Yaliyojiri ziara ya Rais Paul Kagame nchini Tanzania na Mwenyeji wake Rais Magufuli

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698



Habari wakuu,
Leo Rais wa Rwanda, Paul Kagame ametua nchini katika uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere na kupokelewa na mwenyeji wake, Rais wa Tanzania, Dr John Pombe Joseph Magufuli na sasa wameelekea Ikulu.

Tuwe sote pamoja kujuzana yanayojiri
======

Rais Magufuli na Paul Kagame tayari wameketi Ikulu tayari kwa shughuli kuanza, kwa sasa mawaziri wanachukua nafasi zao. Anaeongea kwa sasa ni Gerson Msigwa.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Rwanda na Tanzania wamepeana mikono wakikabidhiana taarifa ya tume ya pamoja ya Rwanda na Tanzania ya ushirikiano.

Anaeongea kwa sasa ni Rais wa Rwanda, Paul Kagame.

Rais Magufuli amesema Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA itafunga ofisi katika nchi ya Rwanda. Ili kuongeza ufanisi na kurahisisha biashara.

=======

Kwa sasa Rais Magufuli na Paul Kagame wamehamia Sabasaba kwa ajili ya uzinduzi wa maonyesho ya kimataifa ya biashara(Sabasaba). Rais Paul Kagame ndie mgeni rasmi na ndiye anayeyafungua rasmi maonyesho haya.

Habari kwa Ufupi....

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk Joseph Pombe Magufuli amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) watafungua ofisi nchini Rwanda ili kuraisisha uhakiki wa bidhaa kwa wafanyabiashara wa Rwanda wanaoingia nchini.

Aidha amesema kuwa Serikali imetoa eneo la bandari kavu (ICD) kwa ajili ya kuhifadhia Bidhaa kutoka nchi ya Rwanda ili kupunguza urasimu ambao umekuwa kikwazo kwa maendeleo ya biashara hapa nchini na kwa namna hiyo biashara itakua kwani tunategemea uchumi utapanda kutoka asilimia 7 ya sasa mpaka asilimia 7.2.

Pia amesema kuwa Serikali imepunguza vituo vya ukaguzi barabarani kutoka Tanzania kwenda Rwanda kufikia vitatu na kwa kufanya hivyo itarahisisha safari za magari ya biashara njiani na hivyo kufikisha bidhaa kwa haraka.

Aidha amesema kuwa serikali iko mbioni kuanzisha kituo kimoja cha kukusanya mapato badala ya kila sehemu kuwa na mfumo wake ambao unapoteza mapato mengi kwa kuwa mifumo hiyo haina uthibiti mmoja na hivyo serikali ya Rwanda itasaidia kwa kuleta wataalamu wa Tehama ambao watasaidia kutoa mafunzo ili kusaidia mapato yetu kuwa katika udhibiti mmoja.

Kwa upande Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuendeleza Uchumi wa nchi izi mbili kwani zina historia ndefu na kwa kuendelea kufanya biashara pamoja nchi izi mbili zimejenga taswira mpya katika mahusiano.

Awali Mawaziri wa mambo ya Nje wa nchi za Tanzania na Rwanda walitia saini Muhtasari wa Tume ya Ushirikiano wa pamoja baina ya nchi izi mbili.

Ujenzi wa reli ya kisasa (Standard gauge) kutokea Dar es Salaam hadi Kigali. Rais Magufuli kama alivyowahi kusema awali, leo amesema kuwa reli hiyo itakuwa ni ya kisasa na itasaidia usafirishaji wa mizigo na usafiri kutoka Tanzania hadi Rwanda. Aidha, Mawaziri husika wa miundombinu kutoka pande zote mbili watakutana hivi karibuni ili kuweka mjengo kazi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi huo mara moja.

Bandari ya Dar es Salaam. Rais Magufuli ameeleza kuwa takribani asilimia 70 ya bidhaa zza Rwanda hupita katika bandari ya Dar es Slaam. Aidha ameeleza kuwa kulikuwapo na vikwazo mbalimbali katika ufanisi wa bandari hiyo ambavyo kwa sasa hivimo. Katika hatua nyingine Rais Magufuli amesema kuwa serikali itatenga sehemu ya kuhifadhi mizigo yote ya Rwanda mara inapotolewa bandarini ili kupunguza mloloongo uliopo.

Pia Rais Magufuli amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) itajenga kituo kimoja nchini Rwanda ili kuwasaidia wafanyabaishara wa Rwanda kupunguza mlolongo wa kuja kufanya malipo Tanzania na badala yake wanaweza kufanya wakiwa Kigali.

Usafirishaji wa mizigizo kwa njia ya barabara. Rais Magufuli kama alivyoeleza awali alipokuwa nchini Rwanda, leo amesema tena kuwa, sasa vituo vya kupimia mizigo kwa magari vitakuwa vitatu tu toka Dar es Salaam hadi Rwanda. Hii itasaidia kupunguza usumbufu uliokuwapo mwanzoni kwa magari hayo ya mizigo.

Ununuzi wa ndege mbili kubwa. Katika sekta ya usafirishaji, Rais Magufuli alisema kuwa alipewa ushauri na Rais Kagame juu ya namna ya kupata ndege na sasa serikali kwa kushirikiana na watalaam kutoka Rwanda Air wapo katika mchakato wa kununua ndege hizo na alisema kama mipango yote itakwenda sawa basi mwishoni mwa mwezi Septemba ndege hizo zitawasili nchini.

Suala la Dimplomasia kati ya Tanzania na Rwanda. Akizungumzia hili, Rais Kagame alisema kuwa, lengo kubwa la ujio wake ni kuhakikisha anakuza umoja baina ya nchi hizi mbili ili kuweza kuleta maendeleo katika nchi zote. Kwa upande wa Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania na Rwanda zina uhusiano wa kihistoria na kueleza kuwa wanaamini pamoja wanaweza kusonga mbele.

Ujenzi wa kituo kimoja cha kukusanyia mapato nchini. Rais Kagame alimueleza Rais Magufuli kuwa licha ya uwapo wa makampuni mbalimbali yanayokusanya kodi Rwanda, lakini kuna kituo kimoja cha serikali ambacho hufuatilia kwa karibu makusanyo hayo na kuisaidia serikali kuhakikisha hakuna mtu anayeiibia serikali. Hivyo Rais Magufuli alisema kuwa atapokea msaada wa wataalamu kutoka Rwanda ili kushauri namna ya ujengjia wa kituo hicho kitakachofuatilia namna kila kampuni inavyokusanya mapato ili kuongeza mapato ya serikali.

Rais Magufuli alisema sasa kuna makampuni mengi ambapo kila moja lina namna yake ya kukusanya mapato kitu ambacho kinapelekea serikali kupoteza fedha ku kukosa filisofia moja inayoeleweka kati zoezi la ukusanyaji mapato.
 
Rwanda imetulia.Ninachofurahi,Haijazalisha wakimbizi kwa miaka sasa.Ilikuwa ni umiza kichwa. Unakaa kidogo unaona maelfu ya wakimbizi wanaingia Tanzania. Lakini sasa shwari. Kuna kazi kubwa kaifanya ya kuhakikisha nchi inakuwa na amani ili watu wafanye shughuli zao za maendeleo.
 
Back
Top Bottom