Yaliyopita: Tutafakari Polisi yetu

Yaliyopita: Tutafakari Polisi yetu

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,946
Reaction score
38,665
Amani iwe kwenu nyote.

Wiki ya pili sasa ninawaza na kuwazua kuhhsu jeshi letu tukuka la usalama wa raia na mali zao yaani jeshi la Polisi.

Ifike mahala kama kuna watu katika jamii ambao wanahitaji kuombewa msamaha na wenyewe kujirekebisha ni jeshi la polisi hususan watendaji wake wengi.

Kwa nafasi yangu niliyotumikia serikalini ninatambua kwamba siyo polisi wote wenye mwenendo na tabia ovu za kinyama kinyume na viapo vyao, GPO na haki za binadamu..

Lakini sehemu kubwa ya polisi wamesababisha vilio juu ya haki na uhuru wa raia. Na wanajua kuwa wametenda mengi yasiyosimulika dhidi ya raia ambao waliapa kuwalinda na mali zao.

Naomba leo tuangalie tulivyohadaiwa kisiasa kuhusu polisi. Kwanza uhuru wa maoni na haki ya kukusanyika vikatungiwa sheria ya kibaguzi ambapo CCM hawawajibiki kuomba uhuru ama haki ya kukusanyika bali Watanzania wenye fikra mbadala za kimaendeleo walinyimwa kabisa haki hizo na polisi walitekeleza kwa unyama mkubwa maagizo ya kuzima hatua ama mwenendp wowote wa wanasiasa wa upinzani kukutana na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.

Wapinzani walipaswa kuomba ridhaa ya mikutano kwa polisi ambao kimsingi hawapaswi kujihusisha na siasa na badala yake walipaswa kutoa ulinzi baada ya kutaarifiwa kama wanavyofanya kwa CCM.

Upinzani wamekuwa wananyimwa haki (siyo kibali) ya kufanya shughuli zao za kisiasa kwa kisingizio kwamba jeshi la polisi eneo husika hawana staff wa kutosha kutoa ulinzi kwa shughuli hiyo ya kisiasa.

Badala yake, wapinzani walipoona haki yao inatekelezeka bila ulinzi wa polisi, ndipp kunatokea kikosi kikali cha polisi ambacho lengo lake ni kuvunja mkutano huo bila kuzingatia utu na ubinadamu.
FB_IMG_1672939928459.jpg

Hii hadaa ya kisiasa imefanyika bila taifa kung'amua kuwa hao hao askari wanaotumika kutawanya na kuvunja mikutano ya wapinzani wqngeweza kutoa ulinzi mikutano ikafanyika kwa amani.

SWALI
Je polisi wanaposema hawana ulinzi wa kutosheleza hitaji la usalama wa mkutano ama maandamano ya raia na hapohapo inatuma kikosi cha kushambulia na kutawanya raia ina maana kuwa jeshi letu la polisi lina kikosi cha uvamizi na kivita?

Tukikumbuka wananchi waliopoteza maisha kwenye vita vilivyoanzishwa na polisi dhidi ya raia inaleta picha kuwa polisi yetu inazo zana za kutosha kulinda raia lakini badala yake zinatumika dhidi ya raia ambao kimsingi kodi zao ndizo zinunua zana hizo na kodi hizo ndo mishahara ya polisi

RAI
Wenye hekima na akili tunapaswa kuliombea msamaha jeshi letu la polisi msamaha kwa wananchi ili tufungue ukurasa mpya wa jamii na walinzi wao.

Kama Rais ameshaona umuhimu wa vyama kufanyq mikutano ya siasa maana yake kuna haja ya kuboresha utendaji wa jeshi letu.

Sisi raia tunapaswa kujivunia jeshi letu la pollisi na siyo kuendeleza kuogopana na kukwepana kama panya na paka.

NYONGEZA
Tanzania kwa sasa tunapitia kwenye giza nene zito tena kubwa. Ni vile Mungu anatupa uvumilivu na kustawisha upendo katikati ya mateso na ukatili mkubwa.

Tusiache kuiombea nchi yetu ustawi, mshikamano na dira bora za maendeleo zinazotekelezeka

View attachment 2490764

Tuwaombee walitumika vibaya. Mungu ni mwenye rehema
 
RAI
Wenye hekima na akili tunapaswa kuliombea msamaha jeshi letu la polisi msamaha kwa wananchi ili tufungue ukurasa mpya wa jamii na walinzi wao.

Kama Rais ameshaona umuhimu wa vyama kufanyq mikutano ya siasa maana yake kuna haja ya kuboresha utendaji wa jeshi letu.

Sisi raia tunapaswa kujivunia jeshi letu la pollisi na siyo kuendeleza kuogopana na kukwepana kama panya na paka.
Well
 
Back
Top Bottom