Baba_Enock
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 7,080
- 2,424
Kwa wale waliokuwepo enzi hizo hiki kitu kilivutia sana!
=================================================
Yalaiti napenda pasi kifani
tafauti sikutilii moyoni
sikuachi leo na kesho peponi
Ha ha ha I LOVE YOU
Ni la dhati kwa hakika pendo langu
sikufiti kwani ndicho kilimwengu
sikuwati mpaka mbele za mungu
Toa shaka na wasiwasi moyoni
kukwepuka hilo haliwezekani
takushika leo na kesho peponi
Lanishinda kuwa nawe mbali mbali
wangu nyonda amini naukubali
nakupenda wala sioni badali
Japo watu mno watatulaumu
sio kitu wala singiwe na hamu
pendo letu tulidumishe lidumu
Duniani naomba kwa mwenyeezi
maisha yadumu yetu mapenzi
na peponi tuwe sote laazizi
=================================================
Enjoy your Weekend
=================================================
Yalaiti napenda pasi kifani
tafauti sikutilii moyoni
sikuachi leo na kesho peponi
Ha ha ha I LOVE YOU
Ni la dhati kwa hakika pendo langu
sikufiti kwani ndicho kilimwengu
sikuwati mpaka mbele za mungu
Toa shaka na wasiwasi moyoni
kukwepuka hilo haliwezekani
takushika leo na kesho peponi
Lanishinda kuwa nawe mbali mbali
wangu nyonda amini naukubali
nakupenda wala sioni badali
Japo watu mno watatulaumu
sio kitu wala singiwe na hamu
pendo letu tulidumishe lidumu
Duniani naomba kwa mwenyeezi
maisha yadumu yetu mapenzi
na peponi tuwe sote laazizi
=================================================
Enjoy your Weekend