Ndugu yangu nilimkabili mama aliyetaka turudi tukarekebishe barua tuje na barua ya serikali ya mtaa iliyoandikwa tarehe ya kifo nikamuuliza hii document ya Hospitali huiamini ??Tumeshindwa kuingia barabarani kwa umoja wetu kutokana na uoga wetu,mi napendekeza kila mtu kwa nafasi yake alianzishe huko huko alipo kwa mfano hapo ofisini kwao ungeanzisha timbwili ikibidi usitoke ofisini hadi wakamilishe huduma yako.watanzania tumekuwa waoga sana na ndio maana watumishi na viongozi wanafanya watakavyo na rushwa imekuwa ni kitu cha kawaida
Aisee, huyo mama anafungu lake ndio maana alikuchana hivyoUnashangaa hii mkuu? No wonder basi umezungushwa hivyo.
Mimi niliombwa rushwa macho makavu kabisa kupewa mwili wa marehemu Kigamboni Kijibweni sijui vijibweni hospital. Yaani mtu una msiba mzito wa baba yako kisha gaidi inakuomba rushwa macho makavu kabisa na inakuzingua balaa. Nikajifanya nunda kupanda ngazi nikapelekwa kwa boss wake mwanamama mmoja nae hakupepesa macho kanichana tu we toa hela mambo yasiwe mengi
Wewe uvccm acha ujinga .
Sijaandika hapa Kama mtihani ili nisahihishwe wewe ndio Aina ya watu wa hovyo ktk Nchi hii.....
Mpyuuuuu
Ndugu yangu Mtanzania mwenzangu nilifuata taratibu zooote sijathubutu kumtafuta staff yyt nje ya utaratibu ili anisaidie ndiyo maana nilianzia kupiga simu kitengo cha huduma kwa wateja kupata utaratibu ,Mkuu umekua kama mgeni kwenye nchi yako,mbona mambo yapo wazi tu
kitendo cha wewe kufatilia hicho cheti tayari ulishajitengenezea ugumu wa haki yako
ni kweli ni haki yako kupata hicho cheti lakini hukupaswa ufatilie wewe, ulichotakiwa
ni kutoa tu pesa kwa wahusika (chagua mtu m1) ambae n mfanyakazi wa RITA
mpe pesa mwachie akufanyie kazi yako,ndani ya wiki 1 ushapata cheti tena kikiwa
hakijakosea hawa rangi,kitakua clean n clear, ila ukijifanya unafatilia wanakufanyia
makusudi maana washatonyana na "nina mashaka" wewe kuna mtu ulianza nae
akakutangazia dau ukamtema,ukaamua kufatlia mwenyewe,Huyo mtu ndio anafanya
firigisu zote hizo,ni wamesha ambiana cheti cha flani kifanyieni hivi vile nk "hadi akome"
Next time ya ngoswe muachie Ngoswe,Tupo Tanzania nchi yenye sifa ya rushwa hilo
huitaji kurudia rudia kuambiwa unatakiwa tu uwe ushalielewa na kutambua huu utaratbu
wa nchi yetu hasa unapotaka haki yako,Time is Money imagine umepoteza muda kiasi gani kufatilia hicho cheti'
Huo muda thamani yake n sawa na 50k au 100k? Muda ni gharama sana Mkuu next time jiandae kisha fata tu taratbu zao,yako yakuendee.
Niombeee nije kuwa Rais "labda" naweza ondoa rushwa kama sio ipunguza ila kwasasa Fata tu wanachotaka nenda nao sawa.
Watanzania waoga sana, taarifa yako imekaa kama umbea vile si utoe details za kutosha halafu usikilizie au unaogopa niniTaasisi ya RITA Ni nyeti mno na ilistahili kuwa na wafanyakazi mahili na waadilifu.
Miezi miwili nafuatilia cheti Cha kifo Cha mwanafamillia hadi leo sijakipata.
Kabla yakuanza mchakato wa kufuatilia cheti hicho nilipiga simu huduma kwa wateja kuulizia utaratibu wa kufuata ,
Waliniambia kunahitajika nyaraka ya Hospitali inayothibitisha kifo cha marehemu , kunahitajika barua ya mukhtasari wa kikao Cha ndugu Cha kumteua msimamizi wa mirathi,barua ya utambulisho toka serikali ya mtaa inayothibitisha kifo Cha marehemu, na msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa ndiye anayepaswa kufuatilia hiko cheti.
Baada ya kukamilisha nyaraka hizo tulikwenda RITA lakini baada ya nyaraka zetu kukaguliwa tukaambiwa kunahitajika kopi ya kitambulisho Cha NIDA Cha kila mwana ndugu aliyehudhuria kikao Cha ndg Cha kumteua msimamizi wa mirathi ,
Tukarudi NYUMBANI kukusanya kopi ya cheti Cha NIDA Cha hao ndg. Baadhi ya ndg.walikuwa wamesafiri baada yamuda tukapata kopi zote tukarejea RITA ,
Baada ya kufika nyaraka kukaguliwa tukaambiwa hao ndugu wanahitajika kuwepo kuthibitishwa !!!
Tukarudi NYUMBANI tukatafuta baadhi ya ndugu siku nyingine tukarudi RITA na ndugu ,
Baada ya nyaraka kukaguliwa Tena tukaambiwa eti barua ya serikali ya mtaa haijaandika tarehe ya kifo !
Tukumbuke nyaraka ya Hospitali. Na mukhtasari wa kikao Cha ndg. Tarehe ya kifo ipo lakini mtoa huduma akasema lazima barua ya serikali ya mtaa iandike tarehe ya kifo Cha marehemu ,
Tukarudi NYUMBANI barua ikarekebishwa siku hiyohiyo na hatimaye tukatakiwa kulipia gharama ya cheti na tukapewa tarehe ya kurudi kuchukua cheti Cha kifo .
Tarehe ilipofika tukaenda RITA cheti Kiko tayari lakini tarehe ya kifo imekosewa imeandikwa tarehe ya kuzaliwa ya marehemu na sababu ya kifo imekosewa imeandikwa kifo kisicho Cha kawaida badala ya kifo Cha kawaida kwakuwa marehemu alikufa kwa ugonjwa .
Tukapewa Tena tarehe ya kurudi RITA ili cheti kirekebishwe , baada ya kurudi Tena RITA kukaa foleni masaa mawili baada ya kufika kwahudumu anatuambie eti cheti hakijatoka kwa sababu hatujalipia gharama za marekebisho !!
Ni Jambo la ajabu Sana makosa yamefanywa na RITA lakini gharama alipe aliyekosewa !!
Mbaya zaidi hatukuambiwa kabla tulipie gharama Bali tuliambiwa tarehe ya kurudi kuchukua cheti kilichorekebishwa ,
Baada ya kutaka kujua uhalali wa malipo hayo tukaambiwa ndiyo utaratibu wao.
Tumelipia tunasubiria cheti!!
Ndugu zangu waTanzania tuna safari ndefu Sana kupata maendeleo kwakuwa vikwazo Ni vingi Sana ,
Naomba mamlaka za juu ziichunguze RITA vyeti vinavyokosewa Ni vingi Sana tujue wanakosea makusudi ili wapate mapato ??
Kitengo Cha uchapaji kichunguzwe kama wafanyakazi wake Wana weledi wa kufanya kazi hiyo.
Nina mashaka Tukirudi Tena kuchukua cheti Kama hatutakutana na kikwazo kingine..
TANZANIA NCHI YANGU....
Unataja details gani au wewe ndio mkurugenzi wa RITA hebu Soma comments za wenzako ndio utajua Ni wangapi wanapitia changamoto za kupata huduma RITA wewe endelea kuwa mtetezi wa ujinga kwa kuwa wajinga wa Nchi hii ndiyo mtaji wa watawala na ndio mtaji was Wana siasa hasa wa chama Cha....Watanzania waoga sana, taarifa yako imekaa kama umbea vile si utoe details za kutosha halafu usikilizie au unaogopa nini
Ndugu jiongeze tu.me mwenyewe tanesco hapa Moro wananisumbua mwez wa nne hawataki kunifungia umeme, najipanga niwakatie 50000 tumalizane nipate hudumaTaasisi ya RITA Ni nyeti mno na ilistahili kuwa na wafanyakazi mahili na waadilifu.
Miezi miwili nafuatilia cheti Cha kifo Cha mwanafamillia hadi leo sijakipata.
Kabla yakuanza mchakato wa kufuatilia cheti hicho nilipiga simu huduma kwa wateja kuulizia utaratibu wa kufuata ,
Waliniambia kunahitajika nyaraka ya Hospitali inayothibitisha kifo cha marehemu , kunahitajika barua ya mukhtasari wa kikao Cha ndugu Cha kumteua msimamizi wa mirathi,barua ya utambulisho toka serikali ya mtaa inayothibitisha kifo Cha marehemu, na msimamizi wa mirathi aliyeteuliwa ndiye anayepaswa kufuatilia hiko cheti.
Baada ya kukamilisha nyaraka hizo tulikwenda RITA lakini baada ya nyaraka zetu kukaguliwa tukaambiwa kunahitajika kopi ya kitambulisho Cha NIDA Cha kila mwana ndugu aliyehudhuria kikao Cha ndg Cha kumteua msimamizi wa mirathi ,
Tukarudi NYUMBANI kukusanya kopi ya cheti Cha NIDA Cha hao ndg. Baadhi ya ndg.walikuwa wamesafiri baada yamuda tukapata kopi zote tukarejea RITA ,
Baada ya kufika nyaraka kukaguliwa tukaambiwa hao ndugu wanahitajika kuwepo kuthibitishwa !!!
Tukarudi NYUMBANI tukatafuta baadhi ya ndugu siku nyingine tukarudi RITA na ndugu ,
Baada ya nyaraka kukaguliwa Tena tukaambiwa eti barua ya serikali ya mtaa haijaandika tarehe ya kifo !
Tukumbuke nyaraka ya Hospitali. Na mukhtasari wa kikao Cha ndg. Tarehe ya kifo ipo lakini mtoa huduma akasema lazima barua ya serikali ya mtaa iandike tarehe ya kifo Cha marehemu ,
Tukarudi NYUMBANI barua ikarekebishwa siku hiyohiyo na hatimaye tukatakiwa kulipia gharama ya cheti na tukapewa tarehe ya kurudi kuchukua cheti Cha kifo .
Tarehe ilipofika tukaenda RITA cheti Kiko tayari lakini tarehe ya kifo imekosewa imeandikwa tarehe ya kuzaliwa ya marehemu na sababu ya kifo imekosewa imeandikwa kifo kisicho Cha kawaida badala ya kifo Cha kawaida kwakuwa marehemu alikufa kwa ugonjwa .
Tukapewa Tena tarehe ya kurudi RITA ili cheti kirekebishwe , baada ya kurudi Tena RITA kukaa foleni masaa mawili baada ya kufika kwahudumu anatuambie eti cheti hakijatoka kwa sababu hatujalipia gharama za marekebisho !!
Ni Jambo la ajabu Sana makosa yamefanywa na RITA lakini gharama alipe aliyekosewa !!
Mbaya zaidi hatukuambiwa kabla tulipie gharama Bali tuliambiwa tarehe ya kurudi kuchukua cheti kilichorekebishwa ,
Baada ya kutaka kujua uhalali wa malipo hayo tukaambiwa ndiyo utaratibu wao.
Tumelipia tunasubiria cheti!!
Ndugu zangu waTanzania tuna safari ndefu Sana kupata maendeleo kwakuwa vikwazo Ni vingi Sana ,
Naomba mamlaka za juu ziichunguze RITA vyeti vinavyokosewa Ni vingi Sana tujue wanakosea makusudi ili wapate mapato ??
Kitengo Cha uchapaji kichunguzwe kama wafanyakazi wake Wana weledi wa kufanya kazi hiyo.
Nina mashaka Tukirudi Tena kuchukua cheti Kama hatutakutana na kikwazo kingine..
TANZANIA NCHI YANGU....ndu
Mimi niliwahi kupata connection ya mfanyakazi wa Rita nikamkatia eflu kumi na tano nikampa documents ndani ya wiki chap nikapata cheti cha kuzaliwa ,bongo ukisema kila kitu upite njia za kihalali utapata tabu sana.Ndugu yangu Mtanzania mwenzangu nilifuata taratibu zooote sijathubutu kumtafuta staff yyt nje ya utaratibu ili anisaidie ndiyo maana nilianzia kupiga simu kitengo cha huduma kwa wateja kupata utaratibu ,
Mimi Ni muumini wakufuata utaratibu ndiyo utamaduni wangu napitiaga changamoto Sana kwa sababu ya utamaduni wangu huu lakini ndiyo njia ya maisha niliyoamua kuifuata.....
Kwa hiyo huu ndio ushauri wako,..Mimi niliwahi kupata connection ya mfanyakazi wa Rita nikamkatia eflu kumi na tano nikampa documents ndani ya wiki chap nikapata cheti cha kuzaliwa ,bongo ukisema kila kitu upite njia za kihalali utapata tabu sana.
Rita ni majanga matupu. Angalia wanafunzi wanavyopitia uvuli wa mauti kuhakiki Cheti Cha kuzaliwa.
Mama Samia tupia jicho Rita
Mkuu siku nyingine usije humu kwa issue kama hizi nenda direct pale upanga kuna ofisi ya takukuru,Asante kwa ushauri mTanzania Mzalendo wa mt.wa Lumumba.
Sijaeleza kuwa nimeombwa Rushwa Sasa TAKUKURU nafuata Nini !!,Mkuu siku nyingine usije humu kwa issue kama hizi nenda direct pale upanga kuna ofisi ya takukuru,
Nadhani itakuwa nafuu zaidi
Kutekeleza imani yako ya haki in Africa