Yaliyonikuta RITA

Rita DSM makao makuu.
 
Rushwa cheti Cha kifo !!!?[emoji22][emoji22]
Unashangaa hii mkuu? No wonder basi umezungushwa hivyo.

Mimi niliombwa rushwa macho makavu kabisa kupewa mwili wa marehemu Kigamboni Kijibweni sijui vijibweni hospital. Yaani mtu una msiba mzito wa baba yako kisha gaidi inakuomba rushwa macho makavu kabisa na inakuzingua balaa. Nikajifanya nunda kupanda ngazi nikapelekwa kwa boss wake mwanamama mmoja nae hakupepesa macho kanichana tu we toa hela mambo yasiwe mengi
 
Sasa cheti cha kifo kufatilia Rita kwanza sio sahihi hospital ndiyo ingekuwa inatoa hivyo vyeti sasa uthibitisho wa serikali ya mtaa wa kigo cha mtu aliyefia hospitalini kweli? Ngoja niwache kwanza
 
Hivi hosp hawawezi kuwa wanatoa hivyo vyeti?

Rita wao wangewa wana maintain data base tu.

Baada ya kuthibitisha kifo, cheti kinaandaliwa kabisa papo kwa papo. Maana ni details chache sana za kujaza.

Ikiwezekana wafanye intergration na mfumo wa nida. Baadhi ya taarifa wanazivuta tu.
 
Hii ni syndicate ya rushwa mpaka juu, ndiyo maana hawataki kuweka namba za simu za HQ ili watu wapeleke malalamiko hatua zichukuliwe dhidi ya watumishi wazembe na warasimu
 
Vingeweza kutengenezewa mfumo vikawa generated automatically toka hospital kama viongozi wakitaka kuondoa urasimu
 
CCM chamaaa ooooh Chamaa CCM chamaaa kinajenga nchiiii🎼🎼🎼🎼

Mama Samiaaa Chamaaaa oooh Chamaaa na Samia wetu Chamaa kinajenga nchiiii.... 🎼🎼🎼🎼🎼

Hili nalo nendeni mkalitizame.
 
Pole mno mtoa mada, hivi ni vielelezi kuwa tumo in a shithole country, hizi death certificates zinatakiwa zitolewe na home affairs sio vinginevyo, home affairs ndio kikatiba wanaotunza daftari la raia, huu ni urasimu mwingine wa kuwa na Rita (futilia mbali uchafu huu),na vyeti hivi kifo kikishathibitishwa (doctors death report)cheti kinatolewa within hours, inakatisha tamaa kuishi hapa nchini maana kila kitu ni shida
 
Pole Sana mkuu. Walihitaji 'takrima" ya sabuni
 
Kama ni hivyo basi ina maana wanakosea makusudi ili wakusanye tozo ya marekebisho.
 
Tumeshindwa kuingia barabarani kwa umoja wetu kutokana na uoga wetu,mi napendekeza kila mtu kwa nafasi yake alianzishe huko huko alipo kwa mfano hapo ofisini kwao ungeanzisha timbwili ikibidi usitoke ofisini hadi wakamilishe huduma yako.watanzania tumekuwa waoga sana na ndio maana watumishi na viongozi wanafanya watakavyo na rushwa imekuwa ni kitu cha kawaida
 
Jifunze kuweka aya kwenye uandishi wako
 
Pole sana mkuu, nimeisoma hii habari kwa hisia sana.

Sijui kwa nini tukiwa kwenye nafasi fulani huwa tunajiona special sana na kutoa majibu ya dharau, majivuno
 
Hivi huyo mtumishi alishindwaje kuwaambia vitu vyote muhimu vinavyohitajika? Mtumishi wa hovyo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…