Ya wajumbe wateule wa kamati ya katiba toka Zanzibar na maoni ya wazanzibari

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,882
2,762
Dr Harith Ghassany

Katiba yetu ya Zanzibar ndio dira! Kama kuongeza
au kupunguza ni ndani ya Katiba ya Zanzibar.
Tukiishadidia Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni
sawa na kuutawadhisha ubatili wa Muungano.Ni
sawa na kuambiwa nguruwe ni haramu ukasema
utamtawadhisha na utakapomchinja utaelekea kibla. Ni sawa na kufunga mwezi wa Ramadhani na
inapofika saa tisa ya mchana na ubao wa njaa
unakuuma ukaamua kufunga mapazia ili kiingie
kiza upate kufuturu. Mbona sie mbumbumbu wa mambo ya Katiba na ya
Kisheria, ambao ndio wengi zaidi, tunaiona hii
lakini wanasheria wetu hawaiulizi na
wakionyeshwa hawataki kuiona? Kulikoni? Sawa,
tuliungana ndani ya Muungano, lakini na nani na
yuwapi? Tukikubali kuendelea kujiita Tanzania/ Watanzania kuwa ni sawa na Jamhuri ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, ni sawa na
mke aliezaa udogoni kesha yule mwanawe akaja
hamia kwako na kwa sababu ni mtoto wako wa
kwanza akaja kusimamia mirathi yako dhidi ya
wanao halali. Kiislam hiyo ni batili lakini jamii inasema inamuonea
huruma kizuka ambae ni ***** aliemzaa!
Ukiwauliza wale watoto wako halali, maslahi na
mustakbali wao jee? Jawabu wote ni ndugu kwa
mama! Na ndio maana wamewaachia fahawisha
wanasheria wetu wasasambue Katiba ya
Muungano na kasoro zake badala ya kuichukua
Katiba ya Zanzibar na kuipa dozi ya msimamo wa
kuikomboa Zanzibar ili izidi kupewa nguvu ya
“People’s Power” kupitia Kura ya Maoni, na imtishe atakayeijia Zanzibar kwa nia ya kutaka kuendelea
kuitawala kikatiba. Badala yake tunasasambua
Katiba isiyotuhusu. Chengine cha kustaajabisha ni wako wanaofika
hadi kulalamika kwanini TVZ na Redio Zanzibar
haitangazi mijadala ya makongamano ya Katiba ili
wananchi wapate kuilimika? Kuupeleka umma
kwenye Katiba ya Muungano badala ya Katiba ya
Zanzibar ni kuuilimisha au kuupumbaza? Katiba ya Zanzibar ndio iwe mada na dira yetu ya
siku na ya kila siku dhidi ya Katiba yao! Tunasema
Katiba yao iko tayari na ni Khati za Muungano na
Katiba ya Muungano. Hapana! Wao wana mchakato
wao wenye mtizamo wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano ijayo! Sisi tunatakiwa tushiriki ili papatikane njia ya “mkato” ili tusicheleweshe
kuiweka Katiba yao. Na mtego wenyewe uko hapa. Kwa kushiriki
kwetu katika Katiba ya Muungano tutakuwa
tumeivunja Zanzibar kwa mikono yetu wenyewe
na kuidhoofisha kikatiba! Kivipi na nani
atakayechaguliwa kuifanya kazi hiyo? Atatafutwa
mtu au watu ndani ya vyama vya siasa ambao wanaonekana “wanasikilizwa” na ambao
wanaonekana ni “moderates” ambao wako tayari
kwenda na kujiweka kwenye mapaja ya kundi la
wahafidhina linakula kutoka Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na ambalo haliwezi kuzikosa fadhila zao
za kisiasa na za kimali. Zanzibar inakabiliwa na hatari kubwa kutokana na
wale ambao tunakula nao na tunakunywa nao
kumbe wana ajenda ya siri ya kumtumikia Mtawala
Mkoloni kutoka Bara ili wajijengee nafasi za baadae
za kuunenepesha uroho wao kwa kutarajia
kutunzwa madaraka ya “kuiongoza” Zanzibar. Hawa ni viongozi ambao wameweka maslahi yao
binafsi ya kisiasa mbele zaidi kuliko kuirudishia
Zanzibar haki zake za Kitaifa na za Kimataifa kabla
ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar tarehe 26 Aprili, 1964. Wanasheria wetu wako mstari wa mbele
wanakimbilia wawemo kugombea uundaji na
uandishi wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano na
ukitizama wote ni wanasheria.
Katiba ya Zanzibar ni gari letu la mwisho kabla ya
giza kuingia. Tusiwaachie madereva wanasheria wasioona vizuri kuliendesha usiku wakati Zanzibar
kumeshakucha. Kwa kumalizia, someni haya maneno aliyoniandikia
mzalendo wa Kizanzibari asieyumba:
“Sasa ni kuelezana ukweli machoni na zile haya za
wazee wetu zilizotufanyia ugumu wa kujikomboa
ziishe!”


Mbona tunapenda kubembeleza visivyobembelezeka? Bara inafaidikaje na Zanzibar? Mbona kama vile Zanzibar inapata hasara kwenye Muungano? Ifike wakati hii mbeleko itatuke tu na iwe ya kuvuja kwa pakacha
 
Back
Top Bottom