Yametimia: Ugumu wa maisha umeanza kujitokeza

Yametimia: Ugumu wa maisha umeanza kujitokeza

watu wafanye kazi, tunataka gap la pato la mtanzania lisiwe kubwa na la mwenzake, kipindi cha JK. gap lilikuwa kubwa maana wafanyabiashara na wafanyakazi wa serikali walikuwa hawalipi kodi kwa kukwepa kodi halafu wafanyakazi waliachiwa Uhuru zaidi wa kufanya semina zisizo tija, kusafiri hovyo hovyo nk.

Unamsema jk hapo
 
Kwa hilo bongo ni kitendawili kigumu

Kwanini kila kitu unajipa negative attitude, watu wanasema ndoa ngumu, lkn bado zinafanyika, Singapore walibezwa lkn ni 1st world, jifunze positive response na thinking. Na hapo ulipo najua unasifia Rwanda kufanya vzr, ila kwako hutaki kukubali km utafika. Unajua kuwa ruvu juu na xhini kuna mabwawa makubwa ya kuhifadhi maji ili yasaidie wakati wa upungufu. Muhimbili walikuwa wanalala xhini, no more. Mikoa yt itakuwa na masuka ya msd. Namaanisha juhudi za kuyapata hayo kwa nchi nzima zishaonekana usizibeze
 
Kwanini kila kitu unajipa negative attitude, watu wanasema ndoa ngumu, lkn bado zinafanyika, Singapore walibezwa lkn ni 1st world, jifunze positive response na thinking. Na hapo ulipo najua unasifia Rwanda kufanya vzr, ila kwako hutaki kukubali km utafika. Unajua kuwa ruvu juu na xhini kuna mabwawa makubwa ya kuhifadhi maji ili yasaidie wakati wa upungufu. Muhimbili walikuwa wanalala xhini, no more. Mikoa yt itakuwa na masuka ya msd. Namaanisha juhudi za kuyapata hayo kwa nchi nzima zishaonekana usizibeze

Huwezi kumlazima ngamia kunywa maji
 
WANAOJIELEWA? vyakula bei juu!, maisha magumu, afu unasema unajielewa? UMERIDHIKA NA MAISHA NDUGU ANGALIA WALEMAVU WANAVYOTESEKA, MAMANTILIE,BODABODA, usijiangalie we binafsi
Tusitake kudanganyana, mama ntilie na Bodaboda walisha zoea maisha haya,na hawa sio wakepaji kodi,kwa Bodaboda bei ya mafuta sasa hivi imeimarika , kwa mama ntilie sasa hivi hakuna mfumuko Wa bei za bidhaa masokoni, hao walemavu wanateseka kwa lipi? Mkuu kama wewe ni wa lile kundi la walio kuwa wakikwepa kodi,kuhujumu uchumi, waliokuwa wakitegemea posho na perdiem za hovyohovyo ndio wanao lalamikia ugumu Wa maisha kwa sasa.
 
Magufuli anachotaka ni serikali kuwa na uwezo wa kusukuma uchumi katika makundi mbalimbali, mdhamini wa uchumi wa watu katika makundi yao ni serikali, haiwezekani kuwa na uchumi imara wa watu hali serikali haina pesa na njia pekee ya serikali kupata pesa ni kupitia kodi mbalimbali zinazolipwa.
 
Kipindi cha jk walitajirika sana hawa,sasa ni wakati wa kugawana mapato sawa,
 
Niliwahi leta uzi hapa nikisema watu wa mijini watakuwa na maisha magumu wakati Raisi akiendelea na juhudi zake za kubana matumizi na kuwabana wafanyabiasha katika kulipa kodi.

Niligusia licha ya juhudi hizi za Raisi ambazo zinapaswa kuungwa mkono, maisha ya watu wa mijini yatakuwa magumu na Magugufuli 2020 atapata kura zaidi kwa watu wa vijijini na si mijini.

Ushahidi ni taarifa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Mwananchi la leo ambalo limebeba habari ya wafanyabiasha kulalamika hali imekuwa ngumu kutokana na kubanwa kwenye kulipa kodi na pia wateja wao nao wanalia hali ngumu.

Narudia,kipindi kigumu cha mpito chaja na lazima tujiandae kwa hilo na tusipokuwa makini kitakuwa ni kipindi cha kudumu.

Soma habari kamili:
======

Wafanyabiashara K?koo walia, TRA yawajibu

By Jackline Masinde, Mwananchi

Kwa ufupi
Ugumu wa biashara wawatesa, miongoni mwao wakiri walikuwa wakikwepa kodi.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, wamelalamikia hali ngumu ya biashara zao tangu Rais John Magufuli aliopoingia madarakani na kasi ya kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi.

Wakizungumza na gazeti la Mwananchi katika mitaa ya Mchikichini, Aggrey, Kongo, Nyamwezi, Swahili, Msimbazi na Uhuru baadhi ya wafanyabiashara walieleza kuwa hali hiyo imeathiri shughuli zao kwa kuwa walizoea kusafirisha bidhaa kwa njia za panya.

"Tuseme ukweli tuna hali ngumu, biashara haiendi na hii inatokana na hali ilivyo ya udhibiti wa kodi, hivi sasa huwezi kupitisha mzigo wako bandarini kinyemela lazima 'ukamuliwe' kwanza," alisema Ben Mwasomola mfanyabishara wa nguo Mtaa wa Kongo.

"Mwaka huu Magufuli atatunyoosha, mambo hayaendi, kabana kila kona pamoja na yote zamani bwana siyo siri tulikuwa tunapita njia za chochoro lakini sasa hivi ngumu.

?Mlolongo ni mrefu hadi bidhaa yako ifike sokoni inachukua muda mrefu,? alilalamika Rogders Milambo.

Alifafanua kuwa, bidhaa kama nguo zimekwisha madukani kwa kuwa tangu walipoagiza miezi miwili kabla ya uchaguzi hawajaagiza mpaka mwezi Novemba walipoagiza ambazo mpaka sasa hazijaingia sokoni kutokana na shuguli ya kukamata makontena.

"Tunaamua kulala hatuna cha kuuza, tumeingia hasara wengine hapa mizigo imekwama. Pia, wateja wenyewe hawapo kila mtu analia maisha magumu," alisema Milambo.

Baraka Kikoti alisema hana hamu na awamu ya tano kwa kuwa imebana maeneo mengi jambo linalosababisha kuwapo na ugumu.

"Huyu baba kweli hii kasi yake inatuumiza wafanyabiashara, yaani ukweli ujue wengi humu bidhaa zetu zilikuwa zinapita juu kwa juu, hatukuwa na hali iliyopo sasa," alisema.

Mussa Mohamed alisema inachofanya Serikali siyo kibaya, ila kwa mfumo uliokuwapo zamani uliwafanya wafaidike lakini sasa kila jambo lazima lipitie mkono halali wa kodi.

"Ninachoomba, gharama za ushuru ziainishwe,isiwe kila mtu anajipangia bei yake. Ijulikane ni kiasi gani ambacho mfanyabiashara atakimudu," alisema Mohamed.

Kuhusu hali ya biashara katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka, wafanyabiashara hao walisema hali ni tofauti ikilinganishwa na mwaka jana.

"Sikukuu zingine kipindi kama hiki unakuta biashara ya nguo na vyakula imechanganya lakini kama unavyoona maduka maeupe hakuna wateja," alisema Rwanda Jonathan.

Wanaunuzi walizwa na gharama

Gazeti hili lilizungumza na wananchi waliokuwa wakinunua vitu mbalimbali sokoni hapo ambao walilalamikia bei za bidhaa kama vyakula na nguo.

"Hali ni ngumu kama hivi unaambiwa kilo ya mchele ni Sh1,800 hadi Sh2,000 maisha yenyewe ndiyo haya ya Magufuli, fedha hakuna yaani kiujumla sikukuu ya mwaka huu imekuja na ukata wa hali ya juu," alisema Paulina Petro.

Hadija Ibrahim alisema yanayotokea sasa yanatokana na uchaguzi wa mwaka huu uliokuwa wa kihistoria ambao ulijenga hofu miongoni mwa wananchi kiasi wengine kufunga biashara zao.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara sokoni hapo, Philimin Romano anakiri kuwapo kwa ugumu wa biashara katika kipindi cha baada ya uchaguzi na sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

"Najua ugumu uliopo sasa kwa wafanyabiashara, lakini hii ni kwa muda tunasubiri hadi kufika Januari mambo yatakuwa yamekaa vyema" alisema Romana.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alisema awali kulikuwa na upungufu kwa baadhi ya watendaji, jambo ambalo lilisababisha wafanyabiashara wengi kukwepa kodi na kunufaika zaidi wao kuliko Serikali.

Ni kipindi kigumu cha mpito kwa Wafanya Biashara wakwepa KODI, Kodi lazima ilipwe ili nchi yetu isonge mbele kimaendeleo, muda si mrefu sisi wananchi tutaanza kufurahia kikamilifu Matunda ya kodi..
 
WANAOJIELEWA? vyakula bei juu!, maisha magumu, afu unasema unajielewa? UMERIDHIKA NA MAISHA NDUGU ANGALIA WALEMAVU WANAVYOTESEKA, MAMANTILIE,BODABODA, usijiangalie we binafsi

Kwa hiyo wewe unataka watu wasilipe kodi au???
 
Maisha yatakua magumu kwa wale wote ambao walikua wanapaswa kulipa kodi lkn kiukweli walikua hawalipi kwakua walikwepa sasa wanaona shida kwakua walizoea vya kunyonga na vya kuchinja hawaviwezi.Walikua wakiishi kwa kodi za wafanyakazi ambao hawana namna ya kukwepa kodi kwakua kodi yao hukatwa kwenye mishahara hata kabla ya iliwafikia.Acha kuwe na usawa.
 
Tusitake kudanganyana, mama ntilie na Bodaboda walisha zoea maisha haya,na hawa sio wakepaji kodi,kwa Bodaboda bei ya mafuta sasa hivi imeimarika , kwa mama ntilie sasa hivi hakuna mfumuko Wa bei za bidhaa masokoni, hao walemavu wanateseka kwa lipi? Mkuu kama wewe ni wa lile kundi la walio kuwa wakikwepa kodi,kuhujumu uchumi, waliokuwa wakitegemea posho na perdiem za hovyohovyo ndio wanao lalamikia ugumu Wa maisha kwa sasa.
Kumbuka hawa wafanyabiashara ndio wanaotoa ajira zisizo rasimi kwa vijana wengi mitaani kwa kuwaajiri katika maduka,makampuni yao n.k.Pesa wanazolipwa vijana hawa ndio huzipeleka kwa mama lishe,kwa dereva wa boda boda n.k.Kwahiyo ukiwabana vizuri na wao wakaamua kufunga baadhi ya biashara zao au kupunguza wafanyakazi wao,hata huyu mama ntilie na dereva wa boda boda wataathirika pia.

Pia usisahau wamachinga wengi hutembeza bidhaa za wafanyabiashara hawa kwa makubaliano maalumu ya kibiashara hivyo wengi wao nao wataathirika kwani hutegemea kupata mzigo wa kuuza kutoka kwa wafanyabiashara hawa wakubwa na wa kati.

Vivyo hivyo,ukiwabana watumishi wa umma bila kuwaboreshea maslahi yao, maana yake ni kwamba watashindwa kutoa ajira zisizo rasimi kwa vijana wa mtaani kama vile vibarua vya ujenzi pale mtumishi anapojenga nyumba yake baada ya kulipwa posho au kutoka safari ya nje ya nchi n.k.

Kwa maana hiyo,bila serikali kutengeneza ajira na kuboresha maslahi ya watumishi wake,vijana wengi watakosa kazi na maisha yatakuwa magumu karibu kwa kila mtu kwani vipato vitapungua.
 
Kama kuna majipu ya kukamuliwa nchi hii ni wafanyabiashara. Wanakwepa kodi , wanafanya magendo , bidhaa fake yani ni shida.
 
Kwa taarifa yako akiboresha huduma za jamii, maji, umeme, madawa, watu mjini ndo wa kwanza kumpigia kura.

Lipeni tu kodi mlizoea kukwepa
 
Mbona sisi wafanyakazi huwa hatukwepagi hata sent I kila mwezi kila mwaka NO Weather
 
Back
Top Bottom