Yaliyojiri mkutano tanroads Iringa

Yaliyojiri mkutano tanroads Iringa

Egnecious

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
899
Reaction score
999
*YALIYOJIRI MKUTANO TANROADS IRINGA*

Tarehe 13/11/2018


“Kuhusu korosho sisi mkoa wa Iringa tunamuunga mkono Mhe. Rais kwa msimamo wake imara wa kuwatetea wakulima wa nchi yetu.”
*RC Hapi*

“Soko letu la ndani linatosha kabisa kununua korosho zote zitakazobanguliwa.Mhe. Rais asiwe na shaka kabisa juu ya wanunuzi.”
*RC Hapi*

“Mimi binafsi kutoka kwenye mshahara wangu nitanunua kilo 150 za korosho zilizobanguliwa kwa ajili ya ofisi yangu na familia yangu kumuunga mkono Mhe. Rais na wakulima nchini.”
*RC Hapi*

“Tunamshukuru Mhe. Rais kwa ujenzi wa barabara mkoani kwetu Iringa pamoja na uwanja wetu wa ndege”
*RC Iringa*

“Mkoa wa Iringa ni Mkoa wa 4 kwa GDP nchini kwa takwimu za NBS mwaka 2018.”
*RC Hapi*

“Mkoa wetu tumeamua kubeba agenda ya kukuza utalii na uwekezaji kupitia usafiri wa ndege za Air Tanzania.”
*RC Hapi*

“Tunashukuru kuwa mwakani mwezi march ndege za bombardier zitaanza kutua Iringa. Hii itakuza uchumi na uwekezaji.”
*RC Hapi*

“Tunaiomba wizara yako Mhe Waziri itusaidie ujenzi wa barabara ya Iringa- Ruaha (KM 104) kwa kiwango cha lami ili watalii wakishuka airport wasafiri kwa barabara hadi RUAHA kusaidia agenda ya utalii mkoani kwetu.”
*RC Hapi*

“Barabara ya Mafinga-Mgololo ni muhimu sana kwa uchumi wa mbao katika Mkoa wetu.Tuna kiwanda kikubwa cha karatasi Mgololo.Tunaomba ijengwe kwa kiwango cha lami.”
*RC Hapi*

“Mhe RC Hapi, wizara tunakamilisha mipango na Benki ya Dunia ambayo itatoa fedha kujenga barabara ya IRINGA- Mbuga ya RUAHA (KM 104 kwa lami).”
*Eng. Kamwelwe (Waziri Ujenzi)*

“Tutajenga viwanja vipya vikubwa vitatu vya ndege nchini ikiwemo upanuzi mkubwa na ujenzi mkubwa wa kiwanja cha ndege hapa mkoani Iringa.”

*Eng Kamwelwe (Waziri Ujenzi)*
 
Duh! Leo naona dogo kaja kwa adabu sana. Inaonekana sasa akili imeshamkaa sawa sawa. Kile kilikuwa ni kiwewe cha kuokota dodo chini ya mnazi it seems...
 
Back
Top Bottom