Yafaa sasa kubadili jina la Ziwa Victoria

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,425
7,211
Nchini Marekani na ulaya kumezuka wimbi kufuta majina ya wabaguzi na waliyokua vinara wa biashara ya utumwa kwenye kumbukumbuku za heshima kama minara au sanamu zao kuvunjwa au kung'olewa.

Baadhi ya mambo yanayotudhalilisha waafrika ni kushindwa kujikubali kutokana na makovu ya utumwa wa mwili na roho.

Miaka mingi baada ya kujitawala unakuta kuna majina ya wakoloni mashuhuri yalipewa sehemu mashuhuri za kijiografia ya nchi zetu bado tumeyaacha kutumika.

Binafsi ningependekeza nchi za Tanzania, Kenya na Uganda tufanye muafaka haraka kubadili jina la Ziwa Victoria na kuliita ziwa nyanza. Hilo ndio jina la asili la ziwa hilo.

Kule Nairobi nimefurahi baada ya kujua kumbe sanamu la malkia huyo wa enzi ya uingereza kusaka makoloni lililokua kwenye bustani moja wananchi walilibomolea mbali miaka mitatu iliyopita
 
Neno nyanza ni la kikabila lenye maana ya ziwa. So ukisema liitwe nyanza ni sawa kusema ziwa la ziwa hebu pendekeza jina jingine.
 
Tuibadili hiyo Victoria tuinyambue kwa kisukuma mpaka tupate jina..😜
 
Wale waheshimiwa walioko dodoma kusifia na kupiga majungu huu ndo ulikuwa muda mwafaka kwao kuchukua mapendekezo Kama haya maana wao wana Mamlaka

Ni upuuzi kuendelea kutuaminisha eti hadi ziwa liligunduliwa na mzungu, milima.
 
Back
Top Bottom