Ya Rutabanzibwa ni Hayo sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ya Rutabanzibwa ni Hayo sasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Elam, Jul 11, 2012.

 1. E

  Elam Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hoja ya j.makamba imemezwa, wajane wana nyanyasika, kigamboni imekufa nakuingia mdudu hatari wa siasa, magari yaliyotolewa na world bank kwamsaada wa kushuhulikia mambo ya ardhi ymeshindwa kulipiwa road insuarance, makadirio madogo ya badget yasio endana na utekelezaji pamoja na majukumu ya wizara. Sasa kunafaida gani kuwa nakiongozi asiye leta maendeleo ktk secta hata kama ni mnoko? Unoko tunao utaka niwakusimamia maendeleo endelevu, hatuna faida nakiongozi kamas Patric Rutabanzibwa anaye leta unoko uku secta ya ardhi ikididimia miradi ya maendeleo imekufa, miradi kama ya kigamboni,kurasini,makongo,arusha sakina,n.k yote imekufa..tunamkumbuka sana mama Balozi Salome Sijaona, JK tunaomba umhamishe huyu Rutabanzibwa anaimaliza secta ya Ardhi ambayo ndio secta mama ya maendeleo yoyote, shirika kama NHC lina endelea kwasababu haliko direct chini ya Rutabanzibwa, sina personal interest au chuki binafsi ila patrick rubanzibwa hatufai sisi wana nchi ktk secta ya ardhi
   
 2. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Wewe lazima utakuwa mmoja wa maafisa ardhi waliojilimbikizia viwanja enzi za huyo Mama uliyemtaja. Uzuri wa Patrick Rutabanzibwa waulize wananachi wa maeneo ya Kwembe. Kigamboni n akwingineko ambako watendaji mafisadi ndani ya wizara walikuwa tayari wamesahjipanga kuwapora ardhi yao. Miradi uliyoitaja haihafa isipokwa Patrick Rutabanzibwa kawauliza watendaji je mmezingatia sheria ipasavyo katika kutwaa ardhi husika toka mikononi mwa wananchi? ikwemo kifungu cha 3g cha asheria ya ardhi ya 1999 kinachotaka wananci ambao ardh yao inatwaliwa kulipwa fidia stahiki. Hivyo usitupotoshe anachofanya Patrick Rutabanzibwa ni kurejesha imani ya wananchi kwa CCM ambao ilipotezwa na miradi ya Bibi Salome Sijaona. Tazama kila mahali Bibi huyo alipopeleka miradi yake ya kifisadi kama vile Bunju, Goba nk katikaJimbo la Kawe na Luguruni. Kwembe na Mloganila katika Jimbo la Ubungo majimbo haya yaliangukia upinzania mwaka 2010 kutokana na dhuluma waliyofanyiwa wananchi kuporwa ardhi zao na watendaji waliokuwa chini ya Bibi Salome Sijaona ambaye alikuwa akiwalipa watendaji posho za kujikimu safarini watendaji wanaoenda kutwaa, kupima viwanja maeneo ya Bunju, Luguruni, Kwembe n.k .k hapa hapa mjini, na kisha wananchi kutakiwa kurejesha gharama hizi kupitia bei kubwa za viwanja vinavyouzwa na wizara ya ardhi kuanzaia Milioni 5 hado 30. Ni watanzania wangapi watamudu bei hizi za viwanja?
   
 3. g

  gnsulwa Senior Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 110
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inaonekana Salome ni CDM ndani ya CCM. Na type ya kina Salome ni wengi
   
 4. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,785
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  WATANABE Umechangia upuuzi hapa,naona umetumwa na Rutabanzibwa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  We inaonyesha umetoka usingizini, toa mavyama yako hapa. Tunachofanya ni evaluation. sijaona amepima viwanja vijibweni, kibada, kisota, bunju, mivumoni, kajiungeni nk. Ruta amefanya nini mav yako wewe? tunataka mtu anaedeliver, surveyor kucamp akimuacha mkewe na watoto nyumbani na kwenda kushinda pori na usiku aproces data ili kesho yake aendelee na kazi unaona ni ufisadi? Haya kwa kipindi hiki chote what tangible output tuliyoipata? masiasa kwenye utaalam yanakeraga sana.

   
 6. P

  Pilitoni JF-Expert Member

  #6
  Jul 11, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 1,001
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Rutabanzibwa ni jembe la ukweli,chuki binafsi zitawaua! Prof tibaijuka na rutabanzibwa juu! Mabwege mtakoma
   
 7. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #7
  Jul 11, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama kweli Rutabanzibwa ni jembe la ukweli atasikia kilio chetu dhidi ya afisa mipango miji wilaya ya Hai na huyu si mwingine bali fisadi wa viwanja aitwae MWARABU!! Huyu bwana amesababisha kesi chungu nzima za viwanja hapa Hai kutokana na ufisadi wake ; kumuondoa katika huo wadhifa utaleta amani katika wilaya hii.
   
 8. E

  Elam Member

  #8
  Jul 12, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kama Rutabanzibwa ni jembe niambie anashindwa vipi ata kulipia insurance za magari yaliyotolewa msaada na world bank ambayo yamepaki pale wizarani wiki ya 2 sasa..kazi zinasimam! Unoko au kufwata sheria kusiko leta maendeleo kunafaida gani, wewe uko radhi kufa bila maendeleo kwa kigezo chakufwata sheria..hakuna sheria yenye faida kama haiongozi maendeleo, ameua miradi yote sasa asilimia 10 tuu ya arhdi yote ya TZ ndio imepimwa hiyo ni kazi ya mama S.Sijaona nakumbuka kunasiku aliyekuwa Spika. Samweli Sitta alimfagila Bungeni yule mama kwa utendaji kazi mzuri..huyu bwana Rutabanzibwa ndio chanzo cha wanakigamboni kukataaa mradi wa mji mpya..na hasara inakuwa kwetu sisi wananchi. Kitendo cha kukataa mji mpya kwasababu ya siasa ni hasara kwetu sote waTanzania sio wanakigamboni tuu, Mafisadi ndio wanajimilikisha ardhi kiholela saivi..daraja likijengwa ndio utashuhudia haya niyasemayo apa jamvini, Rutabanzibwa hatufai waTanzania..bora astaafishwe..hafai ata kuwa diwani! angalia kila napopita anaribu tuu
   
 9. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Rutabanzibwa amebana ulaji, tulijua mtaanza kulialia.
   
 10. a

  a-dot Member

  #10
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 26
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 15
  Makazi bora nchi hii hayendelei kwa kuwa hakuna viwanja vinavyopimwa na kuuzwa kwa wananchi huyu jamaa amekazana kufuta tuu hati na kuvunja vunja huku makazi holela yanazidi kujengwa maeneo mengi ya DSM. Kama Rutabanzibwa ni jembe basi arudishe viwanja vya wazi vilivyochukuliwa na CCM, kwa mfano viwanja vya Mwananyamala na Kawe. Kazi ya huyu bwana ni kuvunja vunja tu na kufuta hati za umiliki wa ardhi kwa wananchi wa kawaida.
   
 11. MUSONI

  MUSONI JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Mimi nafikiri mkubwa huna hoja, umefika pale ardhi wanayotutesa wananchi na ni Rutabanzibwa ambaye kawanyoosha pamoja na kwamba ufedhuri na rushwa bado zinaendelea haswa pale gorofa la TATU ambapo ofisi nyingi zinazohusu viwanja , hati, ukaguzi ziko hapo nio manyanyaso kuliko....ongelea kuondoa hao na naona wewe kama mmoja wao...
  we need him there na tutampa data za kutosha amalize kero za wananchi.
  BRAVO Proff na RUTABANZIBWA.
   
 12. B

  Babu Ubwete Senior Member

  #12
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 26, 2008
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mama Sijaona wa the worst of em all. Hakuna ufanisi kabisa alipokuwa Ardhi kina Mushi waliendelea kudhulumu viwanja vya watu. Mpaka Kupata Hati ardhi ni usumbufu mkubwa nenda huku faili liko kule, kuja kukufanyia valuation mpaka ukate pesa ya kutosha. Bora ameondoka hapa mahali, ulikuwa ni msalaba wa chuma haubebeki.


   
 13. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,748
  Likes Received: 12,842
  Trophy Points: 280
  Mbona kama mtoa mada ana chuki binafsi? Povu limemtoka!
   
 14. K

  Kwaito Senior Member

  #14
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi hata sijui nan afadhali ila naona serikal na specifically wzr ya ardhi imeshindwa kaz!yan kuna maeneo sahz yamekuwa mapori ya kujifcha vibaka kisa serikal imesema mrad wa Lugurun umesitishwa na watu wasiendeleze kitu chochote
   
 15. m

  muhinda JF-Expert Member

  #15
  Jul 12, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 340
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Kwakeli Patrick R ni jibu kwa sis wanyonge.
  inaelekea mleta mada ameshapitiwa na fagio la bwana P. Na bado sana, maana wananchi tupo tayari kushirikiana naye kuwafichua nyinyi wabadhilifu, kazi kupoteza mafile ya watu tu..
   
Loading...