Baada ya Blandina Nyoni, zamu ya Patrick Rutabanzibwa Wa Wizara ya Ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baada ya Blandina Nyoni, zamu ya Patrick Rutabanzibwa Wa Wizara ya Ardhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Elam, Feb 10, 2012.

 1. E

  Elam Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimefurahishwa sana na taarifa za kusimamishwa kazi katibu mkuu wa wiazara ya afya ambaye imeonekana kuwa yeye nichanzo cha mgomo wa madaktari na kusababisha matatizo makubwa kwa watanzania wote kwa ujumla. Nikiwa kama mtaalamu wa fani ya manunuzi (procurement) nimesikitishwa pia na tuuma za huyu mama kukiuka taratibu za manunuzi ktk wizara ya Afya, kwakweli anatukosea heshima sana sisi wataalamu na kuizalilisha fani hii kwakuvunja sheria nataratibu zilizo undwa na bunge nakupitishwa na Raisi (sheria ya manunuzi 2004,2010). nadhani sheria hii inajieleza wazi hatua gani za kinidhamu inapaswa zichukuliwa kwa huyu mama Nyoni, natoa rai kwa vyombo husika kufwata sheria bila upendeleo.
  Mimi tatizo langu linakuja kwa huyu Bw. Patrick Rutabanzibwa, katibu mkuu wizara ya Ardhi. Huyu jamaa toka amewasili pale wizarani mambo mengi yemezorota kiutendaji kwa mfano hakuna mradi ata mmoja ulio hai pale yote inaendeshwa kama kiushaidi tuu. Amekuwa anakandamiza maendeleo kwa njia moja au nyingine kiasikwamba Mahakama ilishawahi kutoa tamko la kubatilisha uongozi wake kutokana na maamuzi aliyo yatoa yakamrudi mwenyewe. Serikali na vyombo vingine inabidi mjaribu kumwangalia vizuri huyu Bw.Rutabanzibwa kabla Bomu lingine halijalipuka. Ana roho kama ya mama nyoni, ukienda pale wizarani utajionea mwenyewe jinsi hali ilivyo..huduma ni mbovu, mambo hayaendi vizuri, imefikia hatua mpaka watendaji na watumishi ktk wizara hiyo wanadai hakuna bajeti kwa mwaka 20111/2012 kutokana nakukosa mambo yakuyaandikia bajeti. sasa jiulize New city Kigamboni imefia wapi? Kurasi redevelopment iko wapi? na miradi mingine mingi tuu haina utendaji wa uhakika tena.
  Kigamboni walipo mhamisha Mratibu bw.lamech Mtui kwa maslai ya Rutabanzibwa kumweka mtu wake Mr. Majura ndio chanzo kikuu cha kufa kwa huu mradi, madiwani wa huku kigamboni kwa pamoja walipinga hatua hii ya bwana rutabanzibwa kumwamisha mratibu wa huu mradi, lakini yeye kutokana na mabavu yake aliamua kufanya vile anaona ina masilahi kwake, pia alipofika tu pale wizarani Mkurugenzi wa utawala na rasilimali watu alimwamisha kinguvu toka pale kwenda wizara ya Sheria kisa wana personal conflict, sasa kwa mtindo huu tusubiri kulipuka kwa bomu jipya ktk sekta hii ya Ardhi either kutoka kwa wananchi au watumishi pale wizarani. Kwa ujumla huyu bwana ni mbovu ktk utendaji hasa hasa maamuzi yake ni kumnufaisha yeye mwenyewe..hakuna mtumishi anaye mpenda pale wizarani.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,585
  Likes Received: 4,693
  Trophy Points: 280
  Mwingine anayestahili kupigwa chini ni Baba Mwanaasha.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,560
  Likes Received: 18,289
  Trophy Points: 280
  Elam, kwa sisi tunaomfahamu vizuri Patrick Rutabanzibwa, huyu ndie katibu mkuu no nonsense no.1 aliyepo ndani ya serikali ya jk. Ukiona kuna mambo hayaendi basi ujue kuna madudu ameyaona na anabanana nayo.
   
 4. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Actually Patrick Rutabanzibwa alistahili kuchukua nafasi ya Luhanjo kwa jinsi utendaji wake ulivyo makini. Kabla hajaingia Wizara ya Ardhi migogor ya ardhi ilkuwa kila pembe kuanzia Luguruni hadi Kigamboni kwa watumishi wa wizara kuwanyang'anya wananchi ardhi zao kwa kisingizio cha kupima viwanja na kisha wakajilundikia mamia ya viwanja/

  Mafisadi hao wopte kapiga chini na wapo mitaani. Miradi ya Luguruni na Kigamboni haitekelzeki kutokana na jinsi ilivyokuwa imeasisiwa kuwanyang'anya wananchi ardhi zao, kitu ambacho chini ya Patrick hakiwezi kupitishwa wala kufanyika.
   
 5. E

  Elam Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kimtazamo wa haraka haraka huyu bwana utamsifia kila kona ya njia zake, sababu kubwa haruhusu image yake iharibike mbele ya public..kipindi alipokuwa mambo ya ndani ilikuwa kidogo tuu maovu yake yawe public..but anatumia intelligentsia ya hali ya juu sana kupotosha uma, alipopelekwa nishati na madini pia kuna madudu aliyafanya mpaka jamii ikajua refer www.chadema.co.tz utaona wmeandika mengi tuu..ila sasa mm nashauri tukae kimya kama hamkubali yakilipuka tuu msisikitike nakulaumu wadau! Huyu bwana ni makini sana kutenda nakuficha maovu, anuuwezo wa kuandaa maandamano ya watu 500 kumtetea, sishangai sana nikiona mnamtetea inawezekana your one part of his conspiracy formulation.
   
 6. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Taja madhambi yake moja moja, hata kutajwa katika list of shame ya CDM mwanzoni ilikuwa kwa makosa ndio maana katika second list jina lek halimo. Sisi wananchi tuliokuwa mbioni kudhulumiwa ardhi zetu na mafisadi kutoka wizara ya ardhi maeneo ya Kibamba na Kwembe tunajua umuhimu wa Patrick Rutabanzibwa
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Feb 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Huyo Rutabanzibwa ni nani na anatoka nchi gani? Hilo jina linanikumbusha balozi mmoja hivi tulikuwa naye miaka ya 90 akiitwa Bandora mzaliwa wa Tabora lakini akaishia kufutiwa uraia wake.
   
 8. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,042
  Likes Received: 382
  Trophy Points: 180
  Hapo kwenye RED naungana nawe kabisa kukosa huyu baba watu wangelizwa sana na damu labda ingemwagika. Vijana wa ardhi walifanya ufisadi wa hali ya juu kabisa ktk miradi hii. Mfano kulipa nyumba hewa, kulipa mazao hewa, kulipa wasio husika, kujilipa malipo hewa eti wamekaa Guest inaitwa Msalala ipo kwa Yusuph Mbezi wakilipa eti 150,000/= kwa siku wakati wa kufanya kazi, ikumbukwe walikaa kwa miezi mitatu. Mwisho wananchi wakatakiwa kulipia kila mita ya mraba Tsh 7,100/= ili kulipia gharama hizo. Huu ulikuwa ni ufisadi uliopitiliza na inawezekana mwandishi akawa mmoja wa vijana hao walionyang'anywa tonge mdomoni.

  Kwetu sisi wananchi tunakuombea kila la KHERI RUTA
   
 9. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Patrick Rutabanzibwa ni Mtanzania miaka ya 90 alikuwa Kamishna Wizara ya Nishati kabla ya kupata maradhi ya kupooza hivyo kukaa nje ya ofisi muda mrefu, aliporejea ofisini akakuta Serikali imeingia mkataba wa kifisadi na kampuni ya IPTL. Alichafanya ali[okuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ni kuagiza mitambo kama hiyo hiyo kutoka kwa mtengenezaji huyo huyo ambapo Serikali ikapatiwa bei ya chini sana hivyo akapat ushahidi kuwa IPTL iliibia Serikali hivyo Serikali kupata unafuu katika mkataba huo.

  Alikataa vishaiwshi vya kila aina kutoka kwa agent wa IPTL a,mbaye ni kabila moja na yeey kwa maslahi ya taifa.
   
 10. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Patrick Rutabanzibwa ni Mtanzania miaka ya 90 alikuwa Kamishna Wizara ya Nishati kabla ya kupata maradhi ya kupooza hivyo kukaa nje ya ofisi muda mrefu, aliporejea ofisini akakuta Serikali imeingia mkataba wa kifisadi na kampuni ya IPTL. Alichafanya ali[okuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ni kuagiza mitambo kama hiyo hiyo kutoka kwa mtengenezaji huyo huyo ambapo Serikali ikapatiwa bei ya chini sana hivyo akapat ushahidi kuwa IPTL iliibia Serikali hivyo Serikali kupata unafuu katika mkataba huo.

  Alikataa vishaiwshi vya kila aina kutoka kwa agent wa IPTL a,mbaye ni kabila moja na yeey kwa maslahi ya taifa.


  [TABLE="class: cms_table, width: 879"]
  [TR]
  [TD][TABLE="class: cms_table, width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  Prudence Karugendo​
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [TD="width: 140"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="class: cms_table, width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  KWA siku za karibuni zimekuwapo lawama kutoka kwa wananchi na taasisi mbalimbali za kiraia dhidi ya utendaji usioridhisha unaoonyeshwa na watumishi wa umma. Lawama hizo ambazo kwa kiasi kikubwa zinachochewa na tabia ya ukiukaji wa maadili ya utumishi wa umma ambayo imetokea kuzoeleka kwa lugha ya siku hizi kama ufisadi, kwa kiasi kikubwa zimebebwa na vyombo vya habari.

  Vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kuwanyooshea kidole watumishi wa umma wanaoonekana kuteleza na kutoka nje ya mstari wa maadili ya utumishi wao. Na kwa mwenendo huo vyombo vya habari vimepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa watumishi wa umma walio waadilifu.

  Vimejipatia sifa ya kuufichua na kuufunua uovu uliomo kwenye utumishi wa umma ikiaminika kwamba vyombo hivyo havifanyi hivyo kwa lengo la kumkomoa yoyote bali kuwafanya wahusika wajirudi na kuyazingatia maadili ya utumishi wao kwa manufaa ya jamii nzima ya Watanzania.

  Lakini bahati mbaya kwa sasa kuna minong'ono ya chini chini kuhusu namna vyombo hivyo vya habari vinavyozishughulikia tuhuma za uovu wa watumishi wa umma.

  Inasemekana kwamba kwa sasa tuhuma za uovu zinapotolewa vyombo vya habari vinataka zibaki tu ni tuhuma hata pale zinaposafishwa au kupatiwa ufumbuzi kwa kuonyesha kwamba kilichodhaniwa ni uovu kumbe siyo.

  Papo hapo tuhuma nyingine kuonekana zikifumbiwa macho na vyombo vya habari.
  Minong'ono hiyo imejitokeza kutokana na sakata la Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa, lililokuzwa kwa njia ya kumsakama hadi kufikia kiongozi huyo kuhukumiwa katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kulipa faini ya shilingi laki tano au kwenda jela miezi 6 kwa kilichodaiwa kuidharau mahakama, kabla ya Mahakama ya Rufaa kuibatilisha hukumu hiyo.

  Mpaka sasa ni wananchi wachache wanaoelewa kwamba Mahakama ya Rufaa iliibatilisha hukumu iliyokuwa imewatia Rutabanzibwa na wenzake hatiani.

  Wananchi wengi wanaomfahamu vizuri walikuwa bado wanamsikitikia kutokana na hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Ardhi bila kuelewa kuwa ilishatenguliwa kufuatia vyombo vingi vya habari kukaa kimya juu ya jambo hilo.

  Kitendo cha vyombo vya habari kutolipa uzito wa kutosha suala la kubatilishwa kwa hukumu dhidi ya Rutabanzibwa kimeitia dosari sifa iliyokuwa ikitolewa kwa mhimili huo wa nne usio rasmi wa nchi.

  Kwa sasa imeanza kutafsiriwa kwamba kumbe zilizokuwa zinaonekana kama juhudi za kuufichua uovu zilizokuwa zinafanywa na vyombo vya habari ndani yake kuna kukomoana tofauti na ilivyodhaniwa mwanzo. Huu ndio ni wakati mzuri wa vyombo vya habari kuikana tafsiri hiyo.

  Vinginevyo nguvu ya vyombo vya habari inayotumika kuufichua uovu ingebaki endelevu hata pale sehemu husika inapokuwa imetakaswa ili kudhihirisha kwamba vyombo vya habari havilengi kukomoa bali kurekebisha. Pia hiyo inaondoa dhana ya kwamba vyombo vya habari vinatumiwa na baadhi ya watu kwa ajili ya malengo binafsi.

  Kwa ajili hiyo nimeamua kufuatilia sakata hilo la Rutabanzibwa ili nione kilichojiri mpaka kufikia Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutoa adhabu hiyo ambayo baadaye ilikuja kubatilishwa na Mahakama ya Rufaa. Niliyoyagundua katika kufuatilia kwangu ni ya kushangaza na kusikitisha.

  Kwanza ni kwamba kilichomponza Rutabanzibwa ni msimamo wake wa kuyasimamia maadili ya kazi na kutokubali kuyumbishwa kwa namna yoyote kutoka kwenye maamuzi halali anayoyaamini na kuyasimamia.

  Hayo nimeyagundua baada ya kuisoma barua aliyoandikiwa tarehe 5/7/2011 na taasisi moja ya Kiislamu, barua hiyo iliyojaa matusi na vitisho vya kila aina, iliyonakiliwa kuanzia Ikulu kwa rais, taasisi mbalimbali za serikali na za kidini, hadi kwa ndugu, jamaa na marafiki waRutabanzibwa.

  Ilikuwa ikimtaka Rutabanzibwa na wenzake, kama wao na si kwa nafasi zao, kusaini hati za viwanja Na. 1272 na 1273 vilivyopo katika eneo la Msasani Peninsula, jijini Dar es salaam, katika muda wa siku nne tangu alipopata barua hiyo.

  Kama kawaida yake, Rutabanzibwa si mtu wa kutetereshwa na matusi wala kurubuniwa kwa njia yoyote ile. Kawaida yake ni kusimamia usahihi na ukweli. Ndiyo maana hakusaini hati hizo kama alivyotakiwa na barua hiyo. Ni imani yangu kwamba hakufanya hivyo kutokana na kuyazingatia zaidi maadili ya utumishi wake.

  Kadhia hiyo ndiyo iliyosababisha Mahakama ya Ardhi kumuamuru Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kutoa hati ya viwanja vile vile Na. 1272 na 1273 Msasani Peninsula, vinavyotajwa kwenye barua hiyo ya vitisho.

  Viwanja ambavyo kimsingi havina uhusiano wowote na taasisi hiyo ya Kiislamu iliyokuwa ikitoa vitisho kwa Rutabanzibwa.

  Inasemekana viwanja hivyo ambavyo katika ramani ya jiji vinapaswa kuwa sehemu ya wazi vilipatikana baada ya serikali kutumia viwanja viwili Na. 1860 na 1861 ambavyo vilionekana kama viko katika umiliki wa Oysterbay Properties LTD kule kule katika maeneo ya Msasani Peninsula na baadaye umiliki wa viwanja hivyo kuhamia kwa Kampuni ya Kahama Mining Corporation LTD.

  Lakini hata hivyo inaaminika kwamba viwanja hivyo viwili, Na. 1860 na 1861 vilivyokuwa vinamilikiwa na Oysterbay Properties na baadaye Kahama Mining Corporation navyo vilikuwa katika eneo la wazi ambalo baadaye lilitumika kujengwa shule ya watoto wadogo ambayo mmiliki wa Oysterbay Properties alikuwa mmoja wa wadhamini kabla ya viwanja hivyo havijageuka kuwa mali ya Oysterbay Properties.

  Kumbukumbu zinaonyesha kwamba kulitokea mvutano kati ya serikali na Oysterbay Properties mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambapo serikali ilikuwa inaonyesha kwamba viwanja hivyo viko katika eneo la wazi na kwa upande mwingine Oysterbay Properties ikidai kwamba viwanja hivyo ni mali yake.

  Ni katika kipindi hicho Waziri wa Elimu wa wakati huo, Joseph Mungai, akaagiza pajengwe Shule ya Sekondari ya Bongoyo katika eneo hilo. Miaka sita baadaye, Oysterbay Properties na Kahama Mining Corporation wakafungua shauri Na. 14 la 2008.

  Shauri hilo lilifunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi dhidi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kamishina wa Ardhi, wakidai kwamba viwanja hivyo ni mali ya Kahama Mining Corporation.

  Pia walikuwa wanataka majengo yaliyomo katika viwanja hivyo yabomolewe (Shule ya Sekondari ya Bongoyo) na waliovivamia waondoke.

  Mara baada ya shauri hilo kusajiliwa mahakamani ulitokea uahirishwaji wa mara kwa mara wa shauri hilo wakati pande mbili hizo zikitafuta kumaliza mambo nje ya mahakama, ili kama zingekubaliana zirudi tena mahakamani kuyasajili makubaliano hayo.

  Tarehe 16/10/2009 pande hizo mbili zikafikia muafaka na kuufikisha mahakamani kwa ajili ya kumbukumbu iliyohifadhiwa tarehe 19/10/2009. Tarehe hiyo Jaji Nchimbi akatoa maagizo mbele ya pande zote mbili kwamba kulingana na makubaliano yaliyofikishwa mahakamani hapo shauri hilo lilikuwa limepata muafaka.

  Jaji akaongeza kwamba namna muafaka ulivyokuwa mdaiwa wa kwanza angetoa viwanja mbadala ambavyo ni Na. 1272 na 1273 katika eneo la Msasani Peninsula ambavyo vingegeuzwa katika matumizi ya makazi/biashara na kisha kuamishiwa katika umiliki wa Oysterbay Properties LTD.

  Pamoja na mambo mengine mahakama ikathibitisha kwamba baada ya kusainiwa makubaliano hayo kusingekuwepo na madai mengine.

  Katika kuipitia hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi dhidi yaRutabanzibwa na wenzake, Mahakama ya Rufaa iliona kwamba makubaliano hayo yaliyofikiwa yalikuwa hayatoi uhalali kamili kwa pande zote mbili kwa vile bado yalikuwa yanategemea hatua zaidi ambazo zilihitajika kuchukuliwa baadaye.

  Kwamba kama hatua hizo zingeshindikana makubaliano hayo yangebaki ni nyaraka tupu zisizoweza kutoa haki yoyote kwa pande zote mbili.

  Mahakama ya Rufaa ikaongeza kwamba iwapo vigezo vya mkataba ni vya mashaka au havijakamilika haiwezi kusemwa kwamba pande mbili zimefikia mkataba (makubaliano) mbele ya sheria. Tafsiri ni ya kwangu.

  "Makubaliano yenye mashaka, au yasiyoweza kutekelezwa bila mashaka, ni batili" Law of Contract Act (CAP 345 R.E. 2002) kifungu 29. Katika kubatilisha hukumu ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi dhidi ya Rutabanzibwa na wenzake.

  Mahakama ya Rufaa iliona kwamba wahukumiwa hao wangeweza kuchukuliwa kwa mtazamo wa harakaharaka kuwa nao ni sehemu ya shauri Na. 14 la 2008 kutokana na ukweli kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ambaye mashauri yote dhidi ya serikali yanapaswa yapitie kwake, alikuwa sehemu ya muafaka uliofikiwa.

  Lakini hata hivyo Mahakama ya Rufaa iliongeza kwamba chini ya kifungu 6(2) Mwanasheria Mkuu wa Serikali anaingia mara tu baada ya idara za serikali na maafisa wake kupokea notisi ya siku 90 za kujiandaa na shauri husika.

  Kwa kuwa Rutabanzibwa na wenzake hawakupewa notisi hiyo, moja kwa moja hawahusiki na shauri la Oysterbay Properties LTD na Kahama Mining Corporation LTD.

  Katika kuhitimisha hoja yake Mahakama ya Rufaa iliona kwamba kwa vile hapakuwepo makubaliano yoyote ambayo yangeweza kutekelezwa bila mashaka masuala yote yaliyofuatia yalikuwa ni batili kwa sababu hayakuwa na miguu ya kusimamia.

  Mpaka hapo tutaona kwamba taasisi ya Kiislamu iliyohusika kutoa vitisho kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ili kumshinikiza atoe hati za viwanja Na. 1272 na 1273, Msasani Peninsula, Dar es Salaam, haihusiki wala kutajwa mahali popote katika mgogoro mzima wa viwanja hivyo.

  Hiyo ndiyo inayoleta hisia kwamba nyuma ya mgogoro huo mzima wa viwanja hivyo walisimama watu waliotaka kutumia kila njia na kila mbinu kuhakikisha haramu inageuzwa kuwa halali hata kwa kutumia jina la Mungu.

  Kwahiyo kitendo cha vyombo vya habari kulipa uzito shauri na hatimaye hukumu ya Mahakama Kuu dhidi ya Rutabanzibwa, lakini vikageuka na kupooza pale shauri hilo lilipopelekwa katika Mahakama ya Rufaa, kimeacha maswali kwa wananchi.

  Wnanchi wanajiuliza kama kweli vyombo hivyo vya habari vimedhamiria kupambana na hatimaye kuitokomeza hali hii tata ya maisha inayotafsiriwa kama ufisadi katika jamii ya Watanzania? Na hapo ndipo linaponijia swali la kwamba katika sakata la Rutabanzibwavyombo vya habari vimefanya usaliti?

  [​IMG]

  prudencekarugendo@yahoo.com
  0784 989 512
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 11. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #11
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Nani anakumbuka Pale Victoria katika nyumba za National Housing Corporation (NHC) zilikuwa zikitumika kama parking yarda ya magari mengi meusi maalum kwa ajili ya kukodisha kwa ajili ya harusi. Basi siku moja huyu Bwana Patrick rutabanzabwa akiwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi yeny jukumu la kuismamia NHC akaenda hapo kama mteja kutaka kukodisha gari kwa ajili ya harusi baada ya mapatano akanza kuhoji uhalali wa nyumba ya NHC kutumika kama parking yard ikabainia kuwa eneo hilo limekodishwa na maafisa ya NHC ambao hupokea fedha na hazifiki NHC..

  Matokeo yake parking hiyo ikabidi itafute eneo lingine siku hizi nayaona magari hayo huko maghorifa ya Urafiki. Ni kisa gani cha fefha za shrika zikikuwa zinpotea kwa njia hiyo?
   
 12. t

  tonyking65 New Member

  #12
  Sep 11, 2013
  Joined: Sep 11, 2013
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila mtu ana uhuru wa kufikiri na kuamini atakalo, katiba inampa kila mtu uhuru huo. Kwa lile la Patrick Rutabanzibwa nashauri wale wanaomsema vibaya wajiulize yafuatayo: kama yeye alikuwa kikwazo alikokuwa nafanya kazi mbona hatukuwahi kusikia mgomo wa wafanyakazi? Mbona hakuwahi kupitishiwa azimio la bunge kama lile la Jairo? Mbona kapeta serikalini mpaka mwenyewe akaachia ngazi kwa hiari? Tafuta majibu halafu tuongee.... Wasalaam.
   
 13. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2013
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,483
  Likes Received: 5,570
  Trophy Points: 280
  Huyo mhaya mwenzake walikuwa hawapatani kabisa baada ya kuwatosa kwenye issue ya IPTL.Kaamua kustaafu mwenyewe ingawa wengi wanadhani ni baada ya hizi kashfa za juzi lakini alifanya pati ya kuaga utumishi kwa hiari mapema kabisa kabla ya kelele za hizo.

  Binafsi nafahamu machache kuhusu yeye kama mtu asiyeyumbishwa kwenye maamuzi lakini kuna uzi humu ulizungumzia mengi kuhusu yeye ambayo binafsi nilibaki njia panda.
   
Loading...