Ya Viongozi wa Chadema na Kamati kuu, CDM ijipange?

Aikaotana

Senior Member
Nov 11, 2010
199
9
Nilikuwa miongoni wa waliolaumu uamuzi wale wabunge waCDM kususa hotuba, Niliainisha kwenye moja ya posting zangu kuwa (hapa nanukuu) ” Madai ya KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI NI YA MSINGI, kuacha kuingia katika vikao vyote vya bunge hadi madai hayo yatakapotekelezwa ni ujasiri, kutoka bungeni wakati hotuba ya raisi inaanza ni Unafiki, uzandiki, roho mbaya, ubinafsi na kuendeleza chuki zisizo na maana, sasa mwenye akili apime kutoka bungeni na kubaki kipi kinajenga heshima,kushawishi hata wabunge wasio wa chama chako kukubali hoja hizo ili ipatikane katiba na tume huru ya uchaguzi? Ninachofahamu madai ni ya msingi lakn njia iliyotumika inaturudisha nyuma sana, tunawategemea wabunge wa ccm katika hili, ACHENI UTOTO NA SIASA ZA CHUKI, CHADEMA WAMECHEMSHA NA LAZIMA WAAMBIWE?’ (mwisho wa kunukuu).
Yaliyoendelea kuhusu kuvuliwa unaibu upinzani bungeni kwa Zitto niliona ni yale yale, nikafikia kutoa maoni kwa formula hapa JF na hapa nanukuu TENA.
YR 2010, Mh. Zitto(ujana&maendeleo duni Kigoma)+ Slaa(agenda ya Ufisadi &Kanisa)=Kura mil.2, MP23
YR2015 ‘Absence of zito in Chadema + CCM kuteua mgombea Mkristo = kura laki 3 MP 5.
This marks end of CDM
Wenye msimamo mkali hapa JF hawakusita kuchafua hali ya hewa, wakisema asulubiweeeeeeeeee, msalitiiiiiiiiiiiiiiiii, wakasahau mchango wa Zitto CDM, wengine wakafikia kusema Mh Zitto alijiunga na CDM akaikuta na umaarufu iliyonayo leo.No! navyofahamu alijiunga tokea enzi za Dr Kabourou na ni mtu ambaye hata alipokuwa UDSM alikuwa anashiriki vikao mbalimbali vya Chama, Personally nilishuhudia hilo.
Point yangu hapa nataka ieleweke wazi kuwa Baada ya Kamati kuu kutoa kauli ya kumtambua Rais na kumrudishia ZK uongozi hadi uchunguzi utakapofanyika imezidi kumpandisha ZK na kuonyesha kuwa alikuwa sahihi katika uamuzi wake, ikimaanisha kuwa ana Busara za kushinda Mwenyekiti wake na Katibu wake pia .Viongozi hawa wawili ambao kila siku naona ndio watakaoiangusha CDM kwa ajili ya siasa za fisasi,Chuki,Ubinafsi, Kutaka sifa (hata kama chama kitaathirika) inaonesha hata hawakutaka ushauri wa kamati kuu kususia hotuba ya JK na kutomtambua kama Rais(ambapo baadae wakajichanganya eti ilikuwa ni madai ya katiba mpya, tume huru na kutokubali matokeo ya tume, after thoughts???). Kitendo hiki ni udhaifu mkubwa na sasa naona mantiki ya ZK kuomba uenyekiti wakati ule ambapo hata mimi nilimlaumu.
Sijui Mipango walionayo CDM kwa sasa lakini nawasihi wazee hawa wajipange kukisaidia chama kwa ushauri wa mara kwa mara na sio kusubiri wanachemsha, Baada ya hili la ZK wajitahidi kuondoa dhana ya ukaskazini na udini ambayo wanaCDM wapende wasipende imejionesha kwenye uchaguzi uliopita, wakirudishe kuwa chama cha Watanzania wote kama wanataka waaminiwe na kupewa dhamana ya kuongoza nchi. CDM iwe na Mipango thabiti na ya muda mrefu nakumbuka kwenye POST moja mwana JF mmoja kama ilivyo kwa wengi alijinasibu sana kukusanya wanachama, eti tokea uchaguzi aliwapata 124, na kwamba ZK hata akiondoka hakutakua na effect yeyote nakumbuka nilimwambia hivi, nanukuu,
” I dream chama makini chenye mipango , mipango ya miaka at least 20 hivi ijayo. Kiwe na programu maalumu ya kupata wanachama wasomi vijana, kuwe na programme ya semina elekezi kutoka kwa wataalamu waliobobea ktk siasa, waendelee kusoma na kufanya kazi zao,(their proffesionals) huku wakiwaelimisha jamii wanamotoka umuhimu wa mabadiliko, uhusiano kati ya kura na maendeleo ya kijamii na hivyo kujua umuhimu wa kupiga kura na kwa nini kuna vyama vingi, haya yote wayafanye kama volunteers wakibadilishana katika vipindi tofautitofauti vya masomo yao,Likizo , PT, disertation na hata wakati wakiwa ktk maeneo yao walimoajiriwa. Aidha viongozi wa juu wawe wanawatambua wanawaenzi na kuwatia moyo, wao wenyewe wawe na programu za kwenda vijijini kwa mwaka si chini ya operation 5, wakafungue matawi na kuwatambulisha vijana WAPIGANAJI katika maeneo yao.mwisho wa kunukuu.
Mambo haya hayawezi kufanywa na viongozi wanaotaka uraisi kesho, au kesho kutwa.Tulionao sasa, kama ni wazalendo kweli, waanzishe harakati na wakubali kuwa wakati muafaka wa kutwaa nchi hii wao WATAKUWA WAMESTAAFU, Maana watakuwa wamechoka! ikumbukwe CCM ni chama chenye zaidi ya miaka 40, kina mizizi isiyoweza kungoka kwa agenda moja tu UFISADI, inahitajika mipango ya Muda mrefu.
NAWASILISHA
 

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,604
1,065
Mwenyekiti wa kamati kuu ni Mbowe.
Katibu wa kamati kuu ni Slaa.
Unapaswa kujua kuwa kususia hotuba ya JK ilikuwa kuuonyesha ulimwengu kuwa kuna kasoro katika uchaguzi. Kumkubali JK kuwa ni rais, tangu mwanzo CDM hawakusema JK hakushinda ila walisema tuhakiki matokeo kwa fomu zilizosainiwa na mawakala katika kila jimbo. Matokeo waliyokuwa nayo CDM yalionyesha JK 44.65 na Slaa 44.56, bado JK ni mshindi. Waliyokataa cdm ni ile 61.
Kuhusu Zitto kurudishwa uongozi, ukumbuke waliomvua uongozi ni wabunge wenzake, hivyo kwa chama chenye demokrasia ya kweli, uamuzi wa wabunge siyo wa mwisho - hivyo ngazi ya juu imefanya kazi yake. Nadhani hapa cdm wanafanya sahihi kabisa. Na wanaosema Mbowe ni dikteta, kwenye wabunge waliomuondoa zitto alikuwemo na kamati kuu yeye ndiye mwenyekiti - kwa nini hakutumia udikteta kwenye kamati kuu?
This is pure democracy at work - migongano na misimamo tofauti ni suala la kawaida kila penye mkusanyiko wa watu.
 

Aikaotana

Senior Member
Nov 11, 2010
199
9
masikini KK
Look! Matokeo waliyokuwa nayo CDM yalionyesha JK 44.65 na Slaa 44.56,
Matokeo! 44.65 vs 44.56, Wabunge ccm >200, vs cdm 23 nimekuamini wewe mwanasiasa,
Unapaswa kujua kuwa kususia hotuba ya JK ilikuwa kuuonyesha ulimwengu kuwa kuna kasoro katika uchaguzi
after thoughts!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
kwa nini hakutumia udikteta kwenye kamati kuu?
Asingewaweza pale kuna wataalamu wenye elimu na busara , kwa wale wabunge wa viti maalum na wengi hawajui siasalazima awaburuze wanamuogopa mnooooo
 

Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,170
10,744
" I dream chama makini chenye mipango , mipango ya miaka at least 20 hivi ijayo. Kiwe na programu maalumu ya kupata wanachama wasomi vijana, kuwe na programme ya semina elekezi kutoka kwa wataalamu waliobobea ktk siasa, waendelee kusoma na kufanya kazi zao,(their proffesionals) huku wakiwaelimisha jamii wanamotoka umuhimu wa mabadiliko, uhusiano kati ya kura na maendeleo ya kijamii na hivyo kujua umuhimu wa kupiga kura na kwa nini kuna vyama vingi, haya yote wayafanye kama volunteers wakibadilishana katika vipindi tofautitofauti vya masomo yao,Likizo , PT, disertation na hata wakati wakiwa ktk maeneo yao walimoajiriwa. Aidha viongozi wa juu wawe wanawatambua wanawaenzi na kuwatia moyo, wao wenyewe wawe na programu za kwenda vijijini kwa mwaka si chini ya operation 5, wakafungue matawi na kuwatambulisha vijana WAPIGANAJI katika maeneo yao.mwisho wa kunukuu.
Mambo haya hayawezi kufanywa na viongozi wanaotaka uraisi kesho, au kesho kutwa.Tulionao sasa, kama ni wazalendo kweli, waanzishe harakati na wakubali kuwa wakati muafaka wa kutwaa nchi hii wao WATAKUWA WAMESTAAFU, Maana watakuwa wamechoka! ikumbukwe CCM ni chama chenye zaidi ya miaka 40, kina mizizi isiyoweza kungoka kwa agenda moja tu UFISADI, inahitajika mipango ya Muda mrefu.
NAWASILISHA


Nimeipenda article yako, kuna maswali mengi na kuna ukweli mwingi.Hongera kwa kuthubutu, kutukanwa na baadhi ya wanachadema ni kawaida na usiogope hilo, ni bora uwe huru kwa mawazo kuliko kuwa mtumwa wa mawazo ya wengine!

I told people long ago, that Zito yuko mbali sana miaka hamsini mbele! nilitukanwa pia, kama wengine watakavyotukana tena. Hili la juzi ni dhahiri limempa chat na kuwaaibisha tena akina Slaa However, sababu ya Zito aliyoitoa kuhusiana na JK eti ameleta maendeleo was childish and thanks that he apologized right here at JF, go to Zito's posts you will find that statement. you know what..people made mistake, we all make one or two,kama wale wabunge wana upendo hawakutakiwa kujiaibisha kumpigia mtu kura asiyekuwepo na kesho yake kushushuliwa in THE MEETING THAT SLAA AND MBOWE WAS THERE!! very same SLAA ambey alitakiwa kuwa rais!!! kuhukumu mtu ambaye hajasikilizwa ni sawa kwake, leo nikiwa na ushawishi wa kusema sina 'imani naye' basi aondoke even hata kama nina personal beef!!

Slaa anasahau chachandu yake na Zito ndio imekifanya chadema kuwa hivi, wabunge wengine (kwanu huwa naona hawapo) wanafuata mkumbo wanasahau kesho zamu ya mwingine!!!

Nashukuru pia umetoa ushauri wa nini kifanyike, usishangae kwa ushauri huu ukatukanwa pia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! hawashauriki ndio uzuri wao!
 

Nyangomboli

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
3,400
1,774
zito yuko mbali miaka 50 mbele? your not serious. mdanganyeni tu mwenzenu. we have a new tz. kalagabaho.
 

Aikaotana

Senior Member
Nov 11, 2010
199
9
Naona unajichanganya sana.


Sishangai, hii ndio aina ya watu wasio na umakini waliojaa Chadema, hii ndio inayoreflect pia uongozi wa juu (mwenyekiti na Katibu wa CDM) huwezi amini hawasomi , hawatafakari lakini mabingwa wa kujenga hoja !
 

ngwendu

JF-Expert Member
Jun 7, 2010
1,965
173
All, we know chadema ni nguvu ya soda tu. Is different from CUF. Kama alivyosema mleta thread hapa, ngoja tu 2015 CCM ilete mkristo hapa, utaona, ukizingatia maeneo ambapo wameshinda ni kwenye makanisa mengi, refer gazeti la Habari leo kitendo cha kanisa katoliki kukataa kumzika muumini wao kisa mwanaCCM. Halafu mitaahira mingine humu yanadai eti chadema hakikua chama cha kanisa. this is shame.
Natamani siku zote mmfukuze zito ili kaburi lenu lije hivi karibuni. Si mnaona umaarufu wa slaa/chadema kigoma ni sawa na zero, ndio maana hata kafulila alipohama tu na jimbo likapotea. for sure I liked it.
note; chadema hamna democracy. mpaka hata shibuda kakubali, mwera (ex chadema mbunge-tarime) alishasema, m/kiti wa wanawake kakimbia na chama kabisa. We are still watching a good fallup of chadema.
 

Aikaotana

Senior Member
Nov 11, 2010
199
9
Ngwendu there you are, walishindwa kumsaidia hata Mbunge mteule wa Kigoma mjini, Mlei, probably kwa ajili ya dini yake na umagharibi mpaka ubunge wake ulipochakachuliwa na kutangazwa mgombea wa CCM, Peter
 

Mkerio

Member
Mar 12, 2006
35
0
All, we know chadema ni nguvu ya soda tu. Is different from CUF. Kama alivyosema mleta thread hapa, ngoja tu 2015 CCM ilete mkristo hapa, utaona, ukizingatia maeneo ambapo wameshinda ni kwenye makanisa mengi, refer gazeti la Habari leo kitendo cha kanisa katoliki kukataa kumzika muumini wao kisa mwanaCCM. Halafu mitaahira mingine humu yanadai eti chadema hakikua chama cha kanisa. this is shame.
Natamani siku zote mmfukuze zito ili kaburi lenu lije hivi karibuni. Si mnaona umaarufu wa slaa/chadema kigoma ni sawa na zero, ndio maana hata kafulila alipohama tu na jimbo likapotea. for sure I liked it.
note; chadema hamna democracy. mpaka hata shibuda kakubali, mwera (ex chadema mbunge-tarime) alishasema, m/kiti wa wanawake kakimbia na chama kabisa. We are still watching a good fallup of chadema.

Jaribu ku argue sio ku shout. Jamani wana JF tukitaka tuelimishane tujenge hoja si kutumia hasira. Hilo la kanisa tumeandika sana. Kwamba kanisa haliwatengi wakristo kwa kushabikia ccm ila kwa kushabikia kumkufuru Mwenyezi Mungu. Huyo mgombea wa ccm Rukwa alisema yeye ni Yesu, mgombea urais ni Mungu baba na diwani ni Roho Mtakatifu. Kanisa lililaani na kuwakataza waumini kumshabikia mtu nayekufuru. Nikuulize na chuki zxako, mgombea akijilinganisha na Mtume na kusema mgombea urais ni Mwenyezi Mungu, wewe kama mwiskamu ungejisikiaje?
 

Aikaotana

Senior Member
Nov 11, 2010
199
9
HTML:
Huyo mgombea wa ccm Rukwa alisema yeye ni Yesu, mgombea urais ni Mungu baba na diwani ni Roho Mtakatifu. Kanisa lililaani na kuwakataza waumini kumshabikia mtu nayekufuru
Kama maneno hayo hayo yangesemwa na Mgombea mkristo na akashinda tusingekuwa na khadithi za kutengana na kunyanganywa ukristo kwa baadhi ya waumini
 

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,115
3,058
Teh teh teh teh

Kwani tangu lini chadema kuna viongozi? ha ha uha ha ha Usitupe lulu mbele ya nguruwe maana watazikanyanga kanyanga na hao nguruwe wakugeukie na wakulaluwe mwenyewe . Unaona lulu za CHACHA zilivyokanyangwa kanyagwa. Ohhhhhhhhhhh
 

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
57
ACHA MAJUNGU IJIPANGE NINI HASA?Kwa faida ya wale ambao hawakuipata TAARIFA KAMILI YA CHADEMA
Najua kuna wengi huenda hawakuipata hii. Nimeitafuta sijaiona jamvini baada ya rafiki kuniambia niitafute. Ila nimeikuta feacebook yake. Wanaoitafuta kama mimi, hii hapa

Msimamo wa Chadema haujabadilika

by Dr. Wilbrod Slaa on Tuesday, December 14, 2010 at 7:29pmKuna taarifa ambazo zimekuwa zikiandikwa na kuripotiwa na vyombo vya habari ambavyo zinaashiria kuwa Chadema tumebadili msimamo wetu kuhusu masuala ya uchaguzi.

Hakuna mahali popote Chadema imebadili msimamo wake na kusema kuwa Kura hazijaibiwa au kuchakachuliwa. Taarifa niliyotoa jana kwa TBC ilieleza wazi kuwa Kamati Kuu, ilipokea na kujadili na kuridhia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na Sekretariat ya Chama kuwa Chadema imekataa matokeo ya Uchaguzi kutokana na irregularities 15. Chadema inaamini kuwa iwapo Katiba ya nchi isingelikuwa imezuia kuhoji matokeo ya uchaguzi Mkuu wa Rais mahakamani, matokeo hayo yangeliweza kubatilishwa. Kwa vile Katiba inakataza kuhoji matokeo kuhojiwa mahakamani, basi japo Kikwete's Presidency ni Lawful it is Illegitimate.

Chadema ilitumia maneno ya kiingereza kuonyesha tofuati kubwa kati ya maneno hayo mawili. Huo ndio msimamo wa Chadema toka mwanzo na haijawahi kuyumba, japo maneno ya kiswahili yamekuwa yakipewa tafsiri tofauti na watu mbalimbali. Ni kwa msingi huo, Kamati Kuu ikasisitiza " Kuundwa kwa Tume Huru" kuchunguza Dosari " Irregularities" hizo kubwa katika uchaguzi. Nasisitiza, Chadema ni Chama ambacho toka mwanzo ilisisitiza kuwa "Haiko Tayari kuingia Ikulu kwa kumwaga Damu ya Watanzania".

Inawezekana wanaopenda na kufurahia vurugu, Chadema haiko tayari kwa hali hiyo. Tunasukumwa sana na wapenzi na wanachame wetu kutoka mitaani na kuandamana, na ndicho pia wanachotaka ndugu zetu akina Mwanakijiji. Maandamano, (ya amani au ya kushinikiza), kwa watu wanaojua mchakato wa demokrasia ni hatua ya mwisho kabisa baada ya njia zingine zote kushindikana. Pili, ili Tanzania isiingie katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015 kwa Katiba na Sheria mbovu kama tuliyonayo leo, Chadema inasisitiza upatikanaji wa Katiba mpya, Shirikishi na ya Wananchi.

Upatakanaji wa Katiba hii utakuwa na mchakato, na kama Serikali haitaki, basi Chadema kwa kushirikiana na wadau na watu mbalimbali wakiwemo wananchi itatutumia njia zote zinazoweza kuipatia nchi Katiba ya Wananchi. Yote haya ni mchakato, na kwa mtu yeyote anayoamini kuwa mchakato huchukua muda, basi atakuwa mvumilivu. Hakuna sababu ya kutumia lugha kali, kukashifiana na kutukanana japo jamvi letu ni mahali ambapo "we dare to speak". Tukivumiliana na kuheshimiana tutafika salama bandarini.

Tukikurupuka tunaweza pia tusifikie lengo tunalotaka. Hekima na busara vikitawala na kuongoza matunda yatakuwa mazuri kwa Taifa letu. Taifa ni letu tukilibomoa hatuna pengine pa kwenda, labda tukiamua kulowea penginepo. Tukikurupuka tunaweza kuwaumiza wanaohusika na wasiohusika. Uvumilivu na Busara daima huvuta heri.
Source: Gonga hapa Msimamo wa Chadema haujabadilika | Facebook


NYONGEZA: Kuna thread imewekwa hapa chini na Mwanajamii mmoja (Chapakazi) anauliza tofauti ya maneno haya mawili (Lawful na Legitimate). Kwa uelewa wangu. Naomba niiongeze hapa kwa mtiririko sahihi. Unaweza toa usahihi zaidi


Moja ya tafsiri za legitimate zilizoko kwenye link hii define: legitimate - Google Search


Zinasema kitu
legitimate ni kile ambacho kiko affirmed to be just na in accordance with recognized or accepted standards or principles.


Na kitu
lawful ni kitu ambacho kiko recognized or sanctioned by law(lawful: meaning and definitions — Infoplease.com.


Kwa upeo wangu hii inamanishaa kitu kinaweza kuwa recognize na sheria lakini kisiwe just kwa sababu hakikiendana na accepted principlesTukitumia mfano wa tukio lenyewe naweza kusema hivi,

Sheria inasema Raisi ni Raisi kwa kutangazwa na tume (lawful) lakini ili atangazwe lazima kanuni (principle) kadhaa zifuatwe.


Hivyo kama kanuni hazikufuatwa lakini katangazwa (kama sheria inavyotaka) na tume ya uchaguzi basi ni lawful kwa sababu katangazwa kisheria na tume yenye mamlaka ya kisheria kutangaza lakini kama kanuni za kufuatwa ili atangazwe zimevunjwa tunasema ni illegitimate kwa sababu principle s zimekiukwa.


Kwa msaada zaidi gonga hili link uone mfano kule Georgia

http://georgiandaily.com/index.php?o...2829&Itemid=68
 

Aikaotana

Senior Member
Nov 11, 2010
199
9
i will tell u how are all these after thaughts, unachotaka kusema hapa ni kwamba kiongozi mmoja wa chadema anaweza kutoa msimamo wa chama halafu kiongozi mwingine wa chama hicho hicho asimuelewe nae akaeleza ya kwake, i am about to sleep.
 

Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
7,782
6,568
hahahahahahahahahahahahahah......u pipo a so fani

Yaan we mtu nilivyo sikupendi, ryt ka ungekuwa karibu yangu one day ningekumwagia tindikali usoni.
Kauli zako zimejaa kebehi sana, ka huwezi kucoment si uache? unalazimishwa? Aaargh,
Yaan ningekuwa na uwezo ningehack afu nikuBAN.., Shoga mbabe ww..:redfaces::redfaces:
 

Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
7,782
6,568
yupo mbali sana , huwezi kumlinganisha na mbowe wala Slaa, i think he deserve to be a chairman

Hapo umeJa**ba ka sio ku**ya kabsa., u cn't b serious umfananishe Zito na Slaa na Mbowe. Ni sawa na ufananishe Burj Dubai na Akiba house.
Great Thnker wengine bana..:(
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom