Yaliyoahidiwa, yanatimia watanzania hatujutii kumchagua Dk. Magufuli, Asante Muumba

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
RAIS John Magufuli, ametimiza zaidi ya siku 100 sasa tangu aapishwe kuongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano.

Kasi ya utendaji wake inaakisi ahadi alizotoa wakati wa kampeni akiomba wananchi wamchague. Falsafa ya ukweli na uwazi aliyokuwa akiisimamia kwenye mikutano ya kampeni, sasa ameanza kuitendea haki. “Nikisema jiwe ni jiwe tu… Msema kweli ni mpenzi wa Mungu”, hizi zilikuwa miongoni mwa kauli alizokuwa akitoa kwa wananchi kuwathibitishia atakavyosimamia ahadi zake. Alisisitiza kwamba, hawezi kuahidi mambo yasiyowezekana juu ya namna ya kutatua kero za wanachi kwa ajili ya kupata kura.

Ubadhirifu na uzembe wa watumishi wa umma , ni miongoni mwa mambo aliyoapa kuyavalia njuga atakapokuwa Rais. Alisema kipindi cha kampeni: “Baadhi ya watu wamekuwa wakisema Magufuli ni mkali. Mimi siyo mkali, ni mpole. Lakini nachukia wafanyakazi wazembe, wanaonyanyasa wanyonge.” Hakutaka kuficha ukweli wake wa moyoni alipokuwa akisema wakati wa kampeni: “Nachukia mafisadi… Na nitawafunga na ‘magufuli’ (kufuli) yangu….”

Aliweka wazi kwamba, mafisadi na wazembe hawampendi na hawatamchagua; lakini akasema anaamini watu wazuri, ambao ndiyo wengi, watamchagua na yeye akaweka ahadi kwamba hatowaangusha. Alipania kukabili mafisadi, wazembe, wavivu na wakwepa kodi kuhakikisha mapato ya serikali yanaongezeka na umma wa Watanzania unafaidi. Hata baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha urais, Magufuli aliendelea na msimamo wake akiahidi ‘kutumbua majipu’ kwa maana ya kukabili wizi, ufisadi, uzembe na ubadhirifu wa mali za umma; jambo ambalo sasa limetimia.

Majipu yaliyotumbuliwa tangu aapishwe mpaka sasa anapotimiza siku 100 ofisini ni mengi na Watanzania ni mashahidi. Watendaji, wakiwemo vigogo wa taasisi mbalimbali za serikali, wameonja na wanaendelea kuonja ‘joto ya jiwe’ ya utendaji wa Rais Magufuli dhidi ya mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma. Mamlaka ya Bandari (TPA) ni miongoni mwa taasisi ambazo baadhi ya vigogo, wamesimamishwa kazi kwa tuhuma za kulea uozo bandarini unaoikosesha mapato muhimu kwa maendeleo yetu.

Pia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imekabiliwa na utumbuaji majipu uliokwenda sanjari na kutengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wake, Dickson Maimu. Watumishi kadhaa nao wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi. Taasisi nyingine ambayo Rais Magufuli amezimulika, ni Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli nchini (RAHCO), ambayo Mkurugenzi Mkuu wake, Benhadard Tito amesimamishwa kupisha uchunguzi.

Kinachochunguzwa ni ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati. Wakati majipu mengine akiyatumbua mwenyewe moja kwa moja, mengine yanatumbuliwa na wateule wake katika ngazi mbalimbali ikiwa ni utekelezaji wa kaulimbiu yake ya Hapa Kazi Tu. Kwa ujumla, uadilifu na uchapakazi kwa watumishi wa umma, ni jambo ambalo Magufuli alikuwa akisisitiza kuliimarisha na ndiyo kazi anayoifanya ya kutumbua majipu.

Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue anasisitiza kwamba, Rais pamoja na wao wanaomsaidia , hawaoni raha kuchukua hatua (za kutumbua majipu) dhidi ya viongozi na watumishi wengine isipokuwa wanalazimika. Balozi Sefue amekaririwa katika taarifa zake kwa umma akisema, “Tungependa kila mtu mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha Rais mahali ambapo inabidi amchukulie hatua.”

Anasisitiza kila kiongozi na mamlaka ya nidhamu, asipate kigugumizi kuchukua hatua za nidhamu, lakini kwa kuzingatia kwa ukamilifu sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma. Anahimiza uongozi na watumishi wa umma kuhudumia wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima. Mbali na kutumbua majipu, ahadi nyingine ambazo utekelezaji wake umeanza na kuonekana, ni pamoja na utoaji elimu bure kuanzia awali hadi shule za sekondari.

Ingawa Serikali inakiri utekelezaji huo kukumbwa na changamoto, inasisitiza kwamba inaendelea kuzikusanya kwa ajili ya kuzifanyia kazi ili mpango uwe na tija. Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, George Simbachawene sanjari na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, wanasema wanajitahidi kuhakikisha changamoto husika zinakabiliwa.

Kwa upande wa ahadi ya ‘Tanzania yenye viwanda’, utekelezaji wa mkakati huo unaanza kuonekana kutokana na wizara yenye dhamana ya viwanda, kuanza kushikia bango suala hilo. Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amekaririwa hivi karibuni akiagiza kwamba, ifikapo Julai mwaka, viwanda vyote vilivyobinafsishwa vinatakiwa viwe vimeanza kufanya kazi, vinginevyo hatua za kisheria. Pia ameagiza mikoa kuanza kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda na kukaribisha wawekezaji.

Kuhusu ahadi ya Magufuli kuhakikisha sheria za nchi zinasimamiwa, utekelezaji wake umeanza kujionesha hususani kwenye suala zima la bomoabomoa. Akiwa kwenye kampeni, alikaririwa akisema, “Kura nazitaka lakini lazima niseme ukweli; ukweli unaouma… Ukiifuata barabara hutalipwa, lakini barabara ikikufuata, unapaswa ulipwe.”

Alikuwa akijibu hoja za wananchi mbalimbali waliotaka kusikia kauli yake juu ya wanaowekewa alama za X kutokana na nyumba zao kujengwa sehemu zisizotakiwa ikiwemo kwenye maeneo ya barabara. Magufuli alisisitiza, serikali haiwezi kutumia fedha kulipa fidia kwa watu waliokiuka sheria.

“Msema kweli ni mpenzi wa Mungu; nazungumza ukweli na ukweli utabaki kuwa ukweli.” Bomoabomoa iliyofanyika hivi karibuni, hususan Dar es Salaam ni matokeo ya msimamo wa rais wa kuzingatia sheria na taratibu. Kuhusu ahadi ya kuleta nafuu kwa wakulima ikiwa ni pamoja na kuondoa ushuru na tozo za mazao, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba anasema hayo yameanza kufanyiwa kazi.

Mwigulu anasisitiza, miaka mitano ya uongozi wa Rais Magufuli, itakuwa kipindi cha kuweka mabadiliko makubwa katika sekta nzima ya kilimo na kuipa hadhi. Ahadi nyingine ambayo utekelezaji wake umeiva, ni kuhusu uanzishwaji wa Mahakama ya Mafisadi. Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe anasema mchakato wake umefika hatua nzuri. “Nataka niwaambie Watanzania kuwa iko mbioni na mchakato wake umefikia hatua nzuri hivyo utakapokamilika tutawafahamisha,” anasema Mwakyembe.

Kwa ujumla, watu wa kada mbalimbali wanaelezea kuguswa na ukweli, uadilifu na uchapakazi wa Rais Magufuli kama alivyoahidi wakati wa kampeni. Mbunge wa Mufindi Kusini, Medard Kigola anaeleza furaha yake kuona namna ambavyo Rais amemudu kutekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu.

Anatoa mfano wa mpango wa elimu bure kwa shule za awali hadi sekondari akisema, “Hakuna mtu ambaye hasikii wala haoni kazi inayofanyika.” “ Kufanya utekelezaji ndani ya miezi mitatu… Kuna watu wengine wanasema anatekeleza kidogo kidogo… Tusimkatishe Rais tamaa, ameanza kufanya kazi na anaonekana kwa Watanzania,” anasema Kigola akichangia mjadala bungeni.

Suleiman Murad ni Mbunge wa Mvomero ambaye anasisitiza Watanzania kumwombea Rais atimize malengo yake. Anapongeza juhudi za Rais kupambana na mafisadi, kuimarisha uchumi na kukusanya mapato. Mbunge mwingine anayeguswa na utendaji wa Rais, ni Sixtus Mapunda wa Mbinga anayekiri kwamba mambo mengi ambayo Rais aliahidi, utekelezaji wake umeshaonekana. “Naomba Watanzania tuendelee kumwombea ili azma ya kuleta maendeleo ifanikiwe,” anasema Mapunda.

Kwa ujumla, umma wa Watanzania unahimizwa kutokatishwa tamaa na watu wanaobeza, kuponda na kukosoa utendaji wake. “Wanaomsema Rais kwamba yeye na wateule wake wanakwenda vibaya, itakuwa ndiyo hao ambao Rais alisema mapema kwamba anaamini mafisadi na watendaji wazembe hawatampenda,” ni kauli ya mkazi wa Geita, Zephania Mkiwa. Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe anapigilia msumari akisema, Magufuli ndiye Rais ambaye Watanzania walimhitaji alete mageuzi nchini.

Bashe anasisitiza, taifa liko kwenye dharura likihitaji uongozi wa aina hii. “Wakati mwingi tulikuwa tukiomba kiongozi transformational (mwanamageuzi)… Kiongozi asiyekuwa na mjadala katika jambo analoliamini lina manufaa,” anasema. Hata hivyo Bashe anashauri sheria zinazokinzana na kasi ya Magufuli ya ‘Hapa Kazi Tu’, zifikishwe bungeni zifanyiwe marekebisho na nyingi zifutwe. Pia Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe ingawa anakubali kazi ya kutumbua majipu, anakosoa kwamba inakiuka kanuni na taratibu .

Anasema ni vyema kama zipo sheria zisizoenda sawia katika kufanikisha hilo, zifikishwe bungeni wazifanyiwe marekebisho. Hata hivyo , Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, January Makamba anakwenda mbali zaidi akisema, safari ya kutengeneza Tanzania mpya haiwezi kuwa nyepesi .

Anasema ni lazima Rais Magufuli pamoja na mawaziri wake, wajaribiwe, watiwe mashaka na kukatishwa tamaa kuhusu mwelekeo wao. “Ni kama kutengeneza keki ya mayai lazima upasue mayai,” anasema Makamba na kuhimiza umma wa Watanzania kutopata mashaka wala wasiwasi kwamba nchi inaelekea katika mwelekeo usio. Kama anavyoona Bashe, pia Januari anakiri kwamba, nchi ilifika mahali ikahitaji Rais wa namna hii ambaye amepatikana na anahitaji kuungwa mkono
 
Bashe, January pamoja nawewe mleta mada Na wanaccm wote wanafiki tu, mmezoea kuishi kwa udanganyifu Na uongo
 
Ndugu uongo gani wakati ndio hali halisi, watanzania wamekubali utendaji wa magufuli kasoro mafisadi na watendaji wazembe waliokuwa wamezoea kuingia ofisini saa nne na kutoka saa sita
 
mkuu iongelee nafc yako usitujumuishe wote kwan c watanzania wote tunaomuaprove,wengine tumevunjiwa nyumba zetu mkwajuni japokua hio haikua ahadi ya ccm
 
Kwa upande wangu simkubali maana hakuna kilichobadilika kwenye maisha yangu ya kila siku zaidi ya bei za vitu muhimu zikiendelea kupanda. Alafu kuhusu mafisadi hakuna hata mmoja alitemtumbua zaidi ya kuwapa wizara tena. Mm binafsi huwa siyumbishwi na sinema maana najijua namimi pia ni mtu
 
mkuu iongelee nafc yako usitujumuishe wote kwan c watanzania wote tunaomuaprove,wengine tumevunjiwa nyumba zetu mkwajuni japokua hio haikua ahadi ya ccm

sheria inakutaka ukae mita 6o kutoka bondeni au kwenye vyanzo maji, sasa wewe ulikuwa hujui kuwa hapo mkwajuni ni mkondo wa bahari unaopeleka maji baharini au jeuri tu. hatma hivyo wamekuvunjia ili kunusuru maisha yako na familia yako
 
sheria hiohio iliagiza tupewe viwanja tuahamie huko lakini haikutekelezeka,by the way una uhakika kama nyumba zote zilizobomolewa zilikua ziko ndani ya mita 60,au tu umeckiliza TBC walivyosema mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom