Maswali na majibu
Swali: Serikali ina mpango gani wa kujenga kituo cha afya cha Chiwale ili wazazi wapate mahali pa kujifungulia?
Majibu: Serikali imetenga milioni 80, milioni 20 kutoka halmashauri, milioni 60 kutoka serikali kuu.
Aidha serikali inashughulikia suala la gari la kubeba wagonjwa katika kituo hicho kutokana na kwamba gari zilizokuwepo zilichomwa moto.
Serikali inakusudia kukamilisha ukarabati wa hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro.
Swali: Serikali haioni kwa kuwaweka wakunga wanaume ni kuwadhalilisha wanawake?
Majibu: Wakunga wote wa kike na kiume wanaruhusiwa kutoa huduma, serikali itaendelea kuajiri wakunga wengi zaidi ili kukabiliana na changamoto zilizopo.
Serikali inaendelea kupeleka wakunga wa kike penye wakunga wa kiume pekee.
Swali: Ni lini serikali itajenga kiwanda cha juisi Muheza?
Majibu: Serikali itaweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha wawekezaji kuwekeza eneo husika.
Kampuni ya Samsumua Holding imeanza mradi wa kuwekeza katika kilimo cha matunda mkoani hapo.
Serikali inakusudia kutembelea eneo hilo la kwa Msisi mkoani Tanga kujiridhisha na uwekezaji unaoendelea mkoani hapo.
Serikali inakusudia kutokomeza tabia ya nchi kuagiza toothpick kutoka nje. Serikali inakusudia kununua mtambo wa toothpick wa dola 18,000 na kutokomeza tabia ya kuziagiza kutoka nje.
Swali: Ni lini serikali itajenga senta ya michezo ya riadha mkoani Manyara?
Majibu: Serikali kupitia mkoa wa manyara imepanga kujenga kituo cha michezo kwa kushirikana na wananchi, aidha wanashughulikia kupatikana kwa eneo husika.
Maandalizi yakikamilika na mazungumzo yakikamilika, ujenzi utaanza.
Swali: Je serikali ina mpango gani wa kuhakikisha benk za TIB na TABB zinatekeleza azma yake?
Majibu: TIB imefanikiwa kutoa mikopo kwa mashirika mbalimbali ikiwemo shirika la Reli, TANESCO kupitia REA na kufadhili miradi mbalimbali ya kilimo nchini. Aidha TABB bado haijaanza kutoa mikopo kwa wakulima.
Swali: Ni lini TRA itaanzaisha ofisi zake wilayani Kilindi?
Majibu: Serikali ina mpango wa kukamilisha ofisi Kilindi na wilaya nyingine zisizokuwa na ofisi za TRA baada ya kukamilisha utafiti kuhusu fursa za mapato zilizopo wilayani humo. Aidha serikali inahitaji kufanya tathmini ya gharama za uendeshaji wa ofisi kabla ya kuanzisha ofisi.
Swali: Ni lini serikali itatoa fedha za kukamilisha miradi ya maji inayoendelea Tunduru?
Majibu: Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi hiyo, wizara imetuma fedha kwenye halmashauri kwa ajili ya kukamilisha miradi hiyo. Aidha serikali inakusudia kukamilisha miradi 11 ya maji iliyopo wilayani humo kabla ya kuanza miradi mipya. Pia serikali inakusudia kukarabati miradi yote ya maji nchini hasa katika jimbo la Singida.
Swali: Ni lini serikali itajenga barabara ya Mang'ola hadi Matala,
Majibu: Upembuzi yakianifu na usanifu wa kina tayari umenza na ujenzi utaanza mara moja baada ya hatua hii.
Aidha serikali imeagiza wakala wa barabara kurudisha mawasiliano ya barabara yaliyoathiriwa na mvua.
Swali: Ni lini serikali itakamilisha ujenzi wa kipande cha barabara ya Chaye hadi Tabora?
Majibu: Tayari ujenzi kwa kiwango cha lami umekamilika kwa baadhi ya maeneo mbalimbali unaendelea.
Maeneo mengine yanafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na ujenzi utaanza punde zoezi litakapokamilika.
Swali: Je serikali haioni sababu ya kuipandisha hadhi barabara ya Mlalo hadi Mashewa?
Majibu: Serikali inaendelea na utaratibu wa kuipandisha hadhi barabara hiyo na nyingie zilizowasilishwa wizarani.