Yanayonikera kwenye daladala

Kero ninyingi sana aisee watu kuongea Siri za familia zao bila staha yani mambo ya ndani kabisa bila aibu.

Halafu kuna ile unakuta unaharaka zako dereva anaishtua shtua kama anaondoka hivi, akitaka kuondoka tu konda utamsikia ngoja ngoja chukua huyo

Kurudiarudia kile kitendo hua nikero kubwa sana kama unaharaka zako
 
TENA HAPO GARI IMEJAA NA MPO VITUO VYA NJIANI
 
HAHAHAAAAA WE JAMAA UNADHARAU SANA AISEE
 
Nakasirika sana konda anapolazimisha mrudi nyuma wakati gari limejaa na anaona, anawasubirisha kituoni na mnachelewa safari
 
Nakasirika sana konda anapolazimisha mrudi nyuma wakati gari limejaa na anaona, anawasubirisha kituoni na mnachelewa safari
Kuna konda mmoja wa gari la simu 2000 -Masaki alikuwa anakomaa abiria warudi nyuma wakati gari limejaa alipofika kwa MTOGOLE akazira akashuka chini akamwambia derava usiondoe gari kisha akaenda kukaa mbali duuh ilikuwa asubuhi watu tunawahi job ilibidi abiria washuke waende kumbembeleza kama mtoto kisha akakubali kurudi huku anacheka daaaah yaani daladala Bongo tabu saaana.
 

HAHAHAHAAAA NYIE JAMAA YANI MPO 70+ MNACHEZEWA NA WATU WAWILI MNGEWACHAPA VIBOKO HADI WASHANGAE THEN MNATAFUTA GARI LINGINE.

MBEZI ILITOKEAGA GARI LIMETOKA MAKUMBUSHO KWENDA KIBAMBA SHULE KUFIKA MBEZI MWISHO WAKAANZA KUPAKIA NA ABIRIA WAMECHOKA, GARI LIMEJAZA UPYA HADI WAMESIMAMISHA MISTARI MIWILI NA HAWAONDOKI.

ABIRIA WALIWAKAMATA WAPIGADEBE NA KONDA NA DEREVA WAKAWAPIGA MAKOFI HADI POLISI WAKAINGILIA KATI.
 
Dereva kupiga mziki wa singeli...

Aaaarrggghhh... Aisee aisee aisee.... Nachukia vibaya mno.
Hahaha niliwahi kusafiri kwenda kusini huko dereva mwenyewe ni muimbaji wa hizo masingeli bwana bwanaaa ,tulichezewa singeli hadi nikajutaa ,sikuwahi kupanda basi dereva ni muimbaji [emoji23]
 
Hahaha niliwahi kusafiri kwenda kusini huko dereva mwenyewe ni muimbaji wa hizo masingeli bwana bwanaaa ,tulichezewa singeli hadi nikajutaa ,sikuwahi kupanda basi dereva ni muimbaji [emoji23]
πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…