Yaliyojiri Kutoka Ufipa: Mkutano wa CHADEMA na waandishi wa habari, maandamano ya UKUTA yaahirishwa

Mpaka leo hii bado najiuliza maswali na sipati majibu, akili za wenzetu waliokuwa wanamnadi fisadi lowasa kupitia chadema zilikuwa wapi?
Yaani kweli kabisa mlitaka Mbowe, tundu na fisadi lowasa ndiyo wawe na sauti ya mwisho hapa Tanzania? Mlitaka kuikabidhi hii nchi kwa mbowe, lowasa&Co.? Nafikiri ubongo wenu utakuwa unashambuliwa na vijidudu na nina washauri mkafanye head CT Scanning!
Bora hao kuliko hizi sauti za mwisho tunazozisikia leo.
 
Mnamo tarehe 27/7/2016 mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) alitangaza kwamba tarehe 1/9/2016 itakuwa ni siku ya maandamano na mikutano ya hadhara nchi nzima kwa chama chake na wapenda demokrasia wote nchini ili kupnga udikteta unaodaiwa kufanywa na Rais Magufuli. Hakika maandalizi yalikuwa motomoto nchi nzima kwa kupanga safu ya viongozi watakao si tu wakaosimamia zoezi hilo bali pia kuongoza maandamano hayo nchi nzima juku jeshi la polisi likipiga marufuku maandamano hayo pamoja na mikutatano ya vyama vya siasa kwa lengo la kuimarisha amani ya nchi pamoja na kuwaruhusu wanachi wafanye kazi kwa amani. Wapenzi wa UKUTA walikamatwa kila kona kwa madai ya uchochezi na wengi walifunguliwa kesi za uchochezi kila kona ya nchi.

Viongozi wa upinzan waliishutumu serikali kuvunja katiba ya nchi ya mwaka 1977 pamoja na sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 bila kuweka wazi ni ibara gani inavunja na ni kifungu gani cha sheria kinachovunjwa.

PONGEZI KWA MBOWE

1. Mbowe baada ya kupitia kwa kina katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 aligundua kuwa ibara ya 10 inayohusu Nafasi na Mamlaka ya Chama imefutwaa na sheria Na.4 ya 1992 hivyo madai ya kikatiba hayakuwa na uhalali
2. Mbowe pia alipopitia sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992(the political parties act 1992) kifungu cha 11 "11. (1) Every party which has been provisionally or fully registered shall be
entitled
a)to hold and address public meetings in any area in the United Republic after
giving notification to the police officer in-charge of the area concerned for
purposes of publicizing itself and soliciting for membership" akaona ili maandamano yawe kisheria lazma kuwe na baraka za jeshi la polisi bila hivo maandamano yake yalikuwa hewa
3. Mbowe pia alipitia sheria ya heshi la polisi Sura ya 322 kifungu cha 43. "(1) Mtu yeyote ambaye ana mpango wa kufanya, kukusanya, kuunda au kupanga mkusanyiko au maandamano ya hadhara , kwa muda usiopungua saa 48 kabla ya mkusanyiko au maandamano kwa muda uliopangwa kuanza, atawasilisha kwa maandishi notisi kuhusu kufanyika kwa mkusanyiko au maandamano hayo kwa afisa polisi msimamizi wa eneo hilo akianisha:-
(a) sehemu na muda ambao mkutano utafanyika;
(b) dhumuni kwa ujumla kuhusu mkutano huo; na
(c) maelezo mengine kama Waziri atakavyotangaza kwa notisi, mara kwa mara kwenye gazeti la Serikali, kuainisha.
(2) Pale ambapo mtu anawasilisha taarifa kulingana na kifungu kidogo cha (1), anaweza kuendelea kuitisha, kukusanya, kuunda au kuandaa mkusanyiko au maandamano hayo kama yalivyopangwa isipokuwa na mpaka atakapopokea amri kutoka kwa afisa polisi msimamizi wa eneo ikielekeza kwamba mkusanyiko au maandamano hayo hayatafanyika kama ilivyotaarifiwa" ,,Mbowe akaona anapotea na nafsi ikamsuta
4. Mbowe alituma vijana wake kufanya utafiti ili kuona muitikio wa watu mitaani kuhusu UKUTA,majibu yalikuwa ni kwamba wananchi hawataki kabsa si tu kushiriki Ukuta bali pia hata kuusukia,,nampongeza mbowe kwa usikivu

Nampongeza zaid Mbowe kwa usanii alioufanya kwenye kuahirisha UKUTA kwa kuwasingizia viongozi wetu wa dini

Vyama vya upinzani nchini kwangu fanyeni siasa acheni kutafuta kick

by Ogulu
kwa maana hiyo Intelijensia ya Mboe inapita ya Polisi maana polisi walishindwa kubaini hilo mpaka wakaingia gharama ya kujiandaa nchi nzima kupambana na UKUTA ambapo kwa mawao yako haukuwepo
 
Yalikuwa ni makosa makubwa sana fikiria na kuwapa nchi watu kama hawa. Hivi watu walirogwa au ilikuwaje? Bado siamini ninachokiona kila nikikimbuka hali ilivyokuwa wakati wa kampeni.
 
Kama sifa ya kuwa kiongozi wa chama cha upinzani Tanzania ni ulaghai basi Mbowe amefanikiwa kuwa laghai na mtu asiyemaanisha aliyoyapinga.

Mara kadhaa amekuwa akipaza sauti na shingo kupinga ufanisi mdogo wa mashirika na taasisi za serikali kumbe nyuma ya pazia amenufaika na hali hiyo. Ni mmoja wa watu wenye kukwamisha mashirika ya umma kama NHC na NSSF kwa tabia yake ya kutumia huduma/kukopa lakini hana rekodi nzuri kulipa madeni (first class defaulter).

Nimeamini kuwa kumbe nayeye ni jipu kubwa tu,na imegfika wakati wa kutumbuliwa.
 
Ukuta umeangukia Jengo la Bilicanas watu kadhaa wamejeruhiwa akiwemo Salum Mwalimu alielazwa Mkoani Simiyu
 
kwa maana hiyo Intelijensia ya Mboe inapita ya Polisi maana polisi walishindwa kubaini hilo mpaka wakaingia gharama ya kujiandaa nchi nzima kupambana na UKUTA ambapo kwa mawao yako haukuwepo
Jeshi la polisi siku nzote linajipanga kupambana nja uhalifu ndo maana wanakaa kambin na wanapewan mafunzo maalum,,,
 
Kufuata sheria ndio kufanya siasa ?! Huyu aliyezuia siasa kafuata sheria gani kama siyo kick vilevile ?!

Kuwa fair hata kwa nafsi yako tu.

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
hakuna mwenye mamlaka ya kuzuia siasa ila kilizuiliwa na jeshi la polisi ni mikutano na maandamano ya siasa na hao ndo wenye mamlaka ya kuzuia (soma sababu ya kumpongeza mbowe no.3)
 
Habari wakuu,
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, dakika chache zijazo kuna mkutano wa waandishi wa habari makao makuu ya chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA). Tuwe pamoja kujuzana yatakayojiri.

========

UPDATES;

Amaeongea kwa sasa ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa na anaongelea uamuzi wa jeshi la wananchi kufanya usafi na urushaji wa ndege siku ya leo ambayo anasema haijawahi kufanya tangu uhuru.

Anasema anavyozungumza, katibu mkuu(Salum Mwalimu) anaendelea kushikiliwa na polisi mji wa Bariadi na ilikuwa leo apelekwe mahakamani lakini polisi wamesema wako bize.

Freeman Mbowe amesema maandamano ya UKUTA yameahirishwa kwa mwezi mmoja hadi tarehe Oktoba Mosi.

Mbowe: Tumepata wakati mgumu kufikia uamuzi, sio kila wakati viongozi tutafanya mambo yatayowapendeza wanachama wetu. Viongozi wa dini awali walikuja na ajenda moja, kuomba wabunge wa UKAWA warejee bungeni. Kamati kuu ya CHADEMA imepokea kwa heshima sana wito wa viongozi wa dini.

Mbowe: Ni matumaini yangu wana CHADEMA watatuelewa kamati kuu, asanteni sana kwa kunisikiliza.

Kinachoendelea kwa sasa ni maswali kutoka kwa waandishi wa habari.

Kwa nini hamjapeleka shauri mahakamani: Mbowe: Yamepelekwa mashauri mengi mahakamani na yataendelea kupelekwa. Hatuwezi kuwalazimisha mahakama, hata kipindi hiki kuna mashinikizo kwa baadhi ya mahakama watoe maamuzi watoe maamuzi yanayorandana na serikali, wapo waliosimamia sheria lakini mahakimu nao ni binadamu.

Mimi ni miongoni mwa watu ambao tulitamani kesho watu wawe barabarani, wanachama wetu ambao watakwazika, UKUTA sio CHADEMA, UKUTA ni mchanganyiko wa makundi mbalimbali ya watanzania. Sasa hayo makundi yamekuja kutushauri tuwe pamoja, sisi ni nani tukatae. Watu kama Mwl Nyerere foundation wametusihi, hata Lowassa amaengea na mama Maria Nyerere wametusihi.

Mbowe: Viongozi waliomba wiki mbili mpaka tatu lakini sisi tukasema hapana kuna wengine tutakuwa na majukumu bungeni na hili jambo ni la kitaifa. Hatuna nia ya kuchafua Taifa, tuna nia ya kusaidia Taifa.

Mbowe: Mpaka jana tulikuwa na viongozi 230 amabao wameshtakiwa, viongozi 28 mapaka jana walikuwa hawajaachiwa kwa mujibu wa takwimu zetu akiwemo naibu katibu mkuu Zanzibar.

Mbowe: Nisikitike siku za karibu mahasimu wetu wamekuwa wakijaribu kutugombanisha ndani ya CHADEMA, hizi fitna za mitandao. Mbowe sina tabia ya kutoa matakamko nje ya taratibu za chama, Tamko nililotoa ni la leo.

Lowassa: Mitandao inaandika mambo mengi sana ambayo ni just accusations, ningekua na muda ningefafanua.



Ndugu wanahabari,

Tarehe 27 Julai ya mwaka huu Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ilitangaza azimio la kuanzisha harakati tulizozipa jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (UKUTA). Pamoja na mengine, azimio hili lilipitishwa kufuatia tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kupiga marufuku mikutano yote ya vyama vya siasa katika nchi yetu hadi mwaka 2020. Kama mnavyokumbuka, Kamati Kuu yetu iliteua siku ya Septemba Mosi, yaani kesho, kuwa ni siku rasmi ya kuanza kwa harakati za UKUTA ambazo zingejumuisha mikutano ya hadhara na maandamano ya amani nchi nzima.

Kufuatia azimio la Kamati Kuu ya CHADEMA, mambo mengi sana yametokea. Mengi ya mambo haya ni ya ajabu na ya kusikitisha sana. Tumemwona Rais wa Jamhuri ya Muungano, aliyekula kiapo cha ‘kuilinda, kuihifadhi na kuitetea’ Katiba yetu na Sheria zake, ‘akiikanyaga’ Katiba hiyo hadharani kwa kutishia kwamba mtu yeyote atakayefanya mikutano na maandamano ya amani ‘atakiona cha mtema kuni.’

Tumeshuhudia Jeshi la Polisi, ambalo lina wajibu kisheria wa kutoa ‘ulinzi na msaada’ ili kuwezesha mikutano kufanyika kwa amani na utulivu, likizunguka mitaani mijini na vijijini na kutembeza hadharani magari ya deraya na silaha nyingine nzito za kivita kwa lengo la kuwatisha wananchi wanaopanga kutekeleza kile ambacho Katiba na Sheria za Tanzania zinawaruhusu kukifanya, yaani, mikutano ya hadhara na maandamano ya amani.

Tumeona kwa mshangao mkubwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likitoa tamko la vikosi vyake vyote nchi nzima kufanya usafi siku ya Septemba Mosi, wakati Jeshi hilo lilikwishafanya maadhimisho rasmi ya Sikukuu ya Mashujaa tarehe 25 Julai. Na tangu alfajiri ya leo hadi muda huu, JWTZ imerusha ndege za kivita katika maeneo yote ya Dar es Salaam, kitu ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya majeshi yetu.

Na wote tu-mashahidi wa jinsi ambavyo viongozi wa ngazi zote wa CHADEMA na wanachama wa kawaida wamekamatwa, kuteswa na kufunguliwa mashtaka ya uonevu kwa sababu tu ya kutetea au kutekeleza haki na uhuru wao kwa mujibu wa Katiba yetu. Aidha, tumeona matukio mabaya ya kihalifu – ya kweli ama ya kutengenezwa – yakihusishwa kwa makusudi na UKUTA ili kutengeneza mazingira ya kiusalama ya kuhalalisha ukiukwaji wa Katiba na Sheria zetu na vitendo vya kutesa waTanzania na kukiuka haki zao za binadamu.

Vile vile, kila mmoja wetu ameona sio tu mikutano ya hadhara na maandamano ya amani, ambayo imewekewa utaratibu wa kisheria, bali pia mikutano ya ndani ya vyama vya siasa, ambayo haijawekewa utaratibu wowote wa kisheria, ikikatazwa na Jeshi la Polisi. Mahali pengi katika nchi yetu, mikutano ya CHADEMA ya aina hiyo imevamiwa na kuvunjwa na Jeshi la Polisi na viongozi na wanachama wetu kukamatwa ama kupigwa na kuumizwa vibaya.

Ni juzi tu kikao cha pamoja cha Kamati Kuu yetu na Wabunge wetu kimevamiwa na polisi na viongozi wa ngazi za juu wa Chama kama vile Mwenyekiti wa Chama Taifa, Mh. Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dkt. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu John Mnyika na wajumbe wa Kamati Kuu Mh. Edward Lowassa na Prof. Mwesiga Baregu kukamatwa na kuhojiwa na polisi.

Na hivyo tunavyozungumza, Naibu Katibu Mkuu wetu Zanzibar, Mheshimiwa Salum Mwalimu na viongozi wengine wa chama chetu, wako rumande Bariadi mkoani Simiyu tangu wiki iliyopita, kwa sababu ya kunyimwa dhamana kwa kosa ambalo sheria iko wazi kwamba lina dhamana.

Sio tu uhai wa mfumo wa vyama vingi vya siasa ambao uko hatarini. Uhuru wa vyombo vya habari umeshambuliwa sana katika kipindi hiki. Ndani ya mwezi huu mmoja, gazeti la Mseto limefungiwa na vituo vya radio vya Radio 5 ya Arusha na Magic FM ya Dar es Salaam vimefungiwa kwa kutangaza habari zinazohusu UKUTA.

Ndugu wanahabari,
Yaliyofanywa na Rais Magufuli mwenyewe na Jeshi la Polisi yamefanywa pia na viongozi wa serikali wa ngazi za chini ya Rais, kama vile mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya. Hawa nao wametoa matamko ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara na kutoa amri za kuwakamata viongozi na wanachama wetu watakaofanya mikutano hiyo. Taasisi za nchi yetu ambazo zina wajibu wa kulinda haki za vyama vya siasa na haki za binadamu kwa ujumla zimejionyesha wazi wazi kutokuwa na uhuru unaohitajika katika utekelezaji wa majukumu yao ya kisheria na kikatiba.

Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye, kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa, ana wajibu wa kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo, ameshindwa kabisa kulinda na kutetea haki za vyama vya siasa za kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ya amani. Badala yake, Msajili Francis Mutungi amejidhihirisha kuwa adui mkubwa wa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi katika nchi yetu, kwa kuunga mkono matamko batili ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara na maandamano ya amani.

Kwa kifupi, katika kipindi cha takriban mwezi mmoja tangu kutangazwa kwa UKUTA, tumeshuhudia Tanzania yetu ikiserereka kwa kasi kwenye mteremko mkali wa utawala wa kidikteta.

Ndugu wanahabari,
Katika mazingira haya, taifa letu limeingia katika taharuki kubwa. Watanzania wa kila rika na wa kila kundi la kijamii wameingiwa na hofu kubwa ya nchi yetu kuingia katika machafuko ya kisiasa na umwagaji damu mkubwa endapo siku ya Septemba Mosi, yaani kesho, tutatekeleza azimio letu la kufanya mikutano ya hadhara na maandamano ya amani nchi nzima, na majeshi ya ulinzi na usalama yakatekeleza azma yao ya kutumia mabavu ya kijeshi kuzuia au kuzima mikutano na maandamano hayo ya amani.

Ndugu wanahabari,
Kwa sababu ya taharuki hii na ombwe kubwa la uongozi wa kisiasa lililojitokeza tangu tutangaze UKUTA, viongozi wakuu wa kidini wa madhehebu mbali mbali ya dini zote kubwa hapa nchini, yaani, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Mkuu wa Kanisa la Kianglikana Tanzania, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Katibu Mkuu wa Baraza la Kikristo Tanzania (CCT), Mkuu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT), Katibu Mkuu wa Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT), Mkuu wa Makanisa ya Kipentekoste ya Karismatiki, Mufti Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Mufti Mkuu wa Zanzibar, wametuomba na kutusihi, katika vikao mbali mbali tulivyofanya pamoja nao, tuwape muda wa wiki mbili au tatu, ili waweze kufanya jitihada za kuonana na Rais Magufuli kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huu wa kisiasa, ili kuliepusha taifa letu na machafuko ya kisiasa na umwagaji damu, utakaosababishwa na matumizi ya nguvu za kijeshi yanayotishiwa na Rais Magufuli na majeshi yetu ya ulinzi na usalama.

Aidha, sio viongozi wa kidini tu ambao wametuomba kuahirisha UKUTA kwa muda. Viongozi wa taasisi za kiraia kama vile Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Jukwaa la Wahariri na Jukwaa la Katiba nao wametusihi tuahirishe UKUTA kwa muda, ili tutoe fursa kwa jitihada za mazungumzo na majadiliano kufanyika.

Sisi CHADEMA tunatambua na kujali haki zetu za kisiasa kama zilivyofafanuliwa katika Katiba na Sheria za nchi yetu. Hata hivyo, tunajali na kuheshimu kwa kiasi kikubwa zaidi, haki ya waTanzania ya ‘kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yao’ kama ilivyotamkwa na ibara ya 14 ya Katiba. Tunatambua mchango mkubwa ambao umetolewa na dini zote hapa nchini katika kutunza utulivu uliopo Tanzania na katika ustawi wa kiuchumi na kijamii wa waTanzania. Tunaelewa rai ya viongozi wetu wa kiroho juu ya umuhimu wa kutafuta suluhu ya mgogoro huu wa kisiasa kwa mazungumzo na majadiliano.

Tofauti na wengine ambao wamekataa hata kuwaona viongozi wetu wakuu wa kidini, sisi tunawaheshimu viongozi wetu wa kidini. Tumekutana nao. Tumesikiliza na kutafakari wito wao wa kuahirisha UKUTA kwa wiki mbili au tatu, ili wapate fursa ya kuzungumza na Rais Magufuli na Serikali yake. Huu ni wito wa busara na wenye kulijali taifa letu na watu wake. Sio wito unaopaswa kupingwa kwa sababu nyepesi nyepesi.

Tofauti na wengine, sisi wa CHADEMA hatuwezi kuwakaidi viongozi wetu wa kidini katika wito wao huu wa busara.

Kwa sababu hizi zote, tunaomba kuwatangazia viongozi wetu wa ngazi zote za CHADEMA, pamoja na wanachama, wafuasi na mashabiki wetu na waTanzania wote popote walipo, kwamba tunaahirisha kwa mwezi mmoja mikutano na maandamano ya amani yaliyopangwa kufanyika nchi nzima kuanzia kesho Septemba Mosi, ili kutoa nafasi kwa viongozi wetu wa kiroho kutafuta suluhu ya jambo hili kwa kukutana na Rais Magufuli na Serikali yake.

Endapo jitihada za viongozi wetu wa kidini hazitazaa matunda katika kipindi hicho, mikutano na maandamano hayo ya amani sasa yatafanyika kuanzia Oktoba Mosi ya mwaka huu. Tunawaomba viongozi na wanachama wetu nchi nzima waendelee na maandalizi mbali mbali kwa ajili ya UKUTA katika maeneo yao.

Aidha, tunarudia wito wetu kwa vyama vingine vya siasa, taasisi na mashirika ya kiraia yasiyokuwa ya kiserikali, taasisi za kitaaluma za aina mbali mbali, vyombo vya habari na waTanzania katika ujumla wao, kujiunga na UKUTA na kutetea Katiba yetu na haki za binadamu. Tunasisitiza tena: hakuna atakayepona endapo Rais Magufuli atafanikiwa kuangamiza mfumo wa vyama vingi vya siasa katika nchi yetu kama alivyodhamiria.

Hakuna atakayekuwa salama endapo Rais Magufuli ataruhusiwa kukanyaga Katiba yetu, kupuuza sheria za nchi yetu na kukiuka haki zetu za binadamu kama anavyotaka. Kama inavyotamka Katiba yetu, ‘kila mtu ana haki, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria, kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria za nchi.’ UKUTA ni sehemu ya hatua hizo za kisheria za kuhakikisha hifadhi ya Katiba na sheria zetu. Tujenge UKUTA ili tuokoe nchi yetu.

--------------------------------

FREEMAN AIKAELI MBOWE (MB)
MWENYEKITI TAIFA




at the end of the day ujumbe umefika,
demokrasia ya afrika ni shidaaaa
 
Kwakuwa aliyetangaza kuwepo na kusitishwa kwa UKUTA ni Mbowe, na kwakuwa kuna makamanda walichukua mikopo ili waprint t-shirt za UKUTA kama kujiajiri lakini t-shirt hizo zimekosa soko maana ukionekana umevaa tu ni sawa na umebeba bangi, Kamanda Mbowe inabidi uwafidie wajasiriamali hao.
 
Inahitaji ujasiri mkubwa kuamini anachosema Mbowe. Kwa mfano sasa kasema ni October Mosi wakati anajua fika hamna kitu kama hicho.
 
Kwakuwa aliyetangaza kuwepo na kusitishwa kwa UKUTA ni Mbowe, na kwakuwa kuna makamanda walichukua mikopo ili waprint t-shirt za UKUTA kama kujiajiri lakini t-shirt hizo zimekosa soko maana ukionekana umevaa tu ni sawa na umebeba bangi, Kamanda Mbowe inabidi uwafidie wajasiriamali hao.
Bado zitatumika siku ya kupanda miti kitaifa tarehe 01 October. Kuwa na subira!
 
Back
Top Bottom