Yafuatayo Baada ya "KUNYIMWA" Mkopo.

Yafuatayo Baada ya "KUNYIMWA" Mkopo.

Kirchhoff

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
5,939
Reaction score
8,883
Hali yangu Kiuchumi

Nimetunukiwa Diploma 2010.
Nilikuwa kwenye Ajira hadi march 2015.

Nikapata wazo la kuongeza Elimu hivyo sikutaka kuajiriwa tena ili nisipate usumbufu wa kujiunga Chuo.

Nikalipa 50000 na 30000 kuomba chuo na mkopo respectively.

Umri unaruhusu bado miezi kadhaa nifikishe miaka 30.

Hali ya uchumi hainiruhusu kujisomesha, hivyo nikasoma vizuri HESLB guidebook na kupata Kozi ambayo nina vigezo vyote vya kupewa mkopo.
Sasa mkopo nimenyimwa naambiwa nikate rufaa. Rufaa yenyewe inanilazimu kusafiri hadi huko chuoni, kuiprint na kuiwasilisha kwa Afisa Mkopo wa chuo. Majibu ya Rufaa ni hadi January.
Naambiwa nieleze kwa nini nipewe mkopo wakati sijaambiwa kwa nini nimenyimwa mkopo huku vigezo ninavyo.
Chuo kishafunguliwa na hawataki mtu bila Ada na Bodi haijatoa tamko lolote kwa vyuo hivi.
Mwakani nitakuwa na miaka 30 na miezi kadhaa hivyo sitakuwa eligible kupata mkopo.

Nimeona Mwisho wa kuongeza Elimu ndo hapo. Ajira zenyewe Ngumu.. kujiajiri nako shida.

Kifuatacho..

Sitajiua, sitavuta bangi, sitajiunga na panya road wala vikundi vyovyote hatarishi.

Nimejaliwa mke na watoto wawili ambapo nilitegemea hadi namaliza. degree wangekuwa wanaanza shule hivyo wangesoma kwa raha kweli kweli.

Sasa nitaongeza idadi ya watoto hadi toa kauli ya ufyatuzi ashangae. Nitafyatua haswa na Mungu anisaidie.

Nitageuka Sperm Donor.

Mwanamke yeyote mwemye afya na kipato Bora ambaye hataki usumbufu wa mwanamme anitafute. Namnyuka Mimba na kumwombea ajifungue salama.

Sitakuwa mchoyo. Nilichopewa Bure nitakitoa Bure.

Nipende Kuwashauri Diploma wenzangu tulionyimwa mkopo Tusijisumbue kwenda Vyuoni wala Kukata rufaa kama hatuna uwezo wa kujisomesha.

Na Chuo si Ada tuu bali matumizi mengineyo pia ni gharama kubwa.

Yaani nadahiliwa Kozi ya kipaumbele unashindwa kunipa hata asilimia 60???

Basi wacha nikafyatue tuu maana sina namna.
IMG_20161030_091236.JPG
IMG_20161030_091236.JPG
Screenshot_2016-10-30-16-09-36.png


Halafu watu kibao tuu tena wa Kozi zisizo kipaumbele wamepewa mkopo..
 
Haya mambo hayahitaji hasira. Utakayeumia ni wewe ndugu yangu. Naelewa inaumiza sana na itaharibu maisha ya wengi. La kufanya hapa ni kutulia na kuangalia la kufanya... naamini hutakosa na Mungu atakusaidia.

Wanaamua na kunyanyasa watoto wa walala hoi, wao wanatunyonya na kuwasomesha watoto wao. Mungu aishivyo hatatuacha.
 
una kili maisha magumu, ila unapanga kumpa mimba yeyote atakae katiza mbele yako.

una tofauti gani na serikali hii yenye jukumu la kuhudumia wananchi wake ila inalikwepa. maana hata wewe huta wahudumia hao watoto kwa sababu huna uwezo, huna nia iyo unafurahi wateseke ma mama yao/zao tu.

acha akili kama za serikali yako, tuliza kichwa panga mambo yako.miaka mi 4 sio mingi tukomae alafu itafika zamu kumuonesha na sie video bwana mkubwa.
 
una kili maisha magumu, ila unapanga kumpa mimba yeyote atakae katiza mbele yako.

una tofauti gani na serikali hii yenye jukumu la kuhudumia wananchi wake ila inalikwepa. maana hata wewe huta wahudumia hao watoto kwa sababu huna uwezo, huna nia iyo unafurahi wateseke ma mama yao/zao tu.

acha akili kama za serikali yako, tuliza kichwa panga mambo yako.miaka mi 4 sio mingi tukomae alafu itafika zamu kumuonesha na sie video bwana mkubwa.
Mkuu hebu hiyo Avatar yako Ongezea Isaya kwa nyuma kisha kasome hiyo Aya.
 
una diploma ya mambo gani na umeomba degree ya mambo gan ....ebu tuanzie hapa kwanza....
 
Nashukuru namba inasomeka kwa uzuuri kabisa!!
 
  • Thanks
Reactions: V2d
Yaani inatia huruma saana....anyway ONE DAY YES....tunwaombea dua nzuri nzuri mufanikiwe.
 
una diploma ya mambo gani na umeomba degree ya mambo gan ....ebu tuanzie hapa kwanza....
Mkuu nimeomba Sayansi na Elimu ( Hisabati na ICT)
Nimebobea katika Ufundi wa Kielektroniki na Mawasiliano.

Ajira sikupenda pia kuacha bali Maslahi madogo yaani unafanyia kazi Ugali na Kodi tuu.
 
Back
Top Bottom