Ya Mtwara, Tafadhali Usininukuu!

Ya Mtwara, Tafadhali Usininukuu!

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,251

Ndugu zangu,

KWETU wanadamu, mengi yanayotufanya tufarakane na hata kugombana yanatokana na sisi wenyewe wanadamu. Na ndivyo ilivyo hata kwa ndege na wanyama.

Ukiwaona ndege wanagombana, ukiwaona kuku wanagombana, na hata ng’ombe, basi, sababu kubwa ni ya viumbe hao wenyewe. Na mara nyingi, kugombana huku hutokana na kugombania kisichotosha.



Hivyo basi, suluhu ya yale tunayogombania kama wanadamu yapaswa itokane na sisi wanadamu wenyewe. Na tangu karne ya 17 kuna wanadamu walioliona hili.



Mwanafalsafa Thomas Hobbes alibainisha, kuwa migogoro mingi miongoni mwetu hutokana na ushindani wa kugombania kisichotosha. Kwa vile sote tuna mahitaji yenye kufanana, basi, Thomas Hobbes anasema, kuwa migogoro hii itaendelea, kugombania kisichotosha.



Na Hobbes huyu anaamini, kutokana na hatari hii, basi, jukumu muhimu na kubwa kwa Serikali yeyote ile iwe ni kulinda amani ya nchi. Kwamba kwa kutofanya hivyo, jamii itarudi katika hali ya kutokuwa na taratibu; vurugu, kuuana, umasikini na kupelekea maisha mafupi.



Hata hivyo, tunaamini pia, kuwa siku zote, pasipo haki na usawa hakuna amani, ingawa, katika jamii yeyote ile, uwepo wa amani na utulivu ni msingi mzuri katika kutafuta haki na usawa, kwa njia ya majadiliano.
( Hii ni sehemu ya makala yangu kwenye Mwananchi, leo Jumapili)

Maggid Mjengwa,
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio
 
Fujo za Iringa ulimtaja Msigwa kwamba ndiye anahusika, sasa usiume maneno leo kutueleza fujo za Mtwara ni nani anahusika? uchambuzi wa kiujanjaujanja haukubariki kwa dunia ya leo.
 
Ndugu zangu,

KWETU wanadamu, mengi yanayotufanya tufarakane na hata kugombana yanatokana na sisi wenyewe wanadamu. Na ndivyo ilivyo hata kwa ndege na wanyama.

Ukiwaona ndege wanagombana, ukiwaona kuku wanagombana, na hata ng'ombe, basi, sababu kubwa ni ya viumbe hao wenyewe. Na mara nyingi, kugombana huku hutokana na kugombania kisichotosha.


Hivyo basi, suluhu ya yale tunayogombania kama wanadamu yapaswa itokane na sisi wanadamu wenyewe. Na tangu karne ya 17 kuna wanadamu walioliona hili.


Mwanafalsafa Thomas Hobbes alibainisha, kuwa migogoro mingi miongoni mwetu hutokana na ushindani wa kugombania kisichotosha. Kwa vile sote tuna mahitaji yenye kufanana, basi, Thomas Hobbes anasema, kuwa migogoro hii itaendelea, kugombania kisichotosha.


Na Hobbes huyu anaamini, kutokana na hatari hii, basi, jukumu muhimu na kubwa kwa Serikali yeyote ile iwe ni kulinda amani ya nchi. Kwamba kwa kutofanya hivyo, jamii itarudi katika hali ya kutokuwa na taratibu; vurugu, kuuana, umasikini na kupelekea maisha mafupi.


Hata hivyo, tunaamini pia, kuwa siku zote, pasipo haki na usawa hakuna amani, ingawa, katika jamii yeyote ile, uwepo wa amani na utulivu ni msingi mzuri katika kutafuta haki na usawa, kwa njia ya majadiliano. ( Hii ni sehemu ya makala yangu kwenye Mwananchi, leo Jumapili)

Maggid Mjengwa,
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio
Huwa sikubaliani na Hobbes and Locke philosophies.

Sababu siyo kugombania kisichotosha ... sababu kubwa ni UBINAFSI.
Bila ubinafsi, ugomvi hautakuwepo hata kama hamna mali yeyote. Mfano mzuri ni binadamu wanaoishi sehemu zenye maafa ya njaa huishi kama ndugu na huzika wenzao kwa pamoja NA KUSAIDIANA.

Binadamu wanaioshi penye neema, hugomban a na hata kuuana kirahisi mno!! ... sababu, ubinafsi.

Tafakari tafadhali.
 

Ndugu zangu,

KWETU wanadamu, mengi yanayotufanya tufarakane na hata kugombana yanatokana na sisi wenyewe wanadamu. Na ndivyo ilivyo hata kwa ndege na wanyama.

Ukiwaona ndege wanagombana, ukiwaona kuku wanagombana, na hata ng'ombe, basi, sababu kubwa ni ya viumbe hao wenyewe. Na mara nyingi, kugombana huku hutokana na kugombania kisichotosha.



Hivyo basi, suluhu ya yale tunayogombania kama wanadamu yapaswa itokane na sisi wanadamu wenyewe. Na tangu karne ya 17 kuna wanadamu walioliona hili.



Mwanafalsafa Thomas Hobbes alibainisha, kuwa migogoro mingi miongoni mwetu hutokana na ushindani wa kugombania kisichotosha. Kwa vile sote tuna mahitaji yenye kufanana, basi, Thomas Hobbes anasema, kuwa migogoro hii itaendelea, kugombania kisichotosha.



Na Hobbes huyu anaamini, kutokana na hatari hii, basi, jukumu muhimu na kubwa kwa Serikali yeyote ile iwe ni kulinda amani ya nchi. Kwamba kwa kutofanya hivyo, jamii itarudi katika hali ya kutokuwa na taratibu; vurugu, kuuana, umasikini na kupelekea maisha mafupi.



Hata hivyo, tunaamini pia, kuwa siku zote, pasipo haki na usawa hakuna amani, ingawa, katika jamii yeyote ile, uwepo wa amani na utulivu ni msingi mzuri katika kutafuta haki na usawa, kwa njia ya majadiliano.
( Hii ni sehemu ya makala yangu kwenye Mwananchi, leo Jumapili)

Maggid Mjengwa,
0754 678 252
MjengwaBlog :: Habari, Picha, Matangazo na Matukio

Lile la Ludovicky bado hujamaliza sasa umerukia lingine!!!
Watu bado hawakuamini wewe na Ludovicky!!! Saidiana na hao Mashemeji wa nje!!!
 
Kobello,

Asante sana.
Na ubinafsi hupelekea kile kisichotosha kiwe kidogo zaidi.
Maggid


Huwa sikubaliani na Hobbes and Locke philosophies.

Sababu siyo kugombania kisichotosha ... sababu kubwa ni UBINAFSI.
Bila ubinafsi, ugomvi hautakuwepo hata kama hamna mali yeyote. Mfano mzuri ni binadamu wanaoishi sehemu zenye maafa ya njaa huishi kama ndugu na huzika wenzao kwa pamoja NA KUSAIDIANA.

Binadamu wanaioshi penye neema, hugomban a na hata kuuana kirahisi mno!! ... sababu, ubinafsi.

Tafakari tafadhali.
 
Mzee wa tathmini, ye hachangiagi thredi yeyote, huwa anakujaga kuwabandikia lithredi na harudi kuangalia mmejibu nini.
 
Huyu jamaa ni mwingi wa porojo, mwenyewe anajiona strategist sana.Nadhania kw akiasi cha kujitamani mwenyewe.

Vipi hapa mbona hujaanza weka vionjo vyako?Au huja synchromise na makao makuu ya inteligentia na propaganda?Wewe ni mmojawapo ya walioharibiwa invetment zao na badger.Wekeza tuu,ila omba sana upewe ukuu wa wilaya au uandishi waikulu sasa hivi kabla siku hazijaisha kwani hamta kuwa tena na hii nafasi.Unahitaji ubabane na wengine ktk hii narrow time slice.


Usiogope tafuta hata nafsi isiyo ya fan yako, km novice wanapofany ahta kazi za kupaka rangi wakati wao ni madakatari by profession.Au unasubiri nianzishe bima kwa wanaCCM wanaowekeza hadi sasa ktk miundombinu ya CCM.
 
Back
Top Bottom