Prince Hope
JF-Expert Member
- Jul 21, 2012
- 2,155
- 444
Leo Alhamis March 03, 2016 marais wa Afrika mashariki au wawakilishi wao wamehudhuria uwekaji wa jiwe la msingi barabara ya njia nne kutoka Arusha, Holili/ Taveta-Voi (Km 234.3).
Kenyatta: Jukumu letu kama serikali ni kurahisisha/ kuwezesha wananchi wetu kufanya biashara sio kuwazuia, hio ndio kazi yetu na njia ya kuwezesha wananchi kuweza kufanya biashara zao bila masharti, bila kusumbuliwa ni kufanya kazi ambayo sisi twatakikana kufanya. Tujenge mabarabara, watu wawe na umeme wa kutosha ndio vijana wetu waweze kupata kazi.
Mambo haya hayatawezekana kama tutaendelea kuendelea kuishi katika masoko ambayo mzungu alituachia wakati aliondoka Afika hii yetu, hii mipaka ambayo twasema ni mipaka ya nchi, hii ni mipaka ambayo tulichorewa kule Ujerumani na mtu ambae hata hakua amekanyaga hapa, alikua anachora line, akasema huku ni kwangu na huko ni kwako.
Pamoja na Kenyatta pia Rais wa Uganda, Yoweri Museveni aizungumza na mwisho alihutubia Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania, John Magufuli.