Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao cha 11mkutano wa 3
Maswali na majibu
Swali: Dr Kawambwa, Rais aiwaahidi kambi ya mkandarasi iliyopo Makofia kuwa shule ya msingi taratibu zimefikia wapi?
Majibu: Dhamira ya serikali kuhakikisha majengo ya mkandarasi kutumika katika shughuli za kijamii mara baada ya kumaliza mradi serikali inaendelea kukamilisha kwa mijubu wa taratibu
Swali: DR Hajji Mponda, Je kiasi gani kimejengwa kwa barabara za Kilombero na daraja lake?
Majibu: Kuanzia mwaka wa fedha 2010-2011 na 2015-2016 serikali iliandaa fedha na mradi huu ulipangwa kumamilisha mwezi june mwaka jana na kutokana na upungufu wa fedha mkandarasi alishindwa kukamilisha na serikali itaendelea kumlipa mkandarasi kwasababu madeni yamekwisha, pia ujenzi wa daraja umesimama baada ya bonde la mto Kilombero kujaa maji kwa sasa.
WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI
Swali: Je serikali inamkakati gani kutatua tatizo la maji mkoani Arusha?
Majibu: Serikali imepata mkopo wa Dola Milioni 216 ili kuwezesha mkoa wa Arusha na viunga vyake kupata maji safi na ya uhakika. Serikali imeshapata muhandisi mshauri na ujenzi kuanza mwaka wa fedha 2016-2017
WIZARA YA KATIBA NA SHERIA
Swali: Majengo mengu mahakama za mwanzo yamechakaa serikali inaandaa mkakati gani kuyarekebisha na mahakama ya Kisutu imeelemewa na kesi nyingi serikali inajipanga vipi kupunguza mzigo wakesi.
Majibu: Serikali inampango wa kuboresha mahakama kwa mwaka fedha 2015-2020 na fedha zimepangwa kukarabati mahakama za wilaya 12, Serikali inampango wa kujenga mahakama mpya ya Kinyerezi ili kupunguza kesi za Kisutu
Swali: Je ni utaratibu upi uliotumiwa kuzuia malipo ya majaji kwa asilimia 80
Majibu: Katiba ya JMT imeelezea kuwa malipo ya majaji yalipwe kupitia mfuko wa serikali, sheria zinafafanua kuwa malipo ya majaji wastaafu wa mahakama kuu na mahakama ya rufani. kwa jaji mstaafu asilimia 80 hulipwa kwa utaratibu wa namna alivyochangia.
Swali: Je serikali lini itajenga mahakama ya wilaya ya Rufiji, na serikali imejipanga vipi kuboresha maslahi ya mahakimu?
Majibu: Wizara inaelewa shida ya wilaya ya Rufiji kuhusu Mahakama na mpango wa maendeleo ya mahakama 2015-2020 wilaya ya Rufiji itazingatiwa na ili kukidhi matakwa ya kimataifa na kikatiba lazima majaji walipwe vizuri ili kuepusha vishawishi na upende wa mahakimu bado serikali inaendelea kuboresha maslahi yao.
Swali: Kumekuwa na uchimbaji wa madini katika mgodi wa North Mara chini ya kampuni ya Acacia na mchimbaji hana kibali cha kudumu ingawa anachima madini kwa zaidi ya mwaka sasa
Majibu: Uchimbaji wa madini ktk mgodi wa North Mara ulianza kufanyika zaidi ya mwaka mmoja uliopita na mgodi haukuwa na mkataba wa uchimbai wa madini. na sheria inamtaka mchimbaji kubadiri kibali chake na kupata kibali cha kudumu. Serikali itaendelea kusimamia uchimbaji wa madini katika mgodi huo.
Swali: Lini serikali itauamuru mgodi wa North Mara kuanza kuanza kulipa fedha kwa serikali za vijiji. Na kutoa tamko juu ya uchafuzi unaofanywa na mgodi katika mazingira ya mto Kokona.
Majibu: Mikataba iliyoingiwa kati ya vijiji saba na kampuni ya Acacia ni mikataba ya uchimbaji kwa muundo wa royalty. Na baada ya NEMC kutembelea na kugundua uchafuzi wa mazingira na kamati ya watu 27 imeundwa na serikali tarehe 22 ili kuchunguza uchafuzi wa kimazingira katika mazingira ya mto Kokona na pia fedha ambazo kampuni hulipa katika vijiji ni wa aina ya Royalty na wanalipwa kwa asilimia moja.