Yanayotokea CHADEMA yametokana na nini?

Yanayotokea CHADEMA yametokana na nini?

Alexism

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2011
Posts
3,423
Reaction score
2,046
Wanajamvi kwa takribani mwaka sasa na kupita tunaona nakusikia pamoja na kusoma kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari kuhusu kuwepo migogoro katika chama cha Demokrasia na Maendeleo. Nataka leo wanajamvi tujadiri na mwisho tuje na suluhu na migogoro hii inayotokea katika chama cha CHADEMA. Migogoro hii inayotokea ikiwa inawahusisha viongozi wa juu wa CHADEMA, BAVICHA na wafaasi wa chama.
Ukweli kabisa CHADEMA kuwa na migogoro hii ambayo haina tija kwa chama bali kukibomoa chama inabidi itatuliwe mapema lasivyo CHADEMA haitahaminika tena mbele ya wananchi wa watanzania ambao walikuwa wanaendelea kujiunga na chama.
NAOMBA TUJADIRI KWA MALENGO MAZURI NA YENYE TIJA YA KUKINUSURU CHAMA.
 
Chanzo cha migogoro kiko nje ya chadema, yaani kuna watu ndani ya chadema wanatumiwa kukibomoa.
 
Migogoro ndani ya CHADEMA inatokana na ulafi na kukosa uzalendo ndani ya nchi. Vijana wengi wa Tanzania ni watafutaji, na hali yao ya kiuchumi ni mbaya sana. Wanatumiwa na mafisadi walioko nje ya CHADEMA kwa kupewa hela ili kukivuruga chama. Kuna haja ya kupambana na ufisadi kwa nguvu zote. Bila kupambana na ufisadi, rasilimali za Tanzania hazitamnufaisha mtanzania.
 
Hivi kwa nini watu wengi humu JF hawaamini kama migogoro chanzo chake kinaweza kuwa ndani ya CHADEMA? CHADEMA ni taasisi kwa hiyo kila taasisi ni lazima iwe na migogoro na ndiyo maana kwenye taasisi za kielimu kunafundishwa elimu ya utatuzi wa migogoro!!
 
tatizo vijana tunataka kustarehe bila kufanya kazi so anapokuja mtu anakuambia fanya hv na hv, kwa sababu ya tamaa wanakubali bila kutafakari athari ya wanachotaka kukifanya. NI TAMAA TU.
 
Mkuu kuna Kaskazini na Masalia.Hawa kaskazini ndo wanataka kujifanya wanahatimiliki na chama.Masalia hawa ndo wale wa pande zingine ambao wanatengwa kwenye mambo ya chama.Nadhani mwanga umeupata
 
ni kawaida katika jumuia inayokusanya watu wa calibre tofauti tofauti, hali hiyo pia inapaticana lumumba, cuf nk. kudiffer, hakuepukiki, ila mnayamalizaje ndio issue. na pia kwa sababu ya nature ya jumuia yenyewe, obvious kuna watu nje ya jumuia wanapenda hiyo, kwa hiyo hutumia muda mwingi kuchochea migogoro kama hiyo. kwa hiyo hiyo haishangazi, familia tu ikiwa na mshikamano utaona sumu zinavyorushwa kutoka nje, alimradi waone mnafarakana, hamuishi kwa amani, itakuwa chama kinachotaka kufanya mageuzi! kazeni buti cdm, mengine yanakuzwa tu muendelee kuhisi kuwa mna matatizo makubwa, hata jirani zenu hawana maelewano kihivyo, wanachekaga tu wakitoka nje ili msiwatambue
 
Hela,mshiko,rushwa,ada,nauli,hongo,takrima,billi nk.Kila sehemu ina jina lake!raia wakitembezewa hiyo kitu wanachafua hali ya hewa.in short tamaa ya short cut life.
 
Mkuu kuna Kaskazini na Masalia.Hawa kaskazini ndo wanataka kujifanya wanahatimiliki na chama.Masalia hawa ndo wale wa pande zingine ambao wanatengwa kwenye mambo ya chama.Nadhani mwanga umeupata

Sasa wewe mtu wa CUF hapa unahusikaje?
 
Wanajamvi kwa takribani mwaka sasa na kupita tunaona nakusikia pamoja na kusoma kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari kuhusu kuwepo migogoro katika chama cha Demokrasia na Maendeleo. Nataka leo wanajamvi tujadiri na mwisho tuje na suluhu na migogoro hii inayotokea katika chama cha CHADEMA. Migogoro hii inayotokea ikiwa inawahusisha viongozi wa juu wa CHADEMA, BAVICHA na wafaasi wa chama.
Ukweli kabisa CHADEMA kuwa na migogoro hii ambayo haina tija kwa chama bali kukibomoa chama inabidi itatuliwe mapema lasivyo CHADEMA haitahaminika tena mbele ya wananchi wa watanzania ambao walikuwa wanaendelea kujiunga na chama.
NAOMBA TUJADIRI KWA MALENGO MAZURI NA YENYE TIJA YA KUKINUSURU CHAMA.

Kwani wewe huijui kazi ya USALAMA wa CCM a.k.a Usalama wa TAIFA ni nini? Ikisaidiana na ZITO ambaye ni rafiki (Mshirika) wa ZOKA?
 
Back
Top Bottom