononi mwake. Atafanya kila anachopaswa kufanya kuepusha dhahma hiyo isije ikamfika.
5. Majina mawili au matatu ya wagombe Uspika yatatoka leo na kesho kufikishwa kwenye ' caucus' ya CCM. Wabunge watapelekewa majina hayo. Laweza pia kuwa ni jina moja tu. Saa kumi jioni hiyo kesho, majina au jina hilo litafikishwa ofisi za Bunge ili kesho kutwa likapigiwe kura.
6. Na itafika siku kwa JK kupendekeza jina la Waziri Mkuu. Tayari kuna Mawaziri Wakuu Wastaafu wengi na wenye kuliongezea taifa gharama. Mizengo Pinda anaonekana kuwa na nafasi ya kubaki alipo.
CHADEMA:
Nao wana mtihani. Baada ya uchaguzi mkuu kumalizika, sasa CHADEMA kina lazima ya kuishi ' maisha ya kawaida ya kisiasa'. Na CHADEMA sasa ni taasisi kubwa. Kama ilivyo CCM, kwamba ndani ya CCM kuna Wana-CCM na wa upinzani, vivyo hivyo, CHADEMA ya leo ina Wana- CHADEMA na Wana- CCM ndani yake. Ni mtihani kwa Dr Slaa na wenzake.
CHADEMA wamempeleka Marando kuwania Uspika. Kama CCM wataboronga katika mchakato wao, basi, Mabere Marando anaweza akakalia kiti cha Uspika. Hiyo itakuwa ' Bingo' ya kisiasa kwa CHADEMA. Na kwenye karatasi hilo lawezekana.
Freeman Mbowe alipoulizwa kuhusu nafasi ya kuwa kiongozi wa upinzani bungeni akatamka ; Itaamuliwa kwenye Chama. Freeman Mbowe ni mzoefu katika siasa. Ametoa jibu hilo kwa umakini mkubwa. Lakini kuna Zitto Kabwe pia, naye anawania kuwa kiongozi wa upinzani bungeni.Tafsiri yake, dalili za uwepo wa makundi ndani ya CHADEMA.
Kama Freeman na Zitto watapambanishwa mbele ya wabunge, nahofia, kuwa Freeman anaweza kushindwa vibaya. Lakini, kama ' Hilo litaamuliwa na CC ya CHADEMA' , basi, Freeman anaweza akatoka salama , kugombea na kushinda kwa kishindo kura za wabunge wa kambi ya upinzani.
CUF nao namna gani?
Kule Unguja bado kuna pilau la ushindi linaliwa , maana, Unguja wameshinda wote ati! Maalim Seif na Dr. Shein wote marais, mmoja wa kwanza mwengine wa pili, kisha wanabadilishana. Mmoja akenda bara, aliyebaki kisiwani ndiye Rais, akirudi aliye kisiwani akenda zake bara, huko bara yeye Rais na aliyebaki kisiwani rais! Ndo mambo ya Unguja hayo.
Naam. CUF nao wanakuja, kwa staili mpya; ' Ki-ZenjiBara'!
Maggid
Iringa,
Jumatano, Novemba 10, 2010