Yaliyojiri katika Mkutano wa CHADEMA, Mbeya

Dec 11, 2010
3,321
6,330
Wakuu,

Leo CHADEMA wanafanya mkutano wa hadhara jimbo la Mbeya mjini, nia ni kuendelea kushtaki uonevu unao fanywa na kiti cha spika.

Mkutano unafanyika kwenye kiwanja maarufu kilicho pewa jina la DR slaa.

YANAYOJIRI:

• Maandamano makubwa yametusua katikati ya jiji la Mbeya.

• Watu ni wengi sana! Kama kawaida wanakuja kusikiliza kile wanacho kikosa kwenye vyama vingine.

• Dr slaa anaonekana ni kipenzi cha wana Mbeya! Naomba niweke hakiba ya maneno!

• Mkiti wa Mbeya Mjini, Mwambigija anafungua mkutano: watu wa Mbeya wasingemwelewa Mbunge wao Sugu iwapo asingeinuka bungeni kwenda kuzuia udhalimu na uminyaji haki wa kiti bungeni! Wasingemwelewa!

• Anasema muda wa CCM kutawala umesha-expire, kila mtu anajua hivyo. Amewataka polisi kuacha mpambano wa kuwania udiwani wa CHADEMA na CCM, wasiingilie kati kupendelea na kuibeba upande mmoja.

• Dkt. Slaa kailipua ikulu kwa matumizi ya kifisadi ya bil. 29, fedha ambazo zimewekwa kwenye kitengo kipya cha Presidential Delivery Beareu! Zingeweza kujenga madarasa 4142 Shule ya Msingi, 2071 sekondari, zahanati 580, vituo vya afya 290, bila kuwachangisha wananchi hata senti!

• Dkt. Slaa kamlipua Waziri wa Maji Maghembe kwa kujipelekea mradi wa maji wa bilioni 50 jimboni kwake, wkt miradi mingine ya maji nchi nzima imetengewa bil. 4 tu

• Dkt. Slaa amesema Mwakyembe alilazimisha kampuni ya CCM Jitegemee Trading Company, kupata zabuni kwenye eneo la CCM, SUKITA thamani ya bil. 10 kwa kauli ya kushnikiza ''tuwasaidieni tu''

attachment.php

photo.JPG
 
Nipo kwenye gari hapa foleni inaelekea mkutanoni!!! ndio habari ya mjini sahizi kuwa chadema wana mkutano hapa Mbeya!!
 
mkutano upo maeneo ya ccm na watu tunaelekea huko, mambo yatakwenda sawa tu.

mkuu utupe mapicha basi ukifika kadri mambo yanavyokwenda, mbeya ni kama arusha tu hakuna cha kupoteza, pamoja mkuu..... Usishau ajenda zinazojadiliwa,....utupie tujifunze
 
Tupo mambo mkuu bila kusahau kutujulisha ukubwa wa nyomi la watu leo likoje coz iringa ilikuwa noma kama ilivyokuwa mwanza. Endelea kutujuza kamanda
 
Tupia images/pictures kuonyesha tofauti ya wao bila diamond plutnumz mikutano haiendi sisi tunakwenda kwa hiari ya watanzania.
 
Mkuu, kamanda Tumaini Makene anakuwa na mambo mengi, mtu yoyote anaweza kutupatia updates kama ilivyo kawaida yetu, kamanda anajitahidi kufanya hivya kadri inavyowezekana...

Mkuu the Late Regia alikuwa na mambo mengi pia, lakini nadhani planning zake zilikuwa zinamfanya atimize vizuri majukumu yake kwa wakati.Makene got a lot to do for us,utamaduni wa cdm ulioanzishwa na dada yetu lazima wengine wauenzi kwa kufanya kwa namna ile ile lakini kwa ufanisi.
 
Back
Top Bottom