Yamenikuta; Kutema mate Tanga ni criminal case!

Yamenikuta; Kutema mate Tanga ni criminal case!

Kiluuj

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
692
Reaction score
278
Hii sio hadithi, yamenikuta hiyo jana.

Ni siku nyingi sijatembea Tanzania haswa Tanga. Kwa kawaida huwa ninatuma kupitia mabasi ya kutoka humu Mombasa hadi Tanga. Jana nikaamua niende mwenyewe.

Nilipofika Tanga mjini kumbe coaster za kwenda Mgwashi, Lushoto kwa wakwe zangu zimehamishiwa stendi mpya, KANGE. Kwa vile stendi yenyewe siijuwi ikabidi niliache gari langu na kupanda la abiria.

Baada ya dakika kama kumi hivi tukaingia Kange. Sasa kule kubanana kwa abiria nilipatwa na kizunguzungu, hivyo wakati wa kushuka mate yangu yakawa hayawekeki kinywani. Nikajaribu kumeza, ndio kikazidi. Ikabidi NITEME!

Ghafla nikashtukia nimebanwa nyuma! "Mbona unachafua mji?" Kumbe kutema mate mjini Tanga ni CRIMINAL CASE!
Ilinibidi nilipe 50,000 Tsh ndio niwachiliwe.

Niligharamika lakini I wish ingekuwa hivyo Kenya. Hongera Tanga.
 
Hongera Tanga. Hii ikisambaa kila mkoa, hasa Dar es Salaam itakua poa sana.
 
Mkuu hapo kwenye Kenya cjakuelewa....unamaanisha wakenya wanatema mate hovyohovyo sana?
 
Duuh ndio maana watu wana hasira, haya akija mja mzito kichefu chefu kimemshika pwaa; tayari watu washamkwida mama faini ya sh/50,000 sheria zingine bwana. Kwani kila saa watu wanatema mate kwa makusudi lundo limejaa umevumilia safari nzima walitaka uyameze ungeishia kutapika hiyo fine ingekuwa bei gani tena.

Upuuzi kama huu ndio unawafanya watu waone bora wafanye experiments tu na wengine ata kama uongozi wenyewe wa ovyo.
 
Huyo aliyechukuwa hiyo 50000 alikupa risiti?Na ulilipa hiyo PESA kwenye Ofisi ya serekali?Au ulitapeliwa?
 
Hebu, rudia tena uemesema?

Au naota hapa!

Ama ni!

Ngoja kwanza
 
Waja leo waondoka leo,siku hizi waja leo kisha walowea
 
Tangaa.. tangaa.. yarab toba,ndege pia kwa mwezi twaona mara moja sasa si balaa hili..??Tangaaaa,kunani paleee eeh mbona kila kitu kimekufaa.??by wagosi wa kaya!!nadhan hiyo ya kutema mate ni njia mojawapo ya kuinua Uchumi uliolala wa Viwanda na Bandari
 
Usafi ni muhimu kiukweli ila kwa hili la mate sijakupata vizuri maana kwa ssi ambao tumetumia stand ile hayajatukuta ila kama imeanzia kwako sawa.
 
Mmmh !! Yalinikuta Singapore nililipa fine 2 !! (moja ya kutema mate na ingine kutema chewing gm) !!
Lakini kuweka usafi ni bora na wajibu kwa jamii nzima!!
 
haa elfu50? kwa ushahidi upi?? niliwahi kukutwa moshi nakojoa nikamwambia mgambo anaushahidi gani kama mkojo ni wangu? kama vipi auzoe tukaupime maabara. akaishia kunisonya tuu
 
pole sana mkuu lakini si vyema kutema mate ovyo ovyo
 
Back
Top Bottom