Yajue madhara ya kutumia sanitizers

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,328
12,625
Kwa vyovyote vile faida za kutumia sanitizers kunawa mikono kujikinga na COVID-19 ni nyingi kuliko hasara za kuacha kutumia. Hata ni vema pia mtumiaji akafahamu madhara ya sanitizers.

Kwanza sanitizers nyingi na nzuri huwa zinatengenezwa kwa kutumia pombe kali (60% alcohol) ili iweze kuviua vimelea vinavyokusudiwa. Kiwango hiki Cha alcohol kwenye sanitizers kinafanya yafuatayo pia:

1. Unapoinawa sanitizer huwa inauwa vimelea kusudiwa na visivyokusudiwa kwenye ngozi, zinaua vimelea vibaya na vimelea vizuri (normal flora) kwenye ngozi. Hii itasababisha ngozi ipoteze uimara wake wa kujikinga na magonjwa ya ngozi kama fungus, majipu na michubuko.

2. Sanitizer inaweza kupenya ngozi na kuingia kwenye damu na sehemu nyingine ndani ya mwili kwa kupitia kwenye ngozi na kuweza kusababisha madhara ya kunywa pombe, ukitumia saana unaweza kulewa pia sawa na aliyekunywa pombe. Hivyo tumia kidogo tu kisha weka mikono hewani ikauke na upepo (evaporate)

3. Wako watu ambao wana allergy na ethanol/spirit inayotumika kutengenezea sanitizers, hivyo wanapata allergic reaction.

4. Sanitizer itaondoa mafuta ya ngozi na kuiacha ngozi ikiwa kavu sana kiasi Cha kusababisha kuondoa afya ya ngozi kujilinda na maambukizi

Nini cha kufanya ni
1. Kuendelea kutumia sanitizers maana Corona ni hatari zaidi kuliko haya madhara ya sanitizers

2. Tumia maji kunawa mikono yako zaidi kuliko sanitizers. Tumia sanitizers tu Kama maji hakuna

3. Pala mafuta ya vasseline mwenye mikono ili kurudishia kilainishi Cha ngozi iliyoondolewa na sanitizers na kunawa maji na sabuni kila wakati.

4. Kama una allergy na alcohol epuka kugusa sehemu nyingine ya mwili na mikono yenye sanitizer, na utumie sanitizers zisizo na pombe.
 
1. Fungus majipu ni mtu na kinga zake. Sijawahi pata hayo mavitu kwenye maisha yangu mpaka sasa namba inasoma 30+

4. Mbona kama sio kweli?!! Natumia sanitizer kabla hata corona hajaenda China na sioni huo ukavu mikononi.
 
1. Fungus majipu ni mtu na kinga zake. Sijawahi pata hayo mavitu kwenye maisha yangu mpaka sasa namba inasoma 30+

4. Mbona kama sio kweli?!! Natumia sanitizer kabla hata corona hajaenda China na sioni huo ukavu mikononi.
Una bahati, lakini sina uhakika Kama ulikuwa unatumia sanitizer kila mara kila siku Kama ilivyo wakati huu, vinginevyo labda Kama ulikuwa na Corona yako mwenyewe nyumbani.

Ubapokuwa umewaua au kuwapunguza normal flora kwa kiasi kikubwa kwenye ngozi ngozi itakosa umadhubuti wa kujilinda na vimelea vya maradhi (opportunistic infections)
 
Back
Top Bottom