Yaliyojiri Bungeni Dodoma leo tarehe 22 Aprili, 2016

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao cha 4, mkutano wa 3

Kipindi cha maswali na majibu

Swali:
Mh Chegeni kuna waalimu zaidi ya 3000 wamestaafu na ni lini watalipwa stahiki zao
Majibu: Serikali imetoa maelekezo kwa mfuko wa PSPF kulipa haraka stahiki zao, na hii ni kwa mifuko yote nchini

Swali: Halmashauri ya mbeya vijiji vingi havijanufaika na mradi wa REA ni lini watajumuishwa kwenye mradi huu.
Majibu: Kuna shule za msingi na sekondari, vituo vya afya na nyumba za ibada pamoja na jumla ya vijiji 11 vya mbeya vimejumuishwa kwenye awamu ya 3

Swali: Wizara inampango gani wa kusambaza umeme kwenye vitongoji na kutokana na ungezeko la watumiaji wa umeme je wizara inaandaa mpango gani kuongeza watumishi na vifaa TANESCO?
Majibu: Kuna miradi mingine kama UNDERLINE ili kupitia maeneo yaliyoachwa na REA, kwasasa hivi TANESCO inaongezewa uwezo wa vifaa na miradi mingine inaimarishwa

Swalli: Je lini itapeleka umeme wa REA kwenye kata za jimbo la Mikumi
Majibu: Vijiji vyote vitakavyobakia kwenye mradi wa REA awamu ya pili vitakamilishiwa huduma ya REA kwenye awamu ya 3. na kufikia mwaka 2025 vijiji visivyo na umeme vitakuwa vya kutafuta.

Swali: Je kufika June miradi ya umeme itakuwa imekamilika jimbo la Chemba?
Majibu: Vijiji vilivyosalia kwenye mradi wa REA awamu ya pili vinatambuiwa na kujumuishwa kwenye mradi wa REA awamu ya 3

Swali: Nini kinasababisha ucheleweshwaji wa pembejeo kwa wakulima na serikali imejipangaje?
Majibu: Mawakala kutokulipwa wa wakati, uatatibu wa kupata vocha ni mrefu na huchukua muda mwingi serikali inachukua hatua kutatua hili. Na serikali imeandaa utaratibu wa kuchagua mawakala wa pembejeo kufikisha pembejeo kwa wakati. Mfumo wa pembejeo umekuwa na mapungufu serikali imelenga kufikisha pembejeo kwa wakati na kuwafikia wakulima wengi zaidi na zianze kupatikana kwenye maduka ya kawaida.

Swali: Je wanazania wangapi wanajulikana wako Ughaibuni na wanachangiaje pato la taifa
Majibu: Watanzania walionje ya nchi wanakadiriwa kufikia milioni 1, Wizara inaendelea kuhamasisha watanzania wanaoishi ughaibuni kuchangia pato la taifa na kuja kuwekeza.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa:
Katika kitengo cha huduma ya Jamii Elimu, Waziri Majaliwa amesema ‘Kwa kutambua umuhimu wa Elimu kama nyenzo imara ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Serikali imeanza kuboresha na kuimarisha elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu.’

‘Baada ya kuanza utekelezaji wa mpango wa elimu bila malipo, kumejitokeza changamoto kadhaa, ikiwemo miundombinu kama madarasa, mabweni, maabara, nyumba za walimu na vyoo‘

‘Napenda kuwahakikishia wananchi kwamba Serikali inaendelea kuzifanyia kazi changamoto hizo na jitihada kubwa zimewekwa‘

‘Nitumie nafasi hii kuwashukuru wadau walioanza kuchangia madawati katika maeneo mbalimbali,na niwasihi wengine waendelee kuunga mkono Serikali yao‘

‘Kuanzia leo hii, nawaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wote waliokamata mbao ndani ya Halmashauri zao kuzitumia kutengeneza madawati na siyo kuzipiga mnada‘
 
Mambo ya bunge ni bora yapotezewe tu kutokurushwa live ni maumivu tu kwetu
Mkuu wanaturushia kipindi cha maswali maana ni majibu ambayo washayaandaa kitambo, sisi tunachotaka ni mijadala ile haswa. Mimi sina sababu ya kuangalia kipindi cha maswali na majibu.
 
Dikteta ameamua kutunyima haki ya kutazama wawakilishi wetu. Sina hamu pamoja na kuwa namuunga mkono kwenye mambo mengi ila hapo AMENICHEFUA.
 
Dikteta ameamua kutunyima haki ya kutazama wawakilishi wetu. Sina hamu pamoja na kuwa namuunga mkono kwenye mambo mengi ila hapo AMENICHEFUA.
Ndugu yangu ni wengi wamevunjwa moyo kwa jambo hili. Unajua unaweza kufanya mia mazuri yakaharibiwa yote na moja baya.Wanasema ubaya huenea kwa kasi kuliko uzuri.Kwa sisi tunavyouelewa ufanyakazi wa chama chao na mapungufu yao tunaamini baada ya June mwaka huu Magufuli atakapokabidhiwa kofia ya uenyekiti wa taifa wa chama chao mambo mengi yatabadilishwa sana na raisi.Unafahamu kutokana na urasimu na ubabe wa chama chao vikao vya juu vya chama hicho vina uwezo wa kuingilia maamuzi ya raisi aliyepo madarakani kabla ya kukabidhiwa uongozi wa chama kitaifa.Kwa sasa m/kiti wa chama taifa ni mh.Kikwete na endapo haitatokea figisu June mwaka huu atakabidhi kofia hiyo kwa Magufuli.Hii inampa uwezo raisi kufuata anavyofikiri ni kwa manufaa ya nchi na wananchi wake na anaweza akapokea ushauri na kuufanyia kazi au kuupokea na kuupima na kuuacha.Ni imani ya wengi kuwa kwa kutumia kofia zake mbili yaani chama chake kinachoongoza nchi na yeye akiwa raisi wake anaweza akaanza kukisafisha chama kwa kuwaondoa na kuwafutia uanachama mafisadi wengi waliojificha huko.Vivyo hivyo kuagiza tu rudisheni matangazo ya bunge kama awali na vituo binafsi kuruhusiwa mradi walipe na kufuata sheria.Sio hilo tu anweza kwa kuitumia kofia ya m/kiti taifa wa chama akalirejesha upya azimio la Arusha lenye misingi na miiko ya viongozi na kuagiza kulifutilia mbali lile la Zanzibar walikokimbilia wajanja na kujipa mamlaka za kuwa na hisa kwenye makampuni,kumiliki mabiashara makubwa kuanzia maduka,meli hadi migodi.Raisi akaliagiza bunge la katiba kuacha katiba wanayotaka kuipitisha na ambayo kiukweli ni maoni ya wabunge na baadhi ya wateule wachache kwa manufaa yao na chama chao na kuagiza ipitishwe ya jaji Warioba ambayo ndio maoni ya wananchi.Hakika hayo yakifanyika biashara ya kuviziana na majipu ya kutumbua itakuwa imeishia hapo hapo kwani yatakuwa yameshajitumbua yenyewe kwenye Azimio na Katiba na hakika muhula wake wa pili utahitaji kampeni kidogo tu.Hadi sasa tuzidi kumuunga mkono na kumwombea ulinzi kwa Mungu kwa kazi hii ngumu na hatari. HIYO NDIO ITAKUWA TAFSIRI SAHIHI YA HAPA KAZI TU.
 
Back
Top Bottom