Yametimia: Ugumu wa maisha umeanza kujitokeza

Salary Slip

Platinum Member
Apr 3, 2012
49,068
151,315
Niliwahi leta uzi hapa nikisema watu wa mijini watakuwa na maisha magumu wakati Raisi akiendelea na juhudi zake za kubana matumizi na kuwabana wafanyabiasha katika kulipa kodi.

Niligusia licha ya juhudi hizi za Raisi ambazo zinapaswa kuungwa mkono, maisha ya watu wa mijini yatakuwa magumu na Magugufuli 2020 atapata kura zaidi kwa watu wa vijijini na si mijini.

Ushahidi ni taarifa katika ukurasa wa mbele wa gazeti la Mwananchi la leo ambalo limebeba habari ya wafanyabiasha kulalamika hali imekuwa ngumu kutokana na kubanwa kwenye kulipa kodi na pia wateja wao nao wanalia hali ngumu.

Narudia,kipindi kigumu cha mpito chaja na lazima tujiandae kwa hilo na tusipokuwa makini kitakuwa ni kipindi cha kudumu.

Soma habari kamili:
======

Wafanyabiashara K?koo walia, TRA yawajibu

By Jackline Masinde, Mwananchi

Kwa ufupi
Ugumu wa biashara wawatesa, miongoni mwao wakiri walikuwa wakikwepa kodi.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mitaa ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, wamelalamikia hali ngumu ya biashara zao tangu Rais John Magufuli aliopoingia madarakani na kasi ya kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi.

Wakizungumza na gazeti la Mwananchi katika mitaa ya Mchikichini, Aggrey, Kongo, Nyamwezi, Swahili, Msimbazi na Uhuru baadhi ya wafanyabiashara walieleza kuwa hali hiyo imeathiri shughuli zao kwa kuwa walizoea kusafirisha bidhaa kwa njia za panya.

"Tuseme ukweli tuna hali ngumu, biashara haiendi na hii inatokana na hali ilivyo ya udhibiti wa kodi, hivi sasa huwezi kupitisha mzigo wako bandarini kinyemela lazima 'ukamuliwe' kwanza," alisema Ben Mwasomola mfanyabishara wa nguo Mtaa wa Kongo.

"Mwaka huu Magufuli atatunyoosha, mambo hayaendi, kabana kila kona pamoja na yote zamani bwana siyo siri tulikuwa tunapita njia za chochoro lakini sasa hivi ngumu.

?Mlolongo ni mrefu hadi bidhaa yako ifike sokoni inachukua muda mrefu,? alilalamika Rogders Milambo.

Alifafanua kuwa, bidhaa kama nguo zimekwisha madukani kwa kuwa tangu walipoagiza miezi miwili kabla ya uchaguzi hawajaagiza mpaka mwezi Novemba walipoagiza ambazo mpaka sasa hazijaingia sokoni kutokana na shuguli ya kukamata makontena.

"Tunaamua kulala hatuna cha kuuza, tumeingia hasara wengine hapa mizigo imekwama. Pia, wateja wenyewe hawapo kila mtu analia maisha magumu," alisema Milambo.

Baraka Kikoti alisema hana hamu na awamu ya tano kwa kuwa imebana maeneo mengi jambo linalosababisha kuwapo na ugumu.

"Huyu baba kweli hii kasi yake inatuumiza wafanyabiashara, yaani ukweli ujue wengi humu bidhaa zetu zilikuwa zinapita juu kwa juu, hatukuwa na hali iliyopo sasa," alisema.

Mussa Mohamed alisema inachofanya Serikali siyo kibaya, ila kwa mfumo uliokuwapo zamani uliwafanya wafaidike lakini sasa kila jambo lazima lipitie mkono halali wa kodi.

"Ninachoomba, gharama za ushuru ziainishwe,isiwe kila mtu anajipangia bei yake. Ijulikane ni kiasi gani ambacho mfanyabiashara atakimudu," alisema Mohamed.

Kuhusu hali ya biashara katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka, wafanyabiashara hao walisema hali ni tofauti ikilinganishwa na mwaka jana.

"Sikukuu zingine kipindi kama hiki unakuta biashara ya nguo na vyakula imechanganya lakini kama unavyoona maduka maeupe hakuna wateja," alisema Rwanda Jonathan.

Wanaunuzi walizwa na gharama

Gazeti hili lilizungumza na wananchi waliokuwa wakinunua vitu mbalimbali sokoni hapo ambao walilalamikia bei za bidhaa kama vyakula na nguo.

"Hali ni ngumu kama hivi unaambiwa kilo ya mchele ni Sh1,800 hadi Sh2,000 maisha yenyewe ndiyo haya ya Magufuli, fedha hakuna yaani kiujumla sikukuu ya mwaka huu imekuja na ukata wa hali ya juu," alisema Paulina Petro.

Hadija Ibrahim alisema yanayotokea sasa yanatokana na uchaguzi wa mwaka huu uliokuwa wa kihistoria ambao ulijenga hofu miongoni mwa wananchi kiasi wengine kufunga biashara zao.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara sokoni hapo, Philimin Romano anakiri kuwapo kwa ugumu wa biashara katika kipindi cha baada ya uchaguzi na sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.

"Najua ugumu uliopo sasa kwa wafanyabiashara, lakini hii ni kwa muda tunasubiri hadi kufika Januari mambo yatakuwa yamekaa vyema" alisema Romana.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo alisema awali kulikuwa na upungufu kwa baadhi ya watendaji, jambo ambalo lilisababisha wafanyabiashara wengi kukwepa kodi na kunufaika zaidi wao kuliko Serikali.
 
watu wafanye kazi, tunataka gap la pato la mtanzania lisiwe kubwa na la mwenzake, kipindi cha JK. gap lilikuwa kubwa maana wafanyabiashara na wafanyakazi wa serikali walikuwa hawalipi kodi kwa kukwepa kodi halafu wafanyakazi waliachiwa Uhuru zaidi wa kufanya semina zisizo tija, kusafiri hovyo hovyo nk.
 
Wasiojielewa mjini ndo wataona anawabana lakini wengi wetu as tunaelewa iwe mjini iwe vijijini kote ni Tz. Na ukumbuke, kupanda na kuvuna haviendi pamoja, wakati wa kupanda ni dhiki sana na ikija mavuno watu hunenepa ...funga mkanda.
 
Kumbe wafanyabiashara ndo wanyonyaji wakubwa kwa mwananchi wa kawaida. Walipe kodi hawataki wakalime.
 
Wacha walie kulipa kodi ni wajibu tunataka elimu bure kwa watoto wetu pia huduma za afya bila kulipa kodi hizo huduma zitakufa,kodi ni wajibu,asiyetaka si afunge tu biashara yake.
 
Wasiojielewa mjini ndo wataona anawabana lakini wengi wetu as tunaelewa iwe mjini iwe vijijini kote ni Tz. Na ukumbuke, kupanda na kuvuna haviendi pamoja, wakati wa kupanda ni dhiki sana na ikija mavuno watu hunenepa ...funga mkanda.

WANAOJIELEWA? vyakula bei juu!, maisha magumu, afu unasema unajielewa? UMERIDHIKA NA MAISHA NDUGU ANGALIA WALEMAVU WANAVYOTESEKA, MAMANTILIE,BODABODA, usijiangalie we binafsi
 
kodi lazima ilipwe,itungwe sheria anayekwepa kodi atandikwe risasi.

tumechelewa inabidi tukimbie kwa kasi.

serikali ikusanye pia mapato ya kutosha kwenye utalii, madini,gesi na maliasili nyingine.
 
Hakuna vya bure lazima kodi zilipwe tu.

Kitakachofuata ni wafanyabiashara hawa kupunguza watumishi au kuwapunguzia mishahara.Magufuli asipoztengeneza ajira,kibao kitamgeukia.Hapo bado athari za kuwabana watumishi kimaslahi nazo zinakuja.
 
Zoeeni tu kulipa kodi, wa mjini tukipata kila kitu inavyotakiwa, dawa maji umeme barabara, JPM kura atapata.
 
Back
Top Bottom