Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Yanayojiri muda huu zinaendelea sherehe za kuapishwa Rais mteule wa Zanzibar
Waziri mkuu wa JMT amewasili na viongozi mbalimbali akiwemo Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi, Rais mstaafu Aman Abeid Karume, na Makamu wa rais mstaafu Gharib Bilal
Wakati huu unafanyika utambulisho wa viongozi mbalimbali wa vikosi vya KMKM
Tayari naye Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Davis Mwamunyange amekwisha wasili Uwanjani Amani Zanzibar, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, ameshawasili katika sherehe za kuapishwa Rais Mteule Dk.Shein Uwanja wa Amani Zanzibar.
Kwa muda huu kikundi cha uimbaji kinakaribishwa kutumbuiza kibao cha "Kama yalivyonipata"
Hatimaye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Joseph Magufuli ndiye anayetarajiwa kuwasili hapa viwanjani. Rais Magufuli anaingia na kushangiliwa na umati wa wananchi anashuka kwenye gari na anaenda kupokea salute na kuimba wimbo wa taifa.
Wimbo wa taifa unamalizika na Rais JPM anarudi jukwaa kuu na kusalimiana na viongozi mbalimbali.
Jaji mkuu wa Zanziba na spika wa baraza la wawakilishi pamoja na viongozi wa dini wanajiandaa kwa maandamano kuelekea jukwaa la kiapo.
Hivi sasa msafara wa Rais mteule Dr Ally Mohamed Shein ukiongozwa na askari wa pikipiki ndio unawasili uwanjani wa Amani hapa Zanzibar. Anashuka kwenye gari na kuelekea kwenye jukwaa dogo kwaajili ya kuimba wimbo wa taifa.
Rais Dr Ally Mohamed Shein anakagua gwaride lililoandaliwa, tendo la Omega linafanyika kuashiria kuisha kwa kipindi cha miaka 5 cha utawala wa Dr Ally Mohamed Shein kabla hajaapa rasmi.
Rais mteule anaelekea kwenye jukwaa la kiapo kwaajili ya kuapa, Rais anaapa raismi mbele ya jaji mkuu wa Zanzibar na kutia saini kiapo.
Tukio linalofuata baada ya kiapo na kukabidhiwa katiba ni dua kutoka kwa viongozi wa dini.
Dua ya kumuombea Rais.Shein inasisitiza kuwa Mwenyezi Mungu ampe nguvu wakati wa uongozi wake na Subira akiwatumikia wananchi wake. Dua Kwa Rais Shein inasisitiza awe na Hekima, Busara Uaminifu kwa wananchi wa Zanzibar na awaunganishe wananchi wote bila itikadi.
Zoezi la kumuapisha rais limekamilika na maandamano yanaelekea jukwaa kuu. Rais anakagua gwaride baada ya kuapishwa rasmi.
Wimbo wa taifa wa Zanzibar unaimbwa, na sasa vikosi vya gwaride vinatoka uwanjani kupisha shughuli nyingine.
Rais Dr Ally Mohamed Shein anakarinbishwa kulihutubia taifa: Anawashukuru watu mbalimbali pamoja na tume ya uchaguzi ZEC na waangalishi wa uchaguzi, chama chake CCM kwa kumuamini na kumteua kugombea nafasi y urais, Dr Shein anawapongeza wanzanzibar kwa kumchagua na kwa kutumia haki yao ya kikatiba ya kupiga kura na kusherekea ushindi kwa amani na utulivu.
Kusimamia amani ndio kipaumbele cha serikali atakayoiunda na serikali haitamvumilia mtu yeyote atakayevuruga amani.
Rais Dr Ally Mohamed Shein anamaliza kuhutubia na wanakaribishwa vijana wa Yamoto Band kuja kutumbuiza.
Vingozi mbali mbali wanaanza kuondoka uwanjani kwa kufuata ITIFAKI.
MWISHO.