Maryam Malya
Senior Member
- Nov 29, 2021
- 115
- 258
Anaandika Dr. Sisimizi
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ameendelea kuwadanganya wanachama wake kuhusu suala la kutofanya mikutano yao kwa kutumia Chopa akidai kuwa anashughulikia kibali cha kuruka.
Nafikiri sasa umefika wakati wa Freeman Mbowe kuwafumbua macho wanachama wake na kuwaeleza sababu za ukweli zilizopelekea wao kushindwa kufanya mikutano yao na waache kisingizio cha kutafuta kibali cha chopa.
Ukweli ni kwamba ndani ya Chadema kumekua na mgogoro baina ya viongozi wa Kamati hasa suala linalohusu matumizi ya fedha.
Ndani ya Kamati Kuu ya Chadema, kumekua na mgogoro juu ya namna Pesa za chama zinavyotumika bila mpangilio kwa kisingizio cha kukodi chopa ambapo wanaamini gharama zinazotumika kwenye chopa haziendani na uhalisia.
Mbowe amekua akiwaambia wenzake kuwa huwa anakodi chopa hiyo kutoka nchini Kenya, kiasi cha shilingi Milioni 15 kwa siku, lakini safari hii amekodi kwa gharama ya shilingi Milioni 30 kwa siku hali ambayo imezua taharuki na maswali mengi kwenye kamati ya fedha ya chama hicho.
Kwenye ziara waliyoifanya Kanda ya Kati ambapo Chopa peke yake ilitumia zaidi ya Milioni 200 kwa wiki mbili tu, ambapo wapo waliodai gharama hiyo ni kubwa sana.
Baada ya Kamati ya fedha ya Chadema kuhoji kuhusu Chopa kutumia gharama kubwa, wakakubaliana wasitishe kwanza matumizi ya chopa mpaka pale Mwenyekiti wao atakapotoa ufafanuzi juu ya matumizi halisi ya gharama ya Chopa hadi kufikia Milioni 200 kwa siku 14 tu.
Kufuatia kuhojiwa huko na kutakiwa kutoa maelezo kwenye Kamati ya Fedha kwenda Kamati Kuu Freeman Mbowe ameamua kutumiq vibaraka wake akiwemo Salum Mwalimu na John Mrema kuutangazia umma kuwa wanashughulikia vibali vya chopa wakati si kweli, wanasubiri kikao cha kamati kuu ili wawasilishe ufafanuzi wa gharama za matumizi ya chopa.