Yajue Maajabu ya simu za itel!

Yajue Maajabu ya simu za itel!

Wanjiro

Member
Joined
Oct 27, 2016
Posts
55
Reaction score
110
Huenda jina la kmpuni inayozalisha simu za mkononi ambazo ni smartphone na simu za batani ambayo ni itel si geni masikioni mwa watu wengi. Binafsi itel nilianza kuisikia miaka minne iliyopita, lakini hata hiivyo sikuwa natumia.

Kitu kilichokuja kunishawishi kutumia itel ni kuna siku nilisafiri na rafiki yangu mi nilikuwa na simu nyingine na yeye alikuwa anatumia itel, ilikuwa ni porini, simu yangu iliisha chaji siku hiyohiyo njiani ,lakini yeye ilikaa mpaka siku 7 tukiwa huko porini na hakukuwa na sehemu ya kuchaji. Ile simu ilikuwa ni ya batani itel 5622. Niliporudi mjini niliamua kununua hii simu. itel 5622. Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kupenda simu za kampuni ya itel.

a.png

Tangu hapo nimekuwa nikitumia simu za itel na kwa sasa kuna smartphone itel P51 hii kiukweli kwa chaji ni hatari siku tatu inadumu na chaji yaani 'One Charge Three Days'. Pia ina uwezo wa kuchaji simu nyingine. Kiukweli binafsi imeona itel ni mkombozi mkubwa kwa upande wa chaji.

a.png

Jambo ambalo ni nawapongeza sana itel mobile ni bei zao, simu zao kiukweli zimezingatia viwango lakini bei ni poa sana. Mfano hii simu smartphone inayodumu na chaji chati unavyotaka masaa 72 lazima. Bei ni 190,000 tu. Memory ni ROM GB16 + RAM GB1 na kamera yake ni MP8 nyuma. Ni hayo tu nimeona niwashirikishe haya maajabu.
 
Mimi nilijua utamponda huyu itel kumbe unatangaza hahaha.
 
Back
Top Bottom