Yahya Jammeh: Rais mganga wa mitishamba anayeua mashoga, walawiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yahya Jammeh: Rais mganga wa mitishamba anayeua mashoga, walawiti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jan 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Rais Yahya Abdul-Aziz Jemus Junkung Jammeh

  GAMBIA ni nchi ndogo kuliko zote barani Afrika katika pwani ya magharibi iliyozungukwa na nchi ya Senegal sehemu zote ukiachia sehemu ndogo ya bahari. Kwa maana nyingine Gambia inapakana na nchi moja tu-Senegal.

  Gambia imekatizwa katikati ya ardhi yake na mto Gambia karibu kwa urefu wake wote kwa takriban kilometa 20 kila upande wa mto.

  Aidha Gambia ni nchi ya kwanza kabisa barani Afrika kutembelewa na Rais wa Marekani aliyekuwa madarakani. Wakati Vita vya Pili vya Dunia vinapamba moto, aliyekuwa Rais wa Marekani, Franklin Roosevelt alitua Banjul, mji mkuu wa nchi hiyo akielekea Casablanca, nchini Morocco, kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi kuhusu masuala ya vita hiyo.

  Hata hivyo, jiografia isiyo ya kawaida ya nchi hii na ujio pia usio wa kawaida wa Rais wa Marekani, pengine vinaendana na vituko vya kiongozi wa nchi hiyo – Rais Yahya Abdul-Aziz Jemus Junkung Jammeh, kwa kifupi Yahya Jammeh aliyeshika uongozi wa nchi mwaka 1994 baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomuangusha rais Dawda Jawara.

  Na kama ilivyo kwa viongozi wa nchi nyingi tu barani humu, Jammeh pia amekuwa akituhumiwa kwa kuendesha serikali kwa kukiuka misingi ya utawala bora, kuwepo kwa ufisadi na kadhalika.

  Amekuwa akituhumiwa kwa kufinya uhuru wa vyombo vya habari kwa kuweka sheria kali kwa vyombo hivyo.

  Mnamo Aprili, 2004 aliwataka waandishi wote wa habari nchini, wa ndani na wale wanawakilisha vyombo vya nje waiheshimu serikali yake au sivyo “waende kuzimu.”

  Alisema alikuwa amechoka nao kwani ameruhusu uhuru mkubwa kwao na sasa wanamtukana.

  Kutokana na hili, mnamo Desemba 2004 mwandishi mmoja ha habari, Deyda Hydara aliuawa kwa mazingira ya kutatanisha baada ya kuwa akiandika habari na makala kali dhidi ya Jammeh na utawala wake.

  Hadi sasa wahusika wa kifo hicho hawajajulikana lakini vidole vinanamnyooshea Rais Jammeh.

  Aidha wanandoa wawili, raia wa Uingereza walihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kwa kuandika barua pepe nyingi kwa ndugu na jamaa zao huko Uingereza zilizomtuhumu Jammeh.

  Aliwahi pia kutoa amri kwamba ni yeye pekee tu ndiyo ana mamlaka ya kupita chini ya lango (arch) kuu lililojengwa kwenye barabara moja katikati ya mji mkuu wa Banjul kusherehekea miaka kumi ya utawala wake mnamo mwaka 2004.

  Kuna wakazi kadhaa wa mji huo walipita chini ya lango hilo na walikamatwa na kuwekwa ndani. Walitolewa siku kadhaa baada ya sherehe hizo.

  Lakini haya yote ni tisa, kumi ni pale Jammeh alipotangaza, mapema mwaka jana, kwamba serikali yake itaweka sheria kali dhidi ya mashoga na walawiti, sheria ambazo “zitakuwa kali kuliko hata zile za Iran” na kwamba bila kusita atakata vichwa vya shoga yoyote au mlawiti yoyote atakayepatikana nchini mwake.

  Katika hotuba hiyo, Jammeh alitoa ilani ya mwisho kwa watu wote wenye kuendekeza vitendo hivi waondoke nchini ama sivyo atawachinja.

  Aidha, aliwaonya wamiliki wa vyumba vya kulala wageni na mahoteli kwamba nao pia “watajikuta katika hatari kubwa endapo hawataacha kuwapatia huduma watu hao.”

  Habari mara zilienea nchi nzima kwa kupitia vyombo vya habari kwamba serikali imedhamiria kuwaua walawiti wote nchini.

  Katika ripoti yake iliyotoka Mei mwaka huu, Shirika linalotetea haki za binadamu (Amnesty International) limemshutumu Jammeh kwa kushabikia na kuendeleza mambo yasiyostahili kwa kiongozi wa nchi, kama vile uchawi na uganga wa kienyeji.

  Shirika hilo limesema kuwa hutumia visingizio vya uchawi kwa kuwaua kisirisiri au kupata sababu ya kuwatia ndani wapinzani wake wa kisiasa.

  Aliwahi pia kuwatuhumu wakazi wa mji mmoja uitwao Jambur kwamba ni wachawi na walikuwa wanapanga kumroga na kumuua.

  Chini ya ulinzi mkakli, aliwahutubia wakazi hao kwamba njama zao zinajulikana, lakini kwa masuala ya uchawi yeye ndiyo mchawi zaidi, kwa hivyo aliwaomba mara moja waache njama zao.

  Lakini hakuna kitu kilichowashangaza wengi nchini humo, na duniani kote kwa jumla ni pale, mwaka 2007, alipotangaza kuwa ana uwezo wa kutibu ugonjwa wa UKIMWI, kifua cha pumu na shinikizo la damu kwa kutumia miti shamba.

  Inadaiwa kuwa baadhi ya waaathirtika wa ugonjwa wa UKIMWI walipata ahueni kutokana na tiba yake, ingawa alishutumiwa kwa ku-promote tiba isiyo ya kisayansi ambayo ingeweza kuleta madhara mabaya.

  Hata hivyo, wachunguzi wa mambo na wataalamu wa tiba ya magonjwa mbali mbali waligundua katika hotuba yake, kwamba huenda Jammeh alikuwa akizungumzia magonjwa ya tumbo na minyoo, kwani alisema: “Na kuhusu UKIMWI, wagonjwa wanatakiwa wawekwe sehemu yenye huduma ya vyoo kwani wangeweza kutaka kwenda haja kila baada ya dakika tano.”

  Mwakilishi wa UNDP nchini humo, Fadzai Gwaradzimba, aliamriwa na serikali kuondoka nchini mara moja, baada ya kutangaza hadharani kwamba alikuwa na shaka kuhusu ukweli wa madai ya Rais Jammeh kuhusu tiba hiyo ya UKIMWI.

  Agosti mwaka 2007, Jammeh alitangaza kuwa alikuwa amegundua dozi moja ya mitishamba inayotibu shinikizo la damu, tangazo ambalo mara moja lilipingwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo lilitoa tamko la kumpuuza Rais huyo “mganga.”


  Chanzo: MwanaHalisi
   
 2. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  sijaielewa report hii.....
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,355
  Likes Received: 22,216
  Trophy Points: 280
  Dah...
  Maprezidaa wa afrika ni kiboko.
   
 4. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  dawa ni kumkubali Yesu awe mwokozi wa maisha yao......nothing else...
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Huyu kiboko aisee duu....bado anachaguliwa kila uchaguzi?au ndio wanamuogopa ukipingaana nae utakufa ghafla???Tz yaja...
   
 6. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Nilishawahi kuongoe na Marafiki zangu wanatoka Gambia wakasema kuwa huyu Bwana Alimlipa Mganga mkuu wa kienyeji kutoka nchi ya Guinea ambae alikwenda hapo kijijini Jambur, na kuanza kuwa point waganga wote wa kienyeji pale kijijini wakauliwa watu wote pale kijijini walilazimishwa kumeza dawa za miti shamba atakae kataa atauliwa,kwa wale wenye maadili makali ya kidini(waislam maana hii nchi ni ya kiislam) waliokataa walichinjwa kwa kutuhuma kuwa ndio wale wachawi waliotaka kumuua Rais kwa uchawi.Inasikitisha kuona Rais wa nchi ana tumia uchawi hadharani na hakuna anaempinga. Kwani inasemekana huvaa mihirizi mingi na hakuna anaeruhusiwa kucheka kwa kumuona Rais kavaa mahirizi.
   
 7. B

  Bull JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wangapi wamemkubali na wako kama yeye au zaidi? peleka blabla zako kanisani watakuamini
   
 8. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ushinde na ulegee dawa yako ni kukupekeka kwa Kakobe ukaombewe ndio uone umuhimu wa maombi.
   
Loading...