Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,278
- 8,868
Pazia la Ligi Kuu England linafungwa leo jioni kwa michezo yote 10 kupigwa katika muda mmoja, ambapo burudani zaidi ni kupatikana kwa bingwa katika michezo ya mwisho.
England inakuwa miongoni mwa ligi chache zilizomalizika hadi sasa kwa mshindi kujulikana baada ya mechi za mwisho wa msimu, ambapo Manchester City wanapewa nafasi kubwa kutokana na wingi wa mabao yao na kuwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu England.
Kabla ya michezo ya leo, Manchester City iko kileleni ikiwa na pointi 83, ikiwa na pointi mbili juu ya Liverpool, ambao wanaomba City ifungwe katika mchezo huo dhidi ya West Ham nao waishinde Newcastle leo ili watwae ubingwa.
Kocha wa City, Manuel Pellegrini alisema: Natarajia kushinda. Hatufikirii kupata pointi moja pekee bali tunataka kushinda kabisa. Tutaifunga West Ham na kutwaa ubingwa.
Lakini Kocha wa West Ham, Sam Allardyce Big Sam hana mpango wa kuiachia City kirahisi kutwaa ubingwa, huku akitaka kumpa raha nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard kutwaa taji lake la kwanza la Ligi Kuu katika maisha yake.