Freelancer Wakala
JF-Expert Member
- Feb 6, 2016
- 1,193
- 828
Habari wanaJF,Leo nimefuatilia kwa yale yalotokea uku wilayani tunduru mkoa ruvuma kuhusiana na masuala ya meno ya tembo ipo kama ifuatavyo pia pata tamko la Mkuu wa wilaya tunduru alovosema.Nami Niko jirani na kijiji hicho cha Wenje kilichotokea tukio kutokana na harakati za hapa na pale sikuweza kuchukua picha za msafara huo,wa mkuu wa wilaya ambapo yeye alikuja na magari saba ya polisi kwenda kijijini hapo.
Licha ya kuwakamata watu watatu ambao walihusika na mauaji ya tembo kwa sababu tu ya kujihami na kuchukua maamuzi ya kuchukua meno ya tembo bado serikali imewakamatia hao watu watatu na wawili bado hawajapatikana.
Tembo hao kwakweli wamefanya madhara makubwa sana uku vijijini,mosi wananchi wanahofu ya kwenda mashambani kwasababu ya tembo wanaozurura umo maporini,pili tembo wamesababisha uharibifu wa mazao mashambani kama mahindi kukanyang'wa pamoja na mipunga na midizi.
Hili lote halijangaliwa limehangaliwa la wananchi kupiga tembo na kuchukuliwa kwenda sober house.
Na tamko la mkuu wa wilaya ni kama ifuatavyo.
Amesema mwananchi yeyote asikutwe na nyama pori au akivua samaki,maana hichi kijiji kimepakana na Mto ruvuma kutoka hicho kijiji cha wenje kwenda MTO ruvuma si mbali sana.Akikutwa na kitu chochote kinachohusiana na kutoka porini basi atajwe jina lipelekwe kwa mkuu wilaya tayari kwa kukamatwa,
Na amesema hao wananchi watatu walokamatwa sidhani kama watarudi tena pamoja na miongoni mwa watu kadhaa ambao walikamatwa kipindi cha nyuma na masuala ya tembo maeneo ya mpkani mwa msumbiji.
Hayo ni machache niyoyadaka toka maeneo na kijiji cha jirani cha wenje eneo la tukio ahsanteni.