Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,887
- 2,771
Kaka hata mie hilo nalihitaji kinoma maana na story to tell through the movie..kuna vitabu vingi kaka but cash matters and really they help somehow cuz zina a lot of examples..http://www.10dayscreenplay.com/ cheki hapo I think kinaweza saidia if cash iko mikononi mwako...kama yupo mwenye ujuzi huu wanaJF tusaidiane..
Hope so pia maana nahitaji kweli mkuu...nitaifanyia kazi hiyo. hope wataleta ujuzi wao hapa
Nashukuru kwa kuonyesha kujali mkuu. Kwa sasa niko mbali sana kwenye haya masuala, kwa maana kwamba nimeshaanza kubobea. Si script tu bali kwenye film industry in general. Tuko pamoja sana.Mkuu Raia Fulani,
Thread yako ni ya kitambo sana...tupe mrejesho! Je, ushafahamu kuandika script? IKiwa bado, si mbaya ukiendelea na lengo lako. Kwanza kabisa, ikiwa wewe ni mwandishi mzuri wa stori basi hautapata taabu hata kidogo kuandika script ingawaje kuna tofauti kubwa kati ya uandishi wa story/riwaya na script! Kwanza kabisa, kuna format maalumu ya uandishi wa script...kibongo bongo sifahamu wanaandikaje lakini kama unataka kutumia Industrial/Hollywood Format, basi ni lazima utumie software...screenwriting softwares otherwise ni full headache to almost impossible! So, if u dream to use industrial format basi tafuta softwares kv Final Draft, Movie Magic au unaweza hata kutumia Celtx ambayo ni free software!
Ukishakuwa na software, kingine cha kuzingatia ni kwamba script is all about visualizing ur story...hii ndiyo tofauti ya msingi kati ya stori ya kawaida na script! Kwa mfano, kwenye story unaweza kuandika "kufumba na kufumbua nikajikuta nimetumia zaidi ya robo saa nikiwa sijafanya chochote na ndipo nilipokumbuka kwamba sikuwa na muda zaidi wa kupteza..." Kwenye script, sentensi kama hiyo haitakiwi!!!
Jambo lingine la kuzingatia kwenye script ni suala la Arcs Development....techincally, kuna three arcs, call them whatever; whether ABC! First Arc, unafanya story set up! First arc isivuke page 25...na kama umeenda sana basi usivuke page 30. Second Arc unazungumzia vikwazo anavyokumbana navyo protagonist wako katika ku-achieve kile anachokusudia! Third Arc ni ile ambayo inawakilisha regrets. Na kama script yenyewe ni future film, basi inabidi iwe between 90-120 pages! Unapotumia screenwriting software, 1 page inawakilisha 1 minute shoot!
Hongera sana na ndio maana sikutaka kuandika mengi coz' nilishafahamu kwamba hii thread ni ya zamani sana so nilitarajia kuwapo kwa mabadiliko!Nashukuru kwa kuonyesha kujali mkuu. Kwa sasa niko mbali sana kwenye haya masuala, kwa maana kwamba nimeshaanza kubobea. Si script tu bali kwenye film industry in general. Tuko pamoja sana.
Wapendwa, husikeni na kichwa cha habari. Baada ya kuona uandishi wa riwaya hauna tija, wazo limenijia kuwa mtunzi wa filamu. Sijajua script inaandikwaje. Nauhitaji huu utaalam niweze kuleta mapinduzi fulani kwenye tasnia ya sinema, bongo. Naombeni mawazo yenu
Mkuu hongera sana kwa kuumiza kichwa!
Nikutoe wasi wasi, kuhusu muundo wa script na inavoandikwa, mpaka hapo ulipofikia umeshamaliza kazi kwa zaidi ya 50%, kilichobaki ni rahisi sana! Tulipokuwa o - level ktk Fasihi tulisoma aina 3 za kazi za Fasihi andishi, wengi hapa ni mashahidi! Tofauti ni aina gani ya vitabu. Mf mimi nilisoma:
RIWAYA: Shida - Ndanao Balisidya, Kuli - Shafi A. Shafi & Kusadikika - Shaaban Robert
TAMTHILIYA: Ngoswe: Penzi kitovu cha uzembe (Edwin Semzaba - sasa ni Prof), Hawala ya Fedha (simkumbuki mwandishi)
USHAIRI (kwa case yako hautuhusu) Sasa kwa tatizo lako, unapoichukua hadithi yoyote ile, mf kama hizo hapo juu na kuiweka ama kuiandika ktk mtindo wa majibizano ya WAHUSIKA (DIOLOGUE) kama ule uliokuwemo ktk vitabu vya NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE ama HAWALA YA FEDHA, hapo unapata SCRIPTS! ila naomba ujue, scripts inaenda mbali zaidi na itaainisha mavazi, jukwaa, umri, aina ya wahusika n.k
Nimejaribu!
Nashukuru kwa kuonyesha kujali mkuu. Kwa sasa niko mbali sana kwenye haya masuala, kwa maana kwamba nimeshaanza kubobea. Si script tu bali kwenye film industry in general. Tuko pamoja sana.
Au si vibaya vilevile akituambia changamoto za msingi kuhusu filamu zetu manake ukweli bado unabaki pale pale kwamba filamu zetu bado sana hata kama zinaangaliwa na wengi....leo hii ukiniwekea album ya Diamond na ya Nick Minaj wala sitafikiria mara mbili...nitanunua ya Diamond na kuiacha ya Minaji lakini nitakuwa ni mwendawazimu nisiye na mfano wake nikisema kwamba Diamond ni bora kuliko Nick Minaj! Kwahiyo si mbaya mkuu Raia Fulani akituambia anadhani ni mambo gani hasa anayodhani yanafanya filamu zetu bado zisiwe na ule msisimko wa kweli!Kweli mkuu kwa miaka mi3 utakuwa upo mbali kama vp unaweza uka-share na sisi majina ya filamu ulizozi-direct na scripts ulizoziandika.