CURRENT ISSUE
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 256
- 57
Ada imelipwa vizuri,na mtoto wangu hajaakutwa na hayo.Kilichoniuma ni kuwa huyu aliyeachwa ni mtoto wa jirani yangu ambaye mimi ndie niliyemtafutia hiyo shule.Hata kama kuna deni,sio kuwaacha watoto stendi kituoni.Maisha ya mtoto hayanunuliwi kwa pesa sh. 20,000/= ambayo hajamalizia.Hii ndio hoja yangu ya msingi
Mwenye kujua shule nzuri ya Primary tafadhali nijuze ili niweze kumshauri mzazi yule kufanya maamuzi magumu,maana toka muda ule amekuwa akinitaka nimpe listi ya shule nzuri.Nimekuelewa,
uongozi wa shule umekosea kutoa maelekezo kwa wenye magari kuwaacha vituoni wanafunzi wanaodaiwa bila kujali wamekwisha andaliwa kwenda shule. ilipaswa wawaeleze wazazi wanaodaiwa wasisumbuke kuwaandaa watoto mpaka wawe wamemaliza kulipa madeni yao yote.
ili kuepuka kadhia hii wazazi tujitahidi kuwa na kumbukumbu ya kulipa kwa muda stahiki ada za shule ama angalau kuwa na mawasiliano na uongozi wa shule tunapokuwa na mkwamo wa kiuchumi.
pia si vibaya kufikiria kutafuta shule nyingine ingawa hakuna shule isiyo na changamoto.
Kila la kheri.
Nimeshangazwa na utaratibu wa hawa wajasiriamali wenye shule za majina ya watakatifu.Watoto wameachwa stendi leo na gari ya shule ya St.Hellen kwa kile kinachodaiwa hawajamaliza ada ya shule.Nilipoona hivyo nilimuuliza dreva wa ile gari ya watoto kuwa kwa nini anawaacha,anasema ndivyo alivyoambiwa na boss wake.Imeniuma sana kwa sababu kuwaacha watoto kituoni kwa kosa la mzazi sio sawa.Uongozi wa shule ungetoa taarifa kwa wazazi husika kuwa leo wasiwalete watoto vituoni wataachwa.Kilichoniumiza ni kuwa;1.Huu uroho wa kupenda pesa bila kuthamini maisha ya watoto sio nzuri.2.Niliongea na mzazi ambaye mwanae naye amekutwa na dhahama hiyo,mzazi huyu alimwacha mtoto wake kituoni ambapo gari ya shule inawachukua akitegemea kuwa mtoto wake atachukuliwa kama kawaida,kumweleza kuwa mwanao yupo hapa kituoni ameachwa na gari ya shule alisikitika sana.Maana anasema hajawahi kupewa taarifa zozote na uongozi wa shule hata kama kuna deni hawezi acha kulipa ilikuwa ni taariifa tu.Ila kitendo walichokifanya cha kumwacha mtoto kituoni akishangaa shangaa ni kitendo kiovu na cha kukemewa na mamlaka husika.Mzazi huyu pamoja na mimi tumeanza zoezi la kutafuta shule yenye kuwajali watoto.Wadau naombeni msaada wenu.
Nimekuelewa,
uongozi wa shule umekosea kutoa maelekezo kwa wenye magari kuwaacha vituoni wanafunzi wanaodaiwa bila kujali wamekwisha andaliwa kwenda shule. ilipaswa wawaeleze wazazi wanaodaiwa wasisumbuke kuwaandaa watoto mpaka wawe wamemaliza kulipa madeni yao yote.
ili kuepuka kadhia hii wazazi tujitahidi kuwa na kumbukumbu ya kulipa kwa muda stahiki ada za shule ama angalau kuwa na mawasiliano na uongozi wa shule tunapokuwa na mkwamo wa kiuchumi.
pia si vibaya kufikiria kutafuta shule nyingine ingawa hakuna shule isiyo na changamoto.
Kila la kheri.
Issue sio deni,kwani shule mpya si unaingia gharama mara mbili vile.Ni usumbufu wa kuja kupotelewa na motto kisa mwalimu.Aliyewaacha ni dreva aliyeelekezwa na mwalimu mhusika kufanya hivyo.Nami nimeuona huo uzembe,leo hii nimewasiliana na shule moja inaitwa MARTIN LUTHER iliyopo Dodoma,naombeni kwa wenye taarifa zaidi za shule hii wanijuze.Maana huu uzembe wa staili hii ya hawa Watakatifu(ST.)umenichosha.Mzazi mlee mwanao na umpe elimu nzuri kama uridhi wa maisha yake....Sidhani kama wenye shule ni vichaa kuwaacha watoto wadogo stendi.... wazazi tunakera ufuatiliaji wa watoto kwenye mambo ya elimu na hata ada na inafikia mahali hata wenye shule wanaghadhifika. Najua huyo jamaa yako anataka kumhamisha mwanae ili kuficha kosa la kutokuwajibika kwake. Sio vizuri kuwahamisha watoto shule kutokana na mambo ya kipuuzi kama haya kwani unampa mtoto ugeni wa waalimu na marafiki ktk shule mpya. Mwambie apunguze hasira na akubali uzembe wa kuchelewesha mpunga wa wenye shule.... Tena mwisho wa mwaka kama hivi wazazi wengi tunahamisha watoto shule ili kukimbia madeni.
Issue sio deni,kwani shule mpya si unaingia gharama mara mbili vile.Ni usumbufu wa kuja kupotelewa na motto kisa mwalimu.Aliyewaacha ni dreva aliyeelekezwa na mwalimu mhusika kufanya hivyo.Nami nimeuona huo uzembe,leo hii nimewasiliana na shule moja inaitwa MARTIN LUTHER iliyopo Dodoma,naombeni kwa wenye taarifa zaidi za shule hii wanijuze.Maana huu uzembe wa staili hii ya hawa Watakatifu(ST.)umenichosha.