Yaliyonikuta... Sitosahau kamwe!!!

Yaliyonikuta... Sitosahau kamwe!!!

Josey j

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2017
Posts
473
Reaction score
925
Habarini wana Jf

Straight to the point: Leo ule msemo wa nilizani nimepata kumbe nipatikana umejidhihirisha kwangu...na sasa nmeamini usilo lijua ni kama usiku wa kiza..

Nikiwa nimetoka mishe mishe naangalia usafiri huku na kule... Inapita coastal bus ikiwa na konda akinionesha ishara kua twende, siku sita hapo gari ilikua imejaa lakini ilibak seat moja nyuma kabisaa...fasta nazama ndani ya gari mdogo mdogo napita kwenye korido kuelekea kwenye seat... Baada ya vituo kazaa kupita nagundua kimebaki kituo kimoja ili nishuke... Wakati naangalia na najiandaa kuanza kusogea mbele japo bado gari haija simama...ile kuangalia chini.. Moyo unalipuka paaaaa! Na mapigo yanaongezeka kasi yake baada ya kuona noti ya shilingi elfu kumi kwenye korido ya gari.. Napatwa na kiwewe kisicho jionesha mbele za watu.... Aki inanituma nisishuke hicho kituo ili nipate time ya kuitarget ile noti,
.. Na usawa huu ulivobana.. Najisemea hii fursa muhim.sana ko ntafanya niwezalo ili niokote bila kugundurika... Kwa sababu nikisema nitangaze itakua sio, kuna miwatu itaibuka kusema ni yenyew imedondosha..na itakua fujo... Mbali na hayo hata malaika watanicheka sana kwa pambio na vigeregere...

Basi gari inaposimama... Konda anasema Fanya fasta anko wanga wengi nyuma huko...najifanya kushangaa then nasema kwa saiti..konda Mimi sishuki hapa nmesema kituo cha mbele ...konda anakasirika sana.. Anamuamuru dereva wako kuachia manyoya( kuondoa gari) wakati huo noti nimeikanyaga na kiatu huku nawaza jinsi ya kuinama kuiokota... Basi naamua kuiburuza mdogo mdogo mpaka kwenye siti yangu then naangalia kushoto namuona mzee wa makamo yupo bize na gazeti ..kulia kwangu kuna broo ana sinzia sinzia kwa mawenge..inaonekana mchovu kweli....basi kwa tahadhari najifanya najikuna mguuni then naikota huku nikiwa nimekaza macho mbele ya safari..ile kuangalia vizuri macho yanathibitisha kua kweli ni noti ya ya elfu kumi...mawazo yananijia kua niwe makini Nayo inawezekana ni mtego au chuma ulete... Basi naamua kuitenganusha na hela zangu zilikua mfuko wa kushoto...yenyew naiweka kulia baada ya game kukamilika sasa naamua kushuka kituo kinachofuata......kumbuka kituo nilichomuahidi konda sikushuka ila kuna abiria wengine walishuka kwahyo hata konda hakuuliza....kwa kweli nilishukia kituo cha mbali sana.... ila sikuona shida kwa sababu nilijua nimepata faida

Basi nilishuka tu akili ikanambia tafuta sehem tulivu ushushie hata maji makubwa baridiiiiii, basi nikapendezewa na sehem flani...nikakaa muhudumu kaja nikaagiza changu.. Sasa ikabidi nitoe ile hela naanza kuitathmini..najiliza yaan vyuma vilivyokaza hivi watu wanadondosha pesaa!!!! NAMSIKITIKIA SANA ALIYE DONDOSHA... LAKINI ILE KUTOA ZILE ZA KWANGU ZA UPANDE WA PILI NAGUNDUA KUNA NOTI YA SHILINGI ELFU KUMI IMEPUNGUA,
SIAMINI MACHO YANGU NARUDIA KUHESABU.. MAJIBU NI YALE YALE KUA TEN HAIPO....DAAÀ KICHEF CHEF KINANIBANA GHAFLA NAANZA KUJIONA MKOSAJI SANAA.... SASA HELA IMEENDA WAPI? LAKINI KUNA SAUTI NDANI YANGU INANIJIBU....HIYO ULIYOOLOTA KWENYE GARI NDIO YA KWAKO ULIDONDOSHA ULIPOKUA UNATOA SIMU MFUKONI WAKATI UNAENDA KWENYE SITI... ..........

NDIPO KICHWA KINAZUNGUKWA NA MISEMO MBALIMBALI NA METHARI NYINGI KICHWANI MWANGU...NAKUMBUKA MSEMO WA KWANZA KU HIT KICHWANI MWANGU NI ULE USEMAO.. " NILIZANI NIMEPATA KUMBE NIMEPATIKANA"
NA

" USILO LIJUA NI KAMA USIKU WA KIZA"
 
Siku nyingine utangaze ili kuepuka usumbufu usio wa lazima kama huu
 
Hahahhahhahhahahhahahhahahahahhahahaahhaahah dah baba legeza kidogo
 
Back
Top Bottom