Yaliyonikuta RITA

Sijaeleza kuwa nimeombwa Rushwa Sasa TAKUKURU nafuata Nini !!,
Ndg.hivi shuleni ulifuata Nini...!!!
Nilipata ujanja na mbinu za kuishi kwenye inchi za afrika,
Popote afrika mambo yanaenda fasta tu kwa mbinu sasa wewe endelea kuminyana kazi ya siku moja utaifanya mwezi moja
 
Mimi niliwahi kupata connection ya mfanyakazi wa Rita nikamkatia eflu kumi na tano nikampa documents ndani ya wiki chap nikapata cheti cha kuzaliwa ,bongo ukisema kila kitu upite njia za kihalali utapata tabu sana.
naku-pm kiongozi na mie nina swala langu pale nimejikuta najisemea kimoyomoyo tu uhamiaji wapo wapi wanifukuze hapa nchini ama wanitafutie nchi ya kwenda kama wao hawataki kunitambua kama raia wao
 
naku-pm kiongozi na mie nina swala langu pale nimejikuta najisemea kimoyomoyo tu uhamiaji wapo wapi wanifukuze hapa nchini ama wanitafutie nchi ya kwenda kama wao hawataki kunitambua kama raia wao
Nipo mbali nae sasa ,halafu huyo mtu anashughulikia watu wa DSM tu.
 
Hiv mtu anaweza kubadili jina la mzazi katika cheti cha kuzaliwa?
Msaada
 
Tena bora hata nyie wanandugu walikuwa na NIDA.kuna watu mpaka leo hii wanahangaikia kadi ya NIDA kwa miongo kadhaa na hawajapata.mngekutana na kadhia hii naona ngetumia hata miaka kumi kukipata hicho cheti.nchi yangu tanzania tuendako ni kiza kinene.
 
RITA na NIDA ni taasisi za Ovyo sana.

Bila mlungula hapo mtazungushwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…