Yaliyojiri Bungeni - 15 Mei 2015

Yaliyojiri Bungeni - 15 Mei 2015

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345
Kipindi cha kujadili bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tangu Jumanne hadi Jumamosi, Asubuhi wameanza na kipindi cha maswali na majibu, sasa ni zamu ya wabunge kuchangia...

Kwa ufupi, Miswada ya Takwimu na Makosa ya jinai Mtandaoni imekwisha sainiwa na Rais Kikwete kuwa sheria kwa mujibu wa Spika Makinda.

Kipindi cha kujadili bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, tangu Jumanne hadi Jumamosi

Wabunge wa Chama Tawala waliochangia hadi sasa wameunga mkono hoja, licha ya malalamiko yao!

Wabunge wa Chama Tawala waliochangia hadi sasa wameunga mkono hoja, licha ya malalamiko yao!

Sasa anaongea Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Suzan Lyimo.

Anazungumzia kasoro ya ilani ya Chama cha Mapinduzi kuhusu kilimo, anahoji uwepo wa Benki ya Kilimo ambayo ilahidiwa na ilani hiyo... Anawafananisha na matapeli!

Waziri wa Kilimo anatoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Bunge, taratibu za kuanzisha Benki ya Kilimo zilishakamilika... Ikiwemo kuajiri wafanyakazi na bodi ya Wakurugenzi, Mikopo imeshaanza kutolewa kupitia TIB!

Anahoji kitendo cha kitengo cha protokali kutengewa fedha kubwa kuliko sekta ya kilimo... Safari za nje zimekuwa nyingi sana!

Anazungumzia kusuasua kwa kilimo cha Umwagiliaji, kinyume na ahadi za Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Ilani ilikuwa inasema viwanda vingeongeza pato la taifa, lakini viwanda vingi vimekufa licha ya mahitaji kuongezeka!

Anasisitiza kuwa CCM imechoka

Elimu sio kipaumbele cha Serikali, wanajivunia majengo wakati malengo ya MMEM na MMES hayatimizwi...

Ilani inasema kufikia 2015 kila wilaya inatakiwa kuwa na chuo cha VETA, lakini hadi leo hilo halijatekelezeka

Kulikuwa na ahadi ya kupeleka magari kwenye vituo vya wazee, hilo halijafanyika hadi leo...

Mradi wa maji wa kutoka Igunga, Nzega hadi Tabora haujatekelezwa, lawama zake anazielekeza kwa Serikali ya Chama cha Mapinduzi

Kunatokea kurushiana vijembe Suzan Lyimo na Asunta Mshana, mwenyekiti wa Bunge amemkatiza Suzan kuzungumza

Sasa anazungumza Felix Mkosamali (NCCR Mageuzi): Anaunga mkono alichosema Suzan Lyimo

Analalamikia kitendo cha Bunge kupitisha bajeti ambayo haitekelezeki kila mwaka

Kama Watanzania wataichagua tena CCM, inabidi tutafute mshauri wa kupima uwezo wetu wa kufikiri - Mkosamali

Hakuna ambacho Serikali ya CCM imefanikisha, sio barabara wala maabara...

Anasema mambo mengi ambayo yanahusisha Serikali yana matatizo mengi, shule, usafiri, huduma na kadhalika!

Wizara ya Uchukuzi imezidiwa akili na wakurugenzi wa mashirika ya ndege kama Precision na FastJet. Serikali inaahidi kuchukua hatua lakini hakuna kinachofanyika!

BIG Results Now ni kiini macho. Anashauri fedha ambazo zilitumika kwenye mpango huo zingejenga barabara

Serikali imewadanganya wananchi wa Kigoma kuhusu barabara tangu mwaka 2005, miaka 50 ya Uhuru mkoa wa Kigoma umetelekezwa.

Anasema ni wakati wa wabunge wa CCM Mkoa wa Kigoma kuaga.

Serikali imejenga barabara mbovu, ahadi ambazo hazijatekelezeka!

Bado anaendelea kuipongeza Serikali ya awamu ya Nne, anatambua mchango wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika kuifanya Serikali iwajibike, licha ya mapungufu yake.

Analalamikia njaa iliyosababishwa na ukame wilayani kwake Simanjiro

Ngeleja: Kwenye ziara zangu kumejitokeza swali, moja ya kero zinzowakumba wavuvi ni ndoano zao kuitwa haram. Nyingi zinatoka nje ya nchi, kama ni haram kwanini zinaruhusiwa na kulipiwa kodi!

Kwenye bajeti, Serikali ya CCM ina shauku kubwa kutatua kero za wananchi ikiwemo maji na pale Sengerema kuna mradi mkubwa sana wa maji, mradi ule unakamilika mwishoni mwa mwaka na utakuwa umefikia pazuri katikati ya mwaka huu.

Ushauri, ajira kubwa inatokana na sekta ya kilimo hivyo serikali ijikite hapo, mikopo kwa wanafunzi elimu ya juu ni muhimu, Dar es Salaam inatakiwa kupewa hadhi ya kipekee kama uchumi zaidi ya asilimia 70 uko pale. Maelezo kwamba hii nchi imesimama, benki ya dunia kuwa Tanzania uchumi wake unatembea, nawaomba wenzangu wanapozungumzia waliangalie hili. Watanzania wanaendelea kusoma taarifa za hapa bungeni, wapinzani hawana mawazo mbadala, wanaomba tu ufafanuzi wa hoja hivyo watanzania waendelee kuamini serikali ya chama cha mapinduzi.

Akunay: Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi, bado niko imara, wapinzani wamechambua serikali kwa kutumia ilani yao. Ninashangaa wabunge wa CCM badala ya kuhoji wenyewe wanatetea wakati kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali. Uchaguzi mkuu 2015, hali halisi inaonyesha uandikishaji hautakamilika kabla ya mwezi wa kumi, nimeshangazwa na serikali kuagiza magari 777 ya polisi badala ya vifaa vya uandikishaji.

Naishauri serikali iwajali watu na sio wa kuwapiga mabomu, kuhusu katiba pendekezwa naishauri serikali iachane nayo. Serikali imesema imefanikiwa katika kutengeneza ajira, haiwezi kufauli kwa sababu hamna viwanda.

Watumishi halmashauri, mwaka jana tulirekebisha sheria na tukaruhusiwa kuajiri wafanyakazi wa kada za chini, lakini sheria inasema aajiriwe mtu anapotoka popote Tanzania na tukiajiri kutoka wilaya ya Mbulu eti tunafanya ukabili wakati lengo lilikuwa ni kuondoa gharama ya kumtoa mfanyakazi mbali. Sasa tumefanya nini na tunafanya nini?

Nizungumzie ahadi ya rais Mbulu, daraja la Magala liliahidiwa na rais na mpaka sasa bado ni matatizo. Aliahidi barabara ya Mbulu kwenda Hydom mapaka leo serikali inakaribia kumaliza muda wake bado.

Mgodo: Nimesoma kitabu cha hotuba ya waziri mkuu, sijawi kuona hotuba nzuri namna hii, ilani ya CCM imesema ili kupunguza msongamano Dar watajenga Flyover Ubungo na Tazara, ziko wapi?

Tumesema serikali ya CCM imeshindwa na haijaanza leo ila katika awamu hii ya nne imeshindwa zaidi, Kikuleta karibu hekari 500 linamilikiwa na waziri Lazaro Nyalandu na anawakodisha wanawake wajane 200,000 na nilipoenda kwa waziri mkuu, alisema wewe nenda na akanyanyua simu kuelekeza shamba lirudishwe mikononi mwa wananchi lakini hadi sasa ninavyoongea wanaendelea kuteseka. Serikali ya CCM imejenga matabaka, tunawadhalilisha wananchi kuwapa vizawadi vidogo vidogo ili wakuweke madarakani.

Eti ajira kwa vijana, kitabu kinasifia machinga. Hata mkopo atachukuaje, siamini kama mtaendelea kukaa madarakani baada ya October, siamini kama mnaweza kuleta maendeleo. Kuna matabaka pia katika wizi, kuna watu wanaiba hela nyingi na tuko nao humu ndani mpaka wanaombwa warudishe, kuna watu wakiiba mtaani vitu vidogo wanachomwa moto.

Godfrey Mgimwa: Watu wengi wamekuwa wanazungumzia serikali ilichoka, serikali isiyofaa. Niwahakikishie serikali hii inarudi 25 October. Ushahidi kadhaa, nilivyoingia jimbo la Kalenga kulikuwa na kata saba tu zilizokuwa na umeme, leo kuna nyingine nane. Leo hii wanakuja kusema serikali ya CCM haijafanya chochote. Mimi nadhani wao ambao wanashindwa kuangalia hata nguzo za umeme ndio wanahitaji consultant. Bado wapinzani wanasema wanaweza kuchukua, Jimbo la Kalenga tumewagaragaza kwa asilimia 99.

Masuala ya barabara tunaomba serikali iendelee kufanya kazi ya ziada kuboresha barabara Kalenga ikiwemo kupata lami baadhi ya sehemu(anazitaja), miradi ya maji iko mingi Kalenga na tayari imekamilika na wananchi wangu wanasubiri tu mabomba yafunguliwe. Pia serikali yetu iwaangalie wakandarasi wetu ambao malipo yao yanasua sua.

Taarifa(M. Machali): Sijakutana na Mgimwa kuzungumza nae anayoyasema maana wananchi wangu wana matatizo mengi.

Kiwia: Mnaweza mkatuchukia sisi lakini msichukie hoja za upinzani. Tukisema hamjafanya kitu haina maana hamjafanya kitu kabisa, ukitazama umri wa uhuru ya taifa letu, fursa tulizonazo na hali ya wananchi wa Tanzania, ndio maana tunasema hamjafanya kitu. Tunaposema serikali ya mapinduzi ni chovu, tuna ushahidi.

SHUGHULI ZA BUNGE ZIMESITISHWA MPAKA SAA 10 JIONI
 
TBC wameacha kuonyesha bunge kwa sababu wabunge wa upinzani wamezidisha matusi
 
Wabunge wa Chama Tawala waliochangia hadi sasa wameunga mkono hoja, licha ya malalamiko yao!

Mimi huwa hii kitu inanishangaza na kamwe sijawahi kupata mantiki yake.

Mbunge anasimama na kusema kwamba anaunga mkono hotuba ya WM kwa 100%

Halafu wakati wa kuchangia anaanza kulalamika tangu mwanzo wa hotuba yake hadi mwisho i.e. analalamika kwa 100%

Mbunge wa aina hii tumeweke katika kundi gani?
 
benki ya kilimo ipo na imeshaanza kukopesha cha ajabu inawakopesha wafanyabiashara.
nipo dodoma nimetembelea maeneo ya kizota nimeona yamejengwa maghala makubwa ya wafanyabiashara.
Inasemekana ni mkopo wa bank ya kilimo.
sasa nauliza ni kwa nini isiwakopeshe wakulima?
 
benki ya kilimo ipo na imeshaanza kukopesha cha ajabu inawakopesha wafanyabiashara.
nipo dodoma nimetembelea maeneo ya kizota nimeona yamejengwa maghala makubwa ya wafanyabiashara.
Inasemekana ni mkopo wa bank ya kilimo.
sasa nauliza ni kwa nini isiwakopeshe wakulima?

Wa Kimataifa hii bank imeanza lini na je washasambaa nchi nzima au bado mm nipo Mwanza nani Mkulima
 
Kauli aliotoa rais paul kagame kwamba kama atapewa bandari, ya daresalaam anaweza kuibadilisha tanzania na kuwa nchi ya mfano, kwa kutumia mapato yatayotokana na bandari hiyo, maneno hayo yalikuja kukumbushiwa na mbunge felix mkosamali alipokuwa anachangia hotuba ya waziri mkuu leo bungeni asubuhi, hivi ni kweli kagame akipewa hiyo bandari tu atatubadilishia nchi yetu kuwa ya mfano afrika, au ni dharau kwa viongozi wa tanzania?
 
Kauli aliotoa rais paul kagame kwamba kama atapewa bandari, ya daresalaam anaweza kuibadilisha tanzania na kuwa nchi ya mfano, kwa kutumia mapato yatayotokana na bandari hiyo, maneno hayo yalikuja kukumbushiwa na mbunge felix mkosamali alipokuwa anachangia hotuba ya waziri mkuu leo bungeni asubuhi, hivi ni kweli kagame akipewa hiyo bandari tu atatubadilishia nchi yetu kuwa ya mfano afrika, au ni dharau kwa viongozi wa tanzania?

Mm nahisi hapo kuna kitu anataka kukidhihirisha kwamba Bandarini ukusanyaji wa ushuru haupo Makin au kuna namna ya mwiz inafanyik a !!
 
kuana kitu kaona .. au kasha pitisha yake ya kutosha sasa anasanuka
 
Hata weye ungepewa secta hiyo na Tanesco nchi hii isingelikaa iombe msaada popote. Ukiisimamia kwa mwaka mmoja tu wananchi wanagawiwa pesa wale wasio na kazi
 
Back
Top Bottom