Yako wapi majibu ya haya??

Yako wapi majibu ya haya??

OSOKONI

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2011
Posts
10,965
Reaction score
5,344
Heshima kwa wanajukwaa wote!
Nimeona tuunganishe vichwa vyetu ili kujiuliza yako wapi majibu sahihi ya kashfa mbalimbali zinazolitafuna Taifa letu?
Kashfa hizi zimekuwa zikiripotiwa kwenye vichwa vya habari kurasa za mbele za magazeti na hata kutoka kwenye media kama radio na Runinga, Kikubwa zaidi zimekuwa zikiletwa hapa jukwaani pamoja na picha na ushahidi mbalimbali.
Kilichonigusa kuandika haya ni kwa kuwa muda mfupi baada ya kuripotiwa na kujadiliwa kwa jazba huisha bila hitimisho huku tukisubiri kashfa nyingine!

Mtindo huu wa kutofuatilia kashfa hadi mwisho wake na kudai hitimisho( mfano watu kufikishwa mahakamani, kufungwa, kufukuzwa kazi, kujiuzulu, kufilisiwa kuondolewa kwenye nyadhifa zao) Kumewafanya watawala kutoogopa au kuona haya kujiingiza kwenye kashfa mpya( wanajua itapigiwa kelele then itakwisha bila watu kudai hitimisho)

Kibaya zaidi hata wanasiasa9(hasa wa upinzani) Waandishi wa habari, wana Jf na wananchi wote kwa ujumla ambao tunajadili kwa jazba na munkari sana pale kashfa hizi zinapotolewa huwa baada ya muda tunakaa kimya tukisubiri jingine bila kuuliza na kudai Hitimisho la kashfa zilizotangulia.

Watuhumiwa wanaonekana mitaani wakitamba na kutoa kauli za kejeli huku wengine wakipewa nyadhifa nyeti zaid, sio tusi kwetu sote? Hebu tujiulize yako wapi majibu na hitimisho la kashfa hizi?? (nimebandika chache tu)
1.Richmond, Dowans et al?
2.Ununuzi wa Radar na ndege ya Rais?
3.EPA (Waliorudisha na ambao hawakurudisha, kagoda??)
4.Usafirishaji wa wanyama hai (kupitia KIA na ndege ya jeshi ya Qatar?)
5.Walioficha mapesa Uswiss??
6.Meremeta?
7.Mauaji ya raia(Arusha, Songea,Morogoro na marehemu mwangosi)
8.Mauaji yenye sura ya kisiasa( usariver Arusha, Igunga na kwingineko??)
9.Utekaji na utesaji wa Dr.Ulimboka?
10 Utengenezaji na Usambazaji wa madawa fake ya ARV?
11.Uingizaji na Usambazaji wa mbolea feki?

Hayo ni machache sana ambayo tuliyajadili hapa kwa jazba na munkari lakini yako wapi majibu yake?
Tuendelee kusubiri kashfa mpya bila majibu ya haya??Naomba michango yenu huku tukijikita zaidi kwenye mbinu ya kupata hitimisho ya kashfa hizi!!
 
Mkuu jibu ni moja tu!Lazima CCM iwekwe kando kwanza ndipo huu uozo unaweza kushughulikiwa.kwasababu haya madudu yote ni kazi ya mikono yao hivyo hawawezi kusalitiana.Ni ndoto Serikali hii kumtia adabu Kinana kwa ujangili au Madabida kwa ARV feki.Ndege wanaofanana wanaruka pamoja jombaa!
 
Majibu ya haya hayawezi kuapatikana mpaka ccm ikae kando"
 
Umenena mkuu. Mi nakuongezea kama ifuatavyo.
* PWAGU HUPATA PWAGUZI
* BIRDS OF THE SAME FEATHERS FLOCK TOGETHER
* KESI YA NYANI HAHUKUMU NGEDERE
* ZIMW LIKUJUALO HALIKUL LIKAKWISHA * UKILA NYAMA YA MTU VIGUMU KUACHA

Hata hivyo tuna imani yatakwisha kwani hakuna marefu yasiyokuwa na ncha.
 
majibu yatatoka January 2016 after 31 October 2015 general election
 
Mkuu haya ndo huwa nayasema mara kwa mara, je, ccm wanataka kutuambia wamemaliza kuyashughulika haya? au wanakurupuka kusema uongo, Kashfa, Uzushi na majungu?
 
Back
Top Bottom