OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 51,972
- 114,278
Wakuu yamebaki masaa kadhaa tu wakali wa Dar na Afrika Mashariki waingie katika mtanange wa kukata na shoka mishale ya saa kumi jioni. Kimuhemuhe cha kufa mtu mitaa ya Msimbazi na Jangwani huku tiketi zikigombewa kama pipi za bure.
Mkuu wenu nitawaletea moja kwa moja mtanange huu kutoka uwanja wa Taifa na baadae nitawatupia video ya matukio yote muhimu ya mechi ya leo ikiwemo magoli na kadi kama vitakuwepo. Kwa uchambuzi kabla ya mechi gonga HAPA
Usicheze Mbali na JF
============
00' Refa anapiga kipenga kuashiria mwanzo wa mchezo
01' Yanga wanapata nafasi ya kupiga mpira wa adhabu ndogo kuelekea Simba ambao hata hivyo ulitua mikononi mwa mlinda mlango.
08' Simba wanapata kona ya kwanza ya mchezo hata hivyo haikuzaa matunda
14' Simba wanapata kona ya pili baada ya beki wa Yanga kurudisha mpira kwa golikipa, hata hivyo haikuzaa matunda
17' Kona ya tatu kwa Simba na inatokea piga nikupige lakini haikuzaa goli
18' Kona ya nne kwa Simba, golikipa wa Yanga anazongwa na kuwa adhabu ndogo kwenda Simba
22' Kadi ya kwanza ya njano kwa Banda na unapigwa mpira kuelekea Simba
23' Simba wanacheza gonga nyingi kuelekea Yanga hata hivyo hesabu zao zinatibuliwa na beki wa Yanga
24' Adhabu ndogo nyingine kuelekea Simba
25' Kadi nyekundu kwa Banda baada ya kadi mbili za njano
33' Ngoma anashindwa kupiga kichwa baada ya krosi kutoka kwa Kaseke ambayo ilimzidi kimo.
35' Simba wanahesabu kona nyingine lakini wanashindwa kufunga
39' Goaaaaaaaal, Yanga wanaweka mpira wavuni kupitia kwa Ngoma baada ya beki wa Simba(Ramadhan Kessy) kurudisha mpira 'mfupi' kwa mlinda mlango.
44' Simba wanapata kona mbili nyingine ambazo pia hazikuzaa matunda
45' Faulo kuelekea Yanga ambayo nayo haikuzaa matunda
45+2' Filimbi ya mapumziko inalia, Yanga 1-0 Simba
===
45' Mpira umerejea kumalizia ngw'e ya mwisho ya mchezo
48' Yanga wanaingiza mpira kati mapema kupitia winga lakini wanashindwa kutengeneza goli.
65' Ngonyani wa Yanga yuko chini na anapelekwa nje kwa machela
72' Goaaaaaaal, Yanga wanaandika goli la pili kupitia kwa Hamis Tambwe. Yanga 2-0 Simba.
76' Yanga wanashambulia tena lakini mpira unapaa juuuu
84' Simba wanapiga mpira wa adhabu ndogo karibu na goli la Yanga, hata hivyo wanashindwa kufunga.
85' Kadi ya njano kwa mlinda mlango wa Yanga kutokana na kuchelewesha muda.
90+3' Refarii Rukyaa anapuliza kipenga kuashiria mwisho wa mchezo,
MATOKEO: Yanga 2-0 Simba.
Yanga anapanda kileleni baada ya kukusanya pointi 46 kwa mechi 19 alizocheza, Simba anaenda nafasi ya pili kwa kubakia na pointi zake 45 baada ya mechi 20.
=======
Kutoka Mbeya
Mbeya city 0-3 Azam FC