Yanayoendelea Duniani -Hali ya uchumi - Ushauri kwa Rais Samia.

Yanayoendelea Duniani -Hali ya uchumi - Ushauri kwa Rais Samia.

mwanamichakato

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2015
Posts
1,208
Reaction score
1,109
Tujifunge mikanda..Hali ya uchumi duniani kote si nzuri..Nchi yetu si kisiwa..Athali Za migogoro ya kivita duniani,Mivutano ya mataifa yanayoitwa matajiri,Tishio la vita kuu ya tatu ya dunia,Athari Za Wa Houthi wa Yemen ktk disruption ya Global trade..Scarcity ya Usd dola na mengine mengi..

Nashauri Tupunguze matumizi na kufuta au kusimamisha baadhi ya miradi .Tupunguze mishahara ya wanasiasa.Tupunguze vyeo vya kisiasa (Manaibu Waziri/Wakuu wa Mikoa,RAS/DAS).Tupunguze taasisi zenye majukumu yanayoshabihiana mfano (TIC,TANRADE,BRELA,EPZA,TIRDO,SIDO,etc)..

Nashauri tuepuke kuajiri au kuteua watumishi toka nje ya mfumo wa Utumishi wa Umma na kuwatumia watumishi ambao wamekuwa wakienguliwa na kuendelea kulipwa mishahara pasipo kutekeleza majukumu..Wale wanao vurunda wachukuliwe hatua kali Za kisheria na wakikutwa na hatia wafukuzwe kazi na kuondoa mzigo Kwa Serikali..

Kwa Heshima na unyenyekevu mkubwa namshauri Mh Mtukufu Rais wa JMT apunguze ukubwa wa Baraza la Mawaziri libaki dogo lenye kuwezesha mambo kwenda ili kupunguza mzigo wa gharama kubwa Za kuendesha Wizara nyingi ktk Hali iliopo sasa na baadae ..mfano tuwe na Wizara kitita:-

1:Wizara ya Fedha,Mipango,Uwekezaji na Maendeleo ya Uchumi

2:Wizara ya Usalama,Ulinzi na Mambo ya Ndani

3:Wizara ya Miundombinu,Uchukuzi,na Usafirishaji (Maji,Barabara,Umeme,Bandari,Airport)

4:Wizara ya Natural Resources (Madini,Oil and Gas,Misitu,Vivutio vya Utalii,Etc)

5:Wizara ya Haki,Katiba,Sheria,Utawala Bora,Maadili na Uadirifu

Wizara ya Elimu Bora,Sayansi Za Lisasi,Ubunifu,Ufahamu na Ufundi Stadi

Etc
 
Back
Top Bottom