Yanayojiri Bungeni Dodoma Leo Mei 16 2016

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
BUNGE LA 11, MKUTANO WA 3

KIPINDI CHA MASWALI NA MAJIBU

Swali: Serikali za awamu zilizopita ziliahidi kujenga barabara yaTanga - Saadani hadi Bagamoyo itaanza kujenga kwa kiwango cha lami.
Majibu: Barabara hii iko kweye mradi wa Kikanda inayoanzia huko Kenya na dhamira ya kuijenga barabara hii yenye Km178 mara baada ya kupatikana kwa fedha.

Swali: Je taifa kukosa MCC inamadhara gani kwenye mradi wa mradi wa umeme vijijini yaani REA
Swali: Hakuna hata senti moja ya MCC iliyokuwa iko kwenye mradi wa umeme vijijini wa REA na waziri amekaa na watu wa MCC na wizara ilifanya vikao na wizara ya nishati ya Marekani MCC ilikuwa ikitoa fedha za miradi ya maji, na miradi ya barabara. Fedha za MCC kwenye umeme zilikuwa hazivuki theluthi moja. Watanzania wanatakiwa waelewe

Swali: Miradi ya uchimbaji wa madini katika milima ya Songwe je wananchi wamepewa elimu juu ya miradi hii
Majibu: Kwa mujibu sheria ya madini namba 95 (1b) Sheria humpa kibali cha uchimbaji wa madini na kampuni inakaribia kukamilisha taratibu na wanafanya mazungumzo ili kuona namna ya kulihamisha gereza la Songwe na watatoa elimu kwa wananchi

Swali: Serikali imeandaa makati gani wa kuwatia mbaroni watu wanaofanya vitendo vya kikatili kwa watoto?
Majibu: Serikali inamikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa namba maalumu ya kutoa taarifa za kiaharifu kwa watoto namba hiyo ni 116

Swali: Lini barabara ya kutoka Mhanila mpaka Kasulu itakamilika kama ilivyokuwa ahadi ya Mh Rais
Majibu: Ni barabara iliyopo chini ya Tanroads na kazi ya usanifu wa kina inafanyika na inadhaminiwa na benki ya uwekezaji Afrika.

Swali: Ni lini hospital ya Mkuranga na Mafia zitapata mashine za XRays
Majibu: Ni kweli hospitali ya Mkuranga ilikuwa haina XRay lakini sasa juhudi zimefanyika na hospitali imepata Xray na wizara inapanga ziara katika eneo la nyanda za juu kusini.

Swali:Ni kwanini Benjamini Mkapa Foundation wamejenga vituo vya afya mkoani Rukwa lakini serikali haijaweza kuvitumia vituo hivyo
Majibu:Bado taratibu za makabidhiano zinaendelea na pindi zitakapokamilika vituo vitaanza kutumika

Swali: Hospitali ya Nyamagana inahudumia zaidi ya wangonjwa laki 3 lakini haina vifaa kama XRays
Majibu: Halmashauri ya jiji la Mwanza imetenga jumla ya Milioni 100.34 kwajili ya kuboresha huduma katika hospitali ya Nyamagana

Swali: Kwakuwa sababu kuu za ufaulu duni ni mbinu mbovu na mikakati wa kujifunza, na waathirika wakuu ni watoto wa kike Je serikali ina mkakati gani?
Majibu: Ktk suala la miundombinu mibovu bajeti imelenga kuwafanya waalimu kuwa na mazingira mazuri, na mkoa wa Njombe umepewa kipaumbele, pia watoto wanakosa umakini kwasababu ya malezi mabovu katika ngazi ya familia.

TUNATAKA LIVE KIPINDI CHA hoja za wabunge Hayo majibu yalioandaliwa wachapishe. Kuikwepa hiyo live na ninachokiona hasa kwa zile kauli za Londoni. Kama sio woga wa hoja BASI NI HOJA ZA WOGA
 
Tatizo la huu uzi huwa maswali ya wizara yakiisha nao unaisha
 
Unaona kabisa kuwa wabunge hawa wako pale kuheza tu. Mfano swali la kwanza, jibu lake ni utani kuwa mtu huyu hayuko serious na ishu ya muulizaji. Nani alikuwa anajibu, Mbalawa au?
 
Back
Top Bottom