Yaliyojiri Mwanza: Madhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari 2016, Nape asema Bunge live linajadilika

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,661
119,284
Wanabodi,
Leo ni siku ya Madhimisho wa Uhuru wa Habari, maadhimisho ya Mwaka Huu yanafanyika kitaifa mjini Mwanza, Jamii Forum's Maxence Melo, Waziri Nape Mnauye, Mzee Reginald Mengi, Baraza la Habari Tanzania, MCT, Tanzania Media Foundation, TMF, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, MISA TAN, Shirika la Umoja wa Mataifa UN ... na wengine wengi wako ndani ya nyumba.

Maadhimisho yameishaanza asubuhi hii, andamana nami nikikuletea kile kinachojiri, ila kama kuna mwana JF mwingine, tusaidiane ku update.

Karibu.

Paskali.
=====

Anyazungumza sasa ni Pili Mtambalike anawakilisha Baraza la Habari Tanzania, Media Council of Tanzania, MCT, ameikumbushia kauli mbia ya maadhimisho haya kwa mwaka huu, "Kupata habari ni haki yako, idai!"
===

Sasa hivi anazungumza Edda Sanga, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, TAMWA.
===

Sasa anazungumza Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari, MOAT, Dr. Reginald Mengi.

Mengi amekemea rushwa kwenye vyombo vya habari, amesema zile bahasha ni rushwa, hivyo wapokea bahasha ni majipu!, watumbuliwe!.

Duu!.
===

Leo Tumemkumbuka Mwangosi!. Tumesimama dakika moja for him.
======

Waziri Nape

Nape.jpg

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiongea kwenye siku ya Madhimisho wa Uhuru wa Habari Mwanza

Wanahabari fichueni maovu bila woga na mtukosoe ili tuijenge Tanzania yetu kwa pamoja!

Sote ni watanzania, tunaweza kukaa na kuamua kwa pamoja kuhusu hili la Bunge Live

Tunaweza kukaa mezani kuamua upya kuona namna bora ya kuboresha suala urushaji wa matangazo ya Bunge

Uamuzi wa kuanzisha studio ya Bunge ni uamuzi uliopitishwa na Bunge lililopita kabla hata sijawa mbunge
5223f928-9783-4dc4-8a46-fe91097b2ecf.jpg

Kutoka kushoto Maxence Melo Wa JamiiForums, Mungy wa TCRA, Sarah wa TZNIC na Joan Itanisa wa BBC Media Action

Tutatunga Sheria kwa kuzingatia Sera iliyopo. Muswada ukipita, utafuta sheria kandamizi kama ile ya 1976

Maoni ya wadau juu ya maboresho ya Muswada wa Vyombo vya Habari yatafanyiwa kazi. Tunatunga sheria kwa ajili ya watu

Kuna sheria zinalalamikiwa kuwa na mapungufu... Serikali itakaa chini kuangalia namna ya kuzirekebisha!

Nawahakikishia, Tutalinda, kuutetea na kuukuza Uhuru wa Vyombo vya Habari Tanzania
 
Wanabodi,
Leo ni siku ya Madhimisho wa Uhuru wa Habari, maadhimisho ya Mwaka Huu yanafanyika kitaifa mjini Mwanza, Jamii Forum's Maxence Melo, Waziri Nape Mnauye, Mzee Reginald Mengi, Baraza la Habari Tanzania, MCT, Tanzania Media Foundation, TMF, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, TCRA, MISA TAN, Shirika la Umoja wa Mataifa UN ... na wengine wengi wako ndani ya nyumba.

Maadhimisho yameishaanza asubuhi hii, andamana nami nikikuletea kile kinachojiri, ila kama kuna mwana jf mwingine, tusaidiane ku update.

Karibu.

Paskali.
Nayasubiri mashairi ya waziri mwenye dhamana atakavyotetea hoja yake kuhusu kufunga mapazia wakati wa kazi mjengoni. kama ataongea.
 
Wenye Access na Star TV, tufuatilieni iko live, naomba mwenye nafasi atupatie updates,

Huyu anayeongea ni Theofil Makunga, ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri.

Paskali
 
Anyazungumza sasa ni Pili Mtambalike anawakilisha Baraza la Habari Tanzania, Media Council of Tanzania, MCT, ameikumbushia kauli mbia ya maadhimisho haya kwa mwaka huu, "Kupata habari ni haki yako, idai!"

Paskali
 
sawa ngoja
Tuko Malaika Beach Resort, kumbe huku Mwanza pia kuna jf, afadhali!, ukifika nitafute, tena Mwanza siku hizi kuna baridi!, nimepigwa baridi mpaka basi!, yaani tuko hapa Mwanza tunateseka, kumbe kuna wanajf wenzetu!.

Paskali
nipande daladala za Buhongwa - Ilemela nakuja sasa hivi
 
Mkuu Pasco Mayalla,star tv naona kuna bongo beats au ni star nyingine inayoonesha live hayo maadhimisho?

Anyazungumza sasa ni Pili Mtambalike anawakilisha Baraza la Habari Tanzania, Media Council of Tanzania, MCT, ameikumbushia kauli mbia ya maadhimisho haya kwa mwaka huu, "Kupata habari ni haki yako, idai!"

Paskali
 
Vipi ule mswada wa sheria ya magazeti waziri mwenye dhamana kalizungumzia hilo ndio muda muafaka sasa uende bungeni na kufanyiwa kazi.

Na vipi kuhusu sheria iliyopitishwa na bunge Cyber Crime Act,mmeongelea hilo maana inanyima watu uhuru wa kutoa maoni yao.

Najua hili la juzi kuzuia bunge kuonyeshwa moja kwa moja mtakuwa mmelichambua kwa kina tunatusubiri tamko lenu .
 
Mwandiko wako unafanana sana na wa Pasco.
Mkuu Maiko Mtitu, wewe sio mtaalamu bali ni mtaalamuna, yaani unaweza hata kufananisha miandiko ya key board!, wewe sii mchezo!.

Pasco wa jf ni Pasco wa jf, ni mimi ni Pascal Mayalla, sisi ni watu wawili tofauti ila ni kweli tunafanana sana, na sio wewe peke yako unaotuchanganya, wengi wanatuchanganya, tofauti pekee kati yangu mimi Pascal Mayalla na Pasco wa JF ni content ya michango yetu!.

Mimi Pascal Mayalla, ni mtu wa ukweli, verified member, naleta humu matukio ya kweli kabisa yanayofanyika, hivyo mimi ni mtu mkweli na ninaongea kweli tupu!. Yule Pasco wa jf, sio mtu wa ukweli, ni pen name, yeye analeta vitu vya kufikirika, hivyo sometimes, uwongo mwingi!. Mimi ni CCM damu na ninampenda sana Magufuli, yule Pasco wa JF ni mtu wa Lowassa, hivyo hampendi, hampendi, hampendi Magufuli hata kumsikia!.

Kinachofanya watu wanatuchanganya, mimi Pascal Mayalla, kifupi cha jina langu pia ni Pasco, hivyo rukhsa kutuchanganya!.

Paskali.
 
Sasa hivi anazungumza Edda Sanga, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, TAMWA.

Paskali
 
Vipi ule mswada wa sheria ya magazeti waziri mwenye dhamana kalizungumzia hilo ndio muda muafaka sasa uende bungeni na kufanyiwa kazi.

Na vipi kuhusu sheria iliyopitishwa na bunge Cyber Crime Act,mmeongelea hilo maana inanyima watu uhuru wa kutoa maoni yao.

Najua hili la juzi kuzuia bunge kuonyeshwa moja kwa moja mtakuwa mmelichambua kwa kina tunatusubiri tamko lenu .
Hili litazungumziwa!.

Paskali
 
Back
Top Bottom