Yahusu ujuzi wa kuandika mtiririko wa filam

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,773
2,544
Wapendwa, husikeni na kichwa cha habari. Baada ya kuona uandishi wa riwaya hauna tija, wazo limenijia kuwa mtunzi wa filamu. Sijajua script inaandikwaje. Nauhitaji huu utaalam niweze kuleta mapinduzi fulani kwenye tasnia ya sinema, bongo. Naombeni mawazo yenu
 
Why! Niko serious guys. Any one who knows about movie script, plz let me know. Au anielekeze wapi na kwa nani
 
dogo hiyo mbona simple tuu...andika story yako fresh..kisha ipange ile story kwa mtiririko wa igizo/mchezo wenye wahusika kulingana na story yenyewe...sasa hapo ndio utakuwa umeandika scripti...maana ya scripti ni muongozo wa mtu kuffuata wakati anafanya kitu au mchezo wa kuigiza....

ukiwa kama mwandishi wa scripts za movie unatakiwa pia uwe na utashi wa ziada wa kujua nini au nani anafaa kuigiza au kuuva ule uhusika wa mtu unayemlenga...then hata hao actors/actress wako watatakiwa kuendana na story yako....sio unasema binti mrembo mrefu na mwenye shingo ya upanga ...kisha unatuletea binti wa ajabuajabu tuu...au mtu anaigiza sehemu ya baba wa familia badala ya kutumia mtu mzima unatumia kijana wa 20yrs...pia kuna suala la location...

wapi matukio yanapochukuliwa...usiongelee jumba la kifahari kisha ukafanya shooting kwenye nyumba zetu za manzese kwa tumbo/mtogole.....\

kuhusu kujifunza...sio kila mtaalamu wa kila kitu duniani alipitia shule au darasani...movie scripts writers are creative persons by nature....no school under the sun teaches creativity....this is just a natural gift from the MAN high above

...NI MAONI YANGU TUU...FINITO
 
Dogo, naona hujatatua tatizo. Kusema tu rahisi. Ishu pia ni kuona muundo wa script. Suala la wahusika kuvaa uhusika hilo tuko pamoja
 
Kaka hata mie hilo nalihitaji kinoma maana na story to tell through the movie..kuna vitabu vingi kaka but cash matters and really they help somehow cuz zina a lot of examples..http://www.10dayscreenplay.com/ cheki hapo I think kinaweza saidia if cash iko mikononi mwako...kama yupo mwenye ujuzi huu wanaJF tusaidiane..
 
nitaifanyia kazi hiyo. hope wataleta ujuzi wao hapa
 
Hii thread ni ya kitambo ila wakuu mliotaka kujifunza namna ya kuandika Script kama bado hamjapata hiyo ilmu nipo tayari kusaidia, na itakua raisi sababu hatua ya mwanzo tayari mmeshaipitia kwa maana ya STORY! unahitaji Kisa tu kuandika Script sio lazima uwe na mtililiko wa hadithi, so let me know kama bado ni wahitaji.
 
Mkuu Raia Fulani,
Thread yako ni ya kitambo sana...tupe mrejesho! Je, ushafahamu kuandika script? IKiwa bado, si mbaya ukiendelea na lengo lako. Kwanza kabisa, ikiwa wewe ni mwandishi mzuri wa stori basi hautapata taabu hata kidogo kuandika script ingawaje kuna tofauti kubwa kati ya uandishi wa story/riwaya na script! Kwanza kabisa, kuna format maalumu ya uandishi wa script...kibongo bongo sifahamu wanaandikaje lakini kama unataka kutumia Industrial/Hollywood Format, basi ni lazima utumie software...screenwriting softwares otherwise ni full headache to almost impossible! So, if u dream to use industrial format basi tafuta softwares kv Final Draft, Movie Magic au unaweza hata kutumia Celtx ambayo ni free software!

Ukishakuwa na software, kingine cha kuzingatia ni kwamba script is all about visualizing ur story...hii ndiyo tofauti ya msingi kati ya stori ya kawaida na script! Kwa mfano, kwenye story unaweza kuandika "kufumba na kufumbua nikajikuta nimetumia zaidi ya robo saa nikiwa sijafanya chochote na ndipo nilipokumbuka kwamba sikuwa na muda zaidi wa kupteza..." Kwenye script, sentensi kama hiyo haitakiwi!!!

Jambo lingine la kuzingatia kwenye script ni suala la Arcs Development....techincally, kuna three arcs, call them whatever; whether ABC! First Arc, unafanya story set up! First arc isivuke page 25...na kama umeenda sana basi usivuke page 30. Second Arc unazungumzia vikwazo anavyokumbana navyo protagonist wako katika ku-achieve kile anachokusudia! Third Arc ni ile ambayo inawakilisha regrets. Na kama script yenyewe ni future film, basi inabidi iwe between 90-120 pages! Unapotumia screenwriting software, 1 page inawakilisha 1 minute shoot!
 
Last edited by a moderator:

Nashukuru kwa kuonyesha kujali mkuu. Kwa sasa niko mbali sana kwenye haya masuala, kwa maana kwamba nimeshaanza kubobea. Si script tu bali kwenye film industry in general. Tuko pamoja sana.
 
Hongera sana na ndio maana sikutaka kuandika mengi coz' nilishafahamu kwamba hii thread ni ya zamani sana so nilitarajia kuwapo kwa mabadiliko!
 
Wapendwa, husikeni na kichwa cha habari. Baada ya kuona uandishi wa riwaya hauna tija, wazo limenijia kuwa mtunzi wa filamu. Sijajua script inaandikwaje. Nauhitaji huu utaalam niweze kuleta mapinduzi fulani kwenye tasnia ya sinema, bongo. Naombeni mawazo yenu

Mkuu hongera sana kwa kuumiza kichwa!
Nikutoe wasi wasi, kuhusu muundo wa script na inavoandikwa, mpaka hapo ulipofikia umeshamaliza kazi kwa zaidi ya 50%, kilichobaki ni rahisi sana! Tulipokuwa o - level ktk Fasihi tulisoma aina 3 za kazi za Fasihi andishi, wengi hapa ni mashahidi! Tofauti ni aina gani ya vitabu. Mf mimi nilisoma:

RIWAYA: Shida - Ndanao Balisidya, Kuli - Shafi A. Shafi & Kusadikika - Shaaban Robert

TAMTHILIYA: Ngoswe: Penzi kitovu cha uzembe (Edwin Semzaba - sasa ni Prof), Hawala ya Fedha (simkumbuki mwandishi)

USHAIRI (kwa case yako hautuhusu) Sasa kwa tatizo lako, unapoichukua hadithi yoyote ile, mf kama hizo hapo juu na kuiweka ama kuiandika ktk mtindo wa majibizano ya WAHUSIKA (DIOLOGUE) kama ule uliokuwemo ktk vitabu vya NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE ama HAWALA YA FEDHA, hapo unapata SCRIPTS! ila naomba ujue, scripts inaenda mbali zaidi na itaainisha mavazi, jukwaa, umri, aina ya wahusika n.k

Nimejaribu!
 
imenisaidia hata mimi,nakushukuru sana
 
Nashukuru kwa kuonyesha kujali mkuu. Kwa sasa niko mbali sana kwenye haya masuala, kwa maana kwamba nimeshaanza kubobea. Si script tu bali kwenye film industry in general. Tuko pamoja sana.

Kweli mkuu kwa miaka mi3 utakuwa upo mbali kama vp unaweza uka-share na sisi majina ya filamu ulizozi-direct na scripts ulizoziandika.
 
Mada hii inaonesha wazi kwamba wapo watu wenye interest na suala zima la scriptwriting na filamu kwa ujumla. and am very certain watu wakishafanya vizuri kwenye script basi filamu zetu zitakuwa zimepiga hatua kubwa coz' script ndio base ya filamu! Script ikishakuwa tight na kupata tight director, basi unaweza hata kutumia amateur actors na bado filamu ikawa tight. Lakini ukishakuwa na script ya hovyo basi hata ukiwa na waigizaji wakubwa namna gani bado filamu itakuwa ya hovyo unless director afumue the whole script!

Tatizo la script kwa nchi kama yetu ni tatizo kubwa coz' kwa sehemu ambako hamna formal script writing training basi mwandishi ni lazima awe na talent and not otherwise...hapa ndipo linapoanzia tatizo. Unlike kumwelekeza mtu ku-act, it's quite headache kumwelekeza someone how to write especially kama mwelekezaji sio professional trainer asiyefahamu misingi ya story plotting.
 
Kweli mkuu kwa miaka mi3 utakuwa upo mbali kama vp unaweza uka-share na sisi majina ya filamu ulizozi-direct na scripts ulizoziandika.
Au si vibaya vilevile akituambia changamoto za msingi kuhusu filamu zetu manake ukweli bado unabaki pale pale kwamba filamu zetu bado sana hata kama zinaangaliwa na wengi....leo hii ukiniwekea album ya Diamond na ya Nick Minaj wala sitafikiria mara mbili...nitanunua ya Diamond na kuiacha ya Minaji lakini nitakuwa ni mwendawazimu nisiye na mfano wake nikisema kwamba Diamond ni bora kuliko Nick Minaj! Kwahiyo si mbaya mkuu Raia Fulani akituambia anadhani ni mambo gani hasa anayodhani yanafanya filamu zetu bado zisiwe na ule msisimko wa kweli!
 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine filamu zinaumiza kichwa hasa pale kazi inapokuwa imekamilika na unataka kurudisha gharama zako na pengine kupata faida. Usambazaji ndio tatizo kubwa. Kadhalika ubunifu katika uandishi wa script na story ni tatizo kwetu bongo. story nyingi hazina mashiko. halafu kila mtu anadhani anajua kutengeneza story nzuri. story zinategemea na umri pia. All in all panatakiwa pawepo na filamu chache nchini ambazo zitawashawishi watu makini kuwekeza kwenye hii tasnia. so far inaonekana ni tasnia ya walioshindwa kwingine (kama ilivyo ualimu)
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom