Yamefia wapi maombi ya kumwombea Rais?

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
Miezi kadhaa ya mwanzo ya uongozi wa Mheshimiwa Rais kuna kipengele kilikuwa kimeongezwa cha "kumwombea Rais" katika Nyumba za Ibada, siku hizi hatukisikii, kimefia wapi kipengele hicho?

Au je, wanaona anayoyafanya sasa hayastahili maombezi? Ni wapi mkuu huyu kawakwaza viongozi hawa na waumini wao? Au huu basi tu ulikuwa ni utaratibu wa muda? Ni wapi pameenda ndivyo sivyo?

Nauliza tu..............
 
Bado tunaendelea na maombi, ila tatizo ni manuizo yanatofautiana. Humohumo kwenye waombaji kuna manuizo hasi na chanya, sasa sijui tunasubiri majibu.
 
Ungejiuliza mwenyewe kwamba Maombi Maana yake ni nini.Ungejua hili wala usingeuliza

Maombi sio lazima ukae kwenye mic na uropokwe kwa sauti kubwa,maombi ni siri ya moyoni,na maombi bora ni yale yanayotoka moyoni kwa mtu bila shinikizo.

Wangapi leo tunawaombea wazazi wetu waliofariki katika kila Ibada bila hata mtu mmoja kujua.Na hata mtu unaweza kuwa upo kwenye daladala ukamuombe Dua hata mlemavu tu aliepo njiani ili Mungu ampe wepesi tena unaomba kimya kimya bila mtu kujua.

Sasa maombi hayana sehem rasmi kwamba hapo ndio lazima mtu aombewe.Sehem za Ibada ni sehem Za ukumbusho wa Mungu ili tukiwa nje ya Nyumba za ibada tuendeleze yale Mungu anayotaka katika jamii zetu.

Mwenyezi Mungu hajaribiwi, nionavyo mimi kuna namna Allah wnamjaribu wana test wana joky wana tease.

Tangu ionekane mikono mitatu na vivuli na safari za ikulu kwa waliopita, wengi wamesoma alama mbaya.

Yule jamaa wa kanisa la uwokozi, mwenye jina la Ngwa... hajaropoka....Hivi mungu anawahusu nani kama sio sisi sote?

Tumuombeee mapapa yasimzonge rais lkn nae atuambie yanayomsibu

Ni
 
Ungejiuliza mwenyewe kwamba Maombi Maana yake ni nini.Ungejua hili wala usingeuliza

Maombi sio lazima ukae kwenye mic na uropokwe kwa sauti kubwa,maombi ni siri ya moyoni,na maombi bora ni yale yanayotoka moyoni kwa mtu bila shinikizo.

Wangapi leo tunawaombea wazazi wetu waliofariki katika kila Ibada bila hata mtu mmoja kujua.Na hata mtu unaweza kuwa upo kwenye daladala ukamuombe Dua hata mlemavu tu aliepo njiani ili Mungu ampe wepesi tena unaomba kimya kimya bila mtu kujua.

Sasa maombi hayana sehem rasmi kwamba hapo ndio lazima mtu aombewe.Sehem za Ibada ni sehem Za ukumbusho wa Mungu ili tukiwa nje ya Nyumba za ibada tuendeleze yale Mungu anayotaka katika jamii zetu.

iko vzr
 
Tunamuombea kila siku ila wakat ule wa uchaguz tulifanya maalumbjwa kuwa ni kipindi kigumu kwa sasa tunamuombea mmoja mmoja si kwa kutangaza jpili ila ijumaa tunataratibubza kuombea nchi na yeye yumo.
 
Back
Top Bottom